Tuesday, September 08, 2009

Steven Kanumba Chini ya Macho ya BIG BROTHER


Wadau, mcheza sinema maarufu wa Tanzania, Steven Kanumba aka. Denzel wa Tanzania alikuwa ndani ya nyumba ya Big Brother huko Afrika Kusini kama STARMATE. Alikuwa pamoja na wasanii wengine kutoka nchi zingine za Afrika. Kazi yao ilikuwa kuwakaribisha washiriki wa mwaka huu.

Nashukuru hakutuaibisha huko kama yule kijana, Richard, aliyedhalilisha akina dada na kuwafanyia 'mbaya' wakiwa wamelewa. Richard alishinda lakini bado anazungumzwa kwa uonevu aliyofanya.

Mnaweza Big Brother Africa 4 HAPA:
http://www.bigbrotherafrica.com/

**********************************************************************
The Starmates are Out!

"Please bring them girls. At least three.." -Kanumba

After two fun-packed days in the house, the Starmates say their goodbyes to the Housemates. What will life in the house be like without the Starmates and especially the women?In a group diary session, Big Brother asked the Starmates what they think will happen after they leave the house. Nonhle pointed out that the food would be a problem as some Housemates ate more than others. She also wondered who would prepare the food in their absence.Khanyi thought that conflict would ensue in the coming week as Housemates were panicking about who to align themselves with. “Some of them have even pulled me to a corner to ask me what I think they should say in the diary room” she added.

Steve, however, thought there was more harmony than conflict in the house and that Housemates were behaving like a “family”. He had one request to Biggie though: “Please bring them girls. At least three”. Nonhle also added that some Housemates had mentioned that they were hoping to find love in the Big Brother house.When asked which Housemate they think will win the ultimate prize?Khanyi: “Teddy from Kenya AKA “Teddy Bear” because he keeps a low profileNonhle: “Leonel because “he is the most quiet and is not opinionated”.”Steven: “Itai from Zimbabwe because he’s very natural. Not fake”Tuvi: “Itai from Zim”


Kutoka Bongo 5

Shindano la nne la Big Brother limeanza jana jijini Johannesburg kwa mbwembwe za hali ya juu huku mabadiliko makubwa yakijitokeza kama kauli mbiu yao "mapinduzi" isemavyo.
Moja ya vivutio vikubwa katika uzinduzi wa shindano hilo ni pamoja na uhusishwaji wa mastaa wa tasnia ya filamu barani Afrika ambapo msanii Kanumba wa Tanzania aliungana na mastaa wengine watatu katika jumba hilo kuwakaribisha washiriki 11 kati ya washiriki 14 wanaotakiwa katika nyumba hiyo.

Moja ya mambo yaliyostua wadau na wapenzi wengi wa shindano hilo la Big Brother Revolution 2009 ni pamoja na kutoingia kwa washindani 3 wa nchi za Tanzania, Angola na Zambia kitendo kilichotafsiriwa na wengi ya kuwa huenda Kanumba ndiye mshiriki kamili wa Tanzania. Akizungumza katika hafla ya Uzinduzi huo meneja masoko wa kampuni ya Multi Choice Tanzania aliwataka watanzania kuwa na subira ili kujua hatma ya ushiriki wao.
Uzinduzi huo ambao uliongozwa na MC mahiri kabisa IK kutoka nchini Nigeria ilipambwa na burudani toka kwa K'naan na pia ilikuwa na surprise ya washiriki mapacha kutoka Namibia pamoja na washiriki mmoja mmoja zaidi kutoka Kenya na Uganda.

Aidha washiriki wote 12 walioingia ni wanaume na waliobaki inasemekana ni wanawake hivyo kuweka shauku ya hali ya juu kwa watazamaji wa shindano hilo.

7 comments:

Anonymous said...

Kanumba alituangusha kwa lugha. Hajui kuongea kiingereza. Kama anataka kuwa superstaa aka Denzeli basi ajifunze English!

Anonymous said...

Yaani Da Chemi umenifurahisha!
kweli watanzania mwalimu wao alikuwa kipofu! Richard mpaka sasa wanamuona wa maana sana kisa ameshinda na anajua kiingereza!, wamesahau ufuska aliouonyesha kama nao ni aibu kwetu sote. Wamemsakama Kanumba kuwa alituangusha kisha kiingereza hivi ni kweli na haki mtu kama anastahiki kuwa mahali fulani asipewe nafasi sababu hajui kiingereza?!

Anonymous said...

akikaa na wapopo )wanaijeria) wake anakreim inglish kwenye maigizo yao,basi mtaani fujo tupu anajifanya anajua kiinglish,sasa watu washajua black and white, mtu mzima kaumbuka. nadhani sasa ataacha yale mambo ya kuchomeka maneno ya kiinglishi ktk interview za kiswahili.

Anonymous said...

Anony 6:41 hiyo stahiki unayozungumzia ni ipi kwa Kanumba? Lugha ya kwenye hilo jumba ni kingereza sasa kama hujui lugha kwa ufasaha unabakia kusema "I does, I does" utasema hapo unastahiki? Si kwamba umebebwa na umechukua stahiki ya mwingine? Haya ya kubebana ndo yametufikisha hapa tulipo ufisadi kila kona bongo.

Anonymous said...

Clearly "Talent" is something that is far fetched in this fellow's work. Having the lead role in a self written, self directed, self produced low budget (or maybe no budget) film is not exactly what people would call having talent; least to say skill.... do something else Sir... you and your fellow "Tanzanian celebrities" are going a great job at mocking the entertainment industry and the nation... word of advise.. have you thought of indulging in large scale agriculture... or rather compost manure production... coz you full of it!

John Mwaipopo said...

I think the anon of 8:26 PM has a point. Kanumba is only an anthill where there are no mountains thus we call him a star. the film industry in bongo is just emerging and we have stars who copy Nigerian films in Kiswahili. our 'stars' have a long way to go and many rivers to cross before we call the stars.

Anonymous said...

Suala liko katika uteuzi sio kizungu. BB inaendeshwa kwa kingereza. Kanumba kujua ama kutokujua kingereza sio ishu kwangu kwani ndio majaaliwa yake. ishu iko katika uteuzi. kwa kuwa BB inaendeshwa kwa kingereza basi angetafutwa mtu anayeongea kingereza, kama ilikuwa lazima saaaana tanzania itoe celebrity. Vingineyo kanumba kachukua nafasi ya mtu mwingine.(je kulikuwa na namna?) Pia kanumba hajafikia ustaa wa kualikwa kwenye suala la afrika nzima. Ni staa wa Dar es salaam labda na kibaha hivi ukienda mbali sana labda bagamoyo, basi.