Friday, March 18, 2011

Lowassa Naye Apata Dawa ya Babu Loliondo

Bila shaka mmesikia habari za dawa ya Loliondo. Kuna mchungaji mstaafu ambaye amegundua dawa ya mitishamba inayotibu magonjwa karibu yote. Watu wanahaha kwenda Loliondo, wengine wamekodi hata helikopta! Na serikali ya Tanzania imebariki dawa ya babu! Sasa wagonjwa wanatoroka Muhimbili kwenda kufuata dawa Loliondo!

*****************************************************************************


Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapile aka. BABU akipima dozi

Msongamano wa wangonjwa na wananchi wakienda kupata dosi. Dozi ilikuwa shs 500/- tu. Sijui kwa sasa ni bei gani.

Picha na Habari kutoka Michuzi blog:

Lowassa apata kikombe Loliondo, huduma zaimarishwa, bei ya mabasi Ubungo zapanda
Source: Gazeti la Mwananchi

WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa juzi alipata tiba ya magonjwa sugu inayotolewa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapile katika Kijiji cha Samunge, Tarafa ya Sale, Loliondo, mkoani Arusha.

Lowassa alifika katika eneo hilo mchana akiwa na viongozi kadhaa wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro na Serikali kisha kupata kikombe kimoja chenye dawa kinachotolewa na mchungaji huyo kwa ajili ya tiba.

Tofauti na viongozi wengine, Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli (CCM), Jimbo linalopakana na Kijiji cha Samunge, alikwenda huko akiwa na viongozi mbalimbali wakiwamo viongozi wa dini na baadhi ya wapigakura wake.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Lowassa alithibitisha kwenda Loliondo na kuwataja viongozi wa dini alioambatana nao katika msafara wake kuwa ni Askofu Msaidizi wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini, Dk Frederick Shoo na Mkuu wa Jimbo la Masai Kaskazini, Dayosisi ya Kaskazini Kati (Arusha), Mchungaji John Nangole.
Katika ramani ya utendaji kazi ya KKKT, Jimbo la Masai Kaskazini ndipo kilipo Kijiji cha Samunge ambako ni makazi ya Mchungaji Mwasapile.

“Ni kweli, nimekwenda pale na wapigakura wangu pamoja na viongozi wa dini, Msaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini, Dk Shoo na Mkuu wa Jimbo la Masai Kaskazini, Mchungaji Nangole,” alisema Lowassa na kuuliza: “Kwani hiyo nayo ni habari jamani?”

Baada ya Lowassa kufika katika kijiji hicho akiwa na ujumbe wake, aliongoza moja kwa moja hadi kwa Mchungaji Mwasapile na kuzungumza naye kisha akapata kikombe cha tiba na kuondoka.

Kabla ya Lowassa kwenda kupata tiba, amekuwa akitoa msaada wa nauli kwa wagonjwa mbalimbali wa jimbo lake kwenda kwa mchungaji huyo ambaye dawa yake inadaiwa kutibu magonjwa ya saratani, kisukari, pumu, shinikizo la damu na Ukimwi.

Kwa habari zaidi BOFYA HAPA:

Wednesday, March 16, 2011

Nyoka Auma Titi la Supamodo...Afa Dunia!

Wadau hebu cheki jinsi huyo supamodo wa Israel, Orit Fox, anayojaribu kulamba na kubusu nyoka! Kwanza anajifanya kama anataka kufanya mapenzi na huyo nyoka aina ya boa (kama chatu). Nyoka anachukia anamwuma kwenye titi. Kumbe titi ni zile puto zilizojaa silicone. Siku hizi ni fesheni kwa wazungu na hata weusi wenye matiti madogo kwenda kwa daktari ili wawekewe hizo puto matiti yao yawe makubwa zaidi. Nasikia zinauma. Wanasema hiyo silicone ilimwua nyoka baadaye! BORA! Bi Fox ni mzima ila inabidi abadilishwe puto kwenye titi.



Kwa habari zaidi someni:

http://www.hindustantimes.com/Snake-bites-model-s-breasts-dies/Article1-673607.aspx#

Tuesday, March 15, 2011

Isaidie Sinema ya Weusi - Picture Me Blue No More

Lazima niwasifu hao weusi wa Atlanta. Wanataka kutengeneza sinema ambayo naona itakuwa nzuri kuliko Precious.

Wanafanya kampeni wenyewe ili kupata pesa za kuitengeneza. Ukitaka kuchangia unaweza. Mchango unaanza kwa dola $5 tu!

Niliwasiliana nao, nikawaambia kwa nini wasimwombe Oprah awasaidie. Walisema wamemtumia ujumbe mara nyingi lakini hawapati majibu. Hata ile sinema ya Precious ilikuwa hivyo hivyo ila ilipopata huko Sundance Film Festival maarufu Oprah na Tyler Perry walikuwa mstari wa mbele kuisukuma.

Mwaka huu kulikuwa hakuna sinema ya weusi wala waigizaji weusi waliyofanikiwa kuingia katika mashindano ya Oscars. Perla Fay Humphrey na kampuni yake OnyxPearl wakifanikiwa kutengeza hii sinema huenda mwaka 2013 ndo itakuwa sinema ya weusi inayoongoza.

Natumaini watafanikiwa na lazima niseme ni mara chache kuona waMarekani weusi wenye moyo wa kufanikiwa kutengeneza sinema ya hali ya juu kama hii. Mungu yu mwema watafanikiwa.
Nilisikia habari za mpango wa kutengeza hii sinema mwaka jana Agosti walipokuwa na Casting Call kutafuta waigizaji. Ubaya ilikuwa Atlanta na Los Angeles hivyo nilishindwa kwenda. Kuna kikundi ha waigizaji weusi kutoka hapa Boston ambao walisoma vipande vya script na wali-blow kwa ilivyo nzuri.

Sinema Picture Me Blue No More itahusu maisha ya mtoto wa kike maskini huko Georgia ambaye anafanikiwa kwenda Chuo Kikuu na kuwa na maisha bora ingawa aliishi katika dhiki, uonevu, kubakwa nk.

Mnaweza kupata habari za kampeni yao HAPA:

http://www.onyxpearl.com/picturemebluenomore/

Mimi katika Mchezo- 'The Vagina Monologues'

Washiriki wa Boston Community Production of The Vagina Monologues 2011

Wikiendi iliyopita nilishiriki katika Mchezo wa Kuigiza, The Vagina Monologues (Maongezi ya Uke ..nishahishe kama nimekosea kutafsiri).

Kila mwaka vikundi vya wanawake hapa Marekani na nchi nyingi duniani wanasoma na kuigiza huo mchezo mwezi Machi. Hela wanazopata kutoka kwenye viingilio na mauzo ya chakula zinakwenda kusaidia vyama, mashirika yanayosaidia akina mama. Machi ni mwezi ya Wanawake duniani.

The Vagina Monologues ni hadithi fupi mbalimbali zinazotokana na mahojiano aliyofanya Bi Eve Ensler na wanawake kadhaa kuhusu nyeti zao. Kulikuwa na maongezi ya Bi Kizee, Shoga, Mke, Uke uliyokasirika, Mwanamke aliyedhani kapoteza kiharage chake, Kubalehe, Kubakwa, Kutairiwa, na mengine.

Kwa kweli nimetokea kufurahia huo mchezo na hata wanaume niliyowaalika waliyoenda wameipenda sana. Imewafanya wafikirie haki za akina mama na pia jinsi akina mama wanavyoona maswala kama uke zao, ngono, kunyanyyawa kijinisia.

Tanzania kuna hadithi nyingi sana ambazo zinaweza kuingizwa katika huo mchezo.

Mnauliza niliongelea nini? Nililionogelea uzazi, jinsi mwanamke anavyokuwa na uchungu katika uzazi na jinsi uke unavyofunguka ili mtoto atoke.

Monday, March 14, 2011

Aibu Huko Uwanja wa Ndege wa Iringa

Hii ni gari pekee linalotumika na kikosi cha zimamoto katika uwanja wa ndege wa Nduli mkoani Iringa. (picha kwa hisani ya Mdau Francis Godwin)
Wadau, hii picha aliiposti kaka Michuzi mwezi uliyopita. Bado huo uwanja hawajaongezewa vifaa. Je, wabunge wa mkoa wa Iringa wataongelea swala huu katika Bunge ijayo? Mimi natoka mkoa wa Iringa na kwa kweli naona aibu sana. Hiyo pick-up inaweza kubeba maji kiasi gani? Je, inakaa uwanjani au inatumika kufanya shghuli zingine mfano kupeleka watoto shule, mama sokoni, kimada gesti..... Huu ni swala nzito sana. Ina maana ndege ikianguka huko ndo basi tena.

Swahili Night Stockholm


Saturday, March 12, 2011

Blogu Mpya - Tembea Tanzania

Kuna Blogu mpya kuhusu sekta ya Utalii Tanzania inaitwa:

TEMBEA TANZANIA.

**************************************************

Naomba kuchukua fursa hii kuitambulisha kwako Blog ya Tembea Tanzania
(http://tembeatz.blogspot.com/) Blog ya Kitanzania yenye kubeba habari mbali
mbali zinazohusu sekta ya Utalii ya hapa Nyumbani Tanzania.

Shukran na karibuni nyote

KK

Barabara ya Serengeti

Duh! Dunia ya kimataifa inapinga mpango wa kujenga barabara kwenye hifadhi ya Serengeti. Je, watatoa hela ili hiyo barabara ipite kwingine?

http://www.msnbc.msn.com/id/21134540/vp/42026864#40817595

Tuesday, March 08, 2011

Majita Inakuhitaji Sasa

ITIKIA WITO: MAJITA INAKUHITAJI SASA!


Tumia utaalamu na uwezo wako wa uelevu wa hali halisi ya Majita, kuihudumia Majita, kwa maslahi ya Majita!

Nani? Wewe unayetoka Majita, Musoma, popote pale ulipo – hasa uliyestaafu.

Sababu? Kuiendeleza sehemu ya Majita ukijitolea katika kubuni, kupanga, kutekeleza, kupanua na kutathimini mradi-kusudiwa wa maendeleo–ambatana, ambao utakuwa ni ‘not-for-profit NGO’: Majita Integrated Rural Development Initiative.

Ujuzi? Dini, Kilimo, Komputa, Madini, Maji, Mazingira, Menejimenti, Miundombinu, Mistu, Nishati, Sheria, Takwimu, Ualimu, Uandishi/Utangazaji, Uchukuzi/Usafirishaji, Udaktari/Afya, Ufugaji, Ufundi/Ujenzi, Uhasibu, Ukarani, Upishi, Utalii, Utamaduni, Uvuvi . . . . na kadhalika.

Lini?
Mara moja . . . . Sasa hivi . . . . Leo!

Wapi? Ki-jadi, walipanga, walibuni, walitekeleza, walipanua na walitathimini mikakati kama hii, wakikutana uso kwa uso wakikaa chini ya mti (orality culture). Wakati wa mashini (industrial culture), wanagawana umbali wa kusafiri na kukutana katikati ya nchi ( Canberra , Lilongwe , Rawalpindi , Brasilia, Dodoma ). Tulio na bahati ya mtandao (digital culture), tumewezeshwa kufanikiwa kukutana ‘instantaneously’, kana kwamba tumo katika ‘global village’.

E-Mail? romuinja@yahoo.com (au) MUJUNGU@unhcr.org


Omurimu ogukomera gutakorelwe!
Bhamugaire, najayo!

‘If it is to be, it is up to me.

Wafungwa wa Kike Tanganyika

Hii picha ya Wafungwa wa Kike, ulipigwa mwaka 1895, Dar es Salaam, Tanganyika. Sijui walikosa nini maskini!

Mnaweza kuiona hapa:
http://www.zazzle.com/women_convicts_tanganyika_1895_poster-228015262999522213

Waganga wa Kienyeji wa Tanganyika



Hii picha imepigwa Tanganyika mwaka 1936. Sijui ni waganga wa kienyeji wa kabi la gani. Picha inapatikana hapa:http://www.fotosearch.com/IST515/1631353/

Leo ni Sikukuu ya Wanawake Duniani


Monday, March 07, 2011

Simba Hajatoroka Dar es Salaam Zoo!

Kumbe ule uzushi kuwa simba wa Dar es Salaam katoroka na anazurura mjini Dar es Salaam si kweli! Ifuatayo ni Tamko Rasmi kutoka Dar es Salaam Zoo
**********************************************************************
Habari

Napenda kuchukua nafasi hii kuwataarifu wananchi wa maeneo ya kibanda, kigamboni na maeneo ya jirani na Zoo na Dar es Salaam nzima kwa Ujumla, Kua Taarifa za kutoroka kwa kati ya Simba wetu kwenye Zoo sio za kweli.

Simba wetu wote wako salama pamoja na Wanyama wengine wote. Simba alie patikana maeneo ya Mbagala na huyo mwingine anaesemekana kuepo maeneo ya huko hatoki kwenye Zoo yetu.
Kuhusisha Dar esSalaam Zoo na wanyama hao ni Uzushi na Tetesi za mtaani.

Karibuni Sana Dar es Salaam Zoo
Akhsanteni Sana.

Mr. Salim Hassan
Marketing manager
Dar Es Salaam Zoo
+255 784 524285

Saturday, March 05, 2011

Idi Amin Alitabiri Marekani Itakuwa na Rais Mweusi



Doh! Kumbe Idi Amin alitabiri Marekani itakuwa na rais mwuesi. Jamaa alikuwa haogopi kusema wazungu!

Jessica Tata Anatafutwa na FBI/Interpol Kwa ajili ya Mauji

(Pichani Jessica Tata)

Jessica Tata (22) Mmarekani mwenye asili ya Nigeria anatafutwa na polisi kwa makosa ya kuua watoto wadogo wanne huko Houston, Texas.

Jessica alikuwa na Day Care nyumbani kwake. Kulikuwa na watoto wadogo saba mle wote chini ya miaka mitatu. Aliwaaacha wenyewe na kwenda dukani. Alivyorudi alikuwa nyumba yake inaungua moto. Aliwadanganya polisi kuwa alikuwa chooni nyumbani wakati wote kumbe mwongo! Hakufungwa jela kwa vile polisi hawakutegemea kuwa angekimbia.

Hivi sasa Jessica Tata yuko katika orodha ya wahalifu wakuu 15 wa U.S. Marshals (Top 15 Most Wanted List). Wana hisi kuwa amekimbilia Nigeria kwa ndugu zake.

Mkimwona huyo mwanamke mshenzi wajulishe U.S. Marshals au Interpol!

Mungu alaze roho za hao malaika mbinguni. Amen.

Mnaweza kuona Poster Hapa: http://www.usmarshals.gov/investigations/most_wanted/tata/tata15.pdf

***********************************************************************

Kutoka CNN.COM

(CNN) -- A Houston day care owner is among the U.S. Marshals Service's "most wanted," more than a week after authorities say she carelessly started a fire that killed four children and then fled.

The federal agency on Friday added Jessica Tata to its "15 Most Wanted" fugitive list, cautioning the public that she should be considered "armed and dangerous."

Houston fire department investigators twice tried to talk to the 22-year-old Tata on February 25, the day after the blaze in which seven children were trapped inside the home day care, according to a press release Friday from the U.S. Marshals. She initially refused and then, later that day, referred all questions to her lawyer -- the last known contact between her and law enforcement.

A U.S. Marshals task force later discovered that Tata flew to Georgia on Sunday, and officials have said they believe she may have gone on to Nigeria.

She subsequently was charged with six counts of reckless injury to a child, three counts of abandoning a child under 15 and four counts of manslaughter -- one apiece for the four children's deaths. Another three children were injured, but survived.

In addition, the U.S. Marshals release notes that Tata is also wanted for "unlawful flight to avoid prosecution."

Houston Fire Chief Terry Garrison said Wednesday that the department trusted the day care center operator after she told authorities she would talk about the fatal fire.

He told reporters that investigators initially believed Tata, who was upset at the fire scene, was a victim. She did not say much at the scene or the hospital.

"What she told us was not truthful," said Garrison, adding that investigators did not learn that until later. Tata said she was in the center's bathroom, the chief said. Witnesses contradicted that account, according to an arrest affidavit.

Tata left the seven children unsupervised in the home day-care facility and drove off in her car, according to the affidavit.

The blaze likely originated on an electric stove, which was on and had a pot on it containing oil, according to Houston Fire Department arson investigator Thomas Wood. A definitive cause for the fire will be announced once the investigation is complete.

Neighbors John Chestnut and Geoffrey Deshano told investigators that they heard Tata screaming soon after she pulled into her driveway and went to the front door, the arrest affidavit said. No other adults or day care employees were at the facility, the men said.

The two told reporters that Tata's car was full of groceries when she returned to the house, adding that they called 911 and tried to help get the children out as smoke seeped from the building.

Investigators said they did not believe Tata to be a flight risk.

"Somewhere along the way, we may have made a mistake," Garrison said. "We're going to learn from our mistake. We're not going to blame anybody. We're not going to make excuses."

Wednesday, March 02, 2011

Kumbukumbu - Mwalimu Matthew Douglas Ramadhani

(pichani Mwalimu Mathew Douglas Ramadhani 1915-1961)

50th DEATH ANNIVERSARY: Meet Mwl Mathew Douglas Ramadhani

By a Correspondent, 28th February 2011

IT is 50 years today since Mwalimu Mathew Douglas Ramadhani died. Mwalimu Mathew was a man of many firsts – he was Tanzania’s first university graduate, first black education officer and first black secondary school headmaster.

Born on September 11, 1915 in Zanzibar, Mwalimu Mathew was the fifth out of 10 children of Mwalimu Augustino Ramadhani and Bibi Margaret Majaliwa. Mwalimu Augustino was the founder and the first president of the African Association (AA) of Zanzibar in 1936.

Mwl Mathew got his education at St Paul’s High School in Zanzibar from September, 1925 to July, 1931, when he completed Standard Six and proceeded to St Andrew’s College, Minaki, Kisarawe, where he obtained the Grade I Teachers’ Certificate in 1936. At Minaki, for three consecutive years, he was the Head Prefect.

He then went to Makerere College, Uganda, for two years and obtained the Cambridge School Certificate in 1938.

Because of his father’s death on August 28, 1938, he was permitted by the Director of Education of Tanganyika, who had sponsored him, to terminate his studies in Makerere and to return to Zanzibar to teach at St Paul’s High School, Kiungani, since the school had a majority of pupils from Tanga.

On September 6, 1942, he married Bridget Anne Constance Masoud, a fellow teacher who qualified in 1940 at Kitchwele Girls School, Dar es Salaam.

Five years later, in September, 1947, Mwalimu Mathew obtained a two-year Colonial Development and Welfare Scholarship for Zanzibar and went to the London Institute of Education where he obtained a Teachers’ Professional Certificate in 1948.

He was advised to proceed to a three year degree course as it would be difficult to return to England for a degree. However, the Zanzibar Government was reluctant to sponsor him beyond the initial two years.

One of the reasons given was that the government could not guarantee an employment for him as a graduate! Nevertheless, he went ahead using the funds of the remaining one year of scholarship.

He proceeded to Sheffield University where he studied English, Geography, Mathematics and Economics.

He then toiled for his second under graduate year by washing dishes in hotels and restaurants. His eldest brother, Francis Cecil Ramadhani, contributed immensely by looking after Mathew’s family of a wife and three children: Marina, Augustino and Henry.

However, he was lucky to secure a Colonial Development and Welfare Scholarship for Tanganyika for his third year and he graduated with B.A. (Econ) in 1951.

Because of the scholarship for the third year, he was required to work in Tanganyika for at least three years and he was to teach at St Andrew’s College, Minaki, Kisarawe.

However, a misunderstanding over the terms of service led him to join the Department of Education of Tanganyika as an Assistant Education Officer, though a graduate and was posted to Mpwapwa Secondary School in April, 1952.

On June 9, 1953, he was promoted as an education officer and was posted to Tabora Senior Boys’ Secondary School as a teacher from January 1954 to December 1958, when he returned to Mpwapwa as the Headmaster.

In September 1960, he went to Manchester University for further studies and met his death in a train accident at Guidebridge Station, Ashton-under-Lyne, on March 1, 1961, leaving behind a widow and eight children.

He was buried a week later at the Southern Grave Yard, Manchester, after the Government of Tanganyika decided not to bring his body back home.

The late Mwalimu Julius Kambarage Nyerere had all through wanted Mwalimu Mathew to resign from teaching and assist the late Mzee Abeid Amani Karume in the fight for the independence of Zanzibar.

Every time Mwl Nyerere was in Tabora he sent a taxi at night to pick Mwalimu Mathew for a discussion. However, Mwalimu Mathew was reluctant to join Zanzibar politics. There will be a service at the All Saints Cathedral at Vinghawe, Mpwapwa, where the Bishop’s throne and Canons stalls will be consecrated in his memory.

MAY HIS SOUL REST IN PEACE - AMEN

Tuesday, March 01, 2011

Askari Wa Vita Vya Kwanza ya Dunia - German East Africa

Hii ni meli ya kivita Mjerumani SMS Konisberg ikiwa imita nanga bandarini Bagamoyo. Bagamoyo ilikuwa mji mkuu wa Tanganyika enzi za MJerumani
Askari kwenye foleni
Waliopitia JKT wataelewa hii...ROUTE MARCH!

Sijui ni Tanga au Bagamoyo hapo au Itakuwa kwenye Ziwa Victoria au Nyasa

Hao watakuwa wale Asakri wa kwanza kabisa. Hawana viatu!

Askari wakisfisha bunduki zao

Enzi za MJerumani walikuwa wanatumia Rupia siyo Shilingi


Bahati mbaya hatuna majina ya hao Askari pichani



The Force Publique in German East Africa during World War One

Usafiri Enzi Za MJerumani

Mjerumani alivyotutawala hapakuwa na usafiri wa ndege. Walikuwa wanasafiri kwa meli. Hebu cheki hii tangazo la meli. Cheki waafrika wanavyofurahia kuona meli.

Ukitaka kuigiza Katika Sinema Hii ni Nafasi Yako!

Kama unataka kuwa Extra katika sinema, 'Here Comes the Boom' jiandikishe na Boston Casting. Lazima uwe na makaratasi. Utalipwa dola $100 kwa siku au zaidi kutegemeana na masaa unaokaa kwenye set. Pia kuna chakula na vinywaji tele. Sinema inakuwa filmed Maeneo ya Quincy, MA.



UPDATE - MORE VENUES!

Here Comes the Boom- OPEN CALLS!

Open Call for the film “Here Comes the Boom” starring Kevin James. We are looking for people of ALL TYPES (ages 18+) to be extras on the film that is shooting late March- Early June.
Please feel free to come to any of our open calls- you only need to attend one! Make sure to bring a photo!


OPEN CALL SCHEDULE:

Saturday March 5th
10am- 3pm
North Quincy High School
316 Hancock Street
Quincy, MA 02171

Saturday March 12th
10am- 3pm
Quixote Studios
184 Everett Street
Boston, MA 02134

Sunday March 20th
10am- 3pm
Burlington Mall
Middlesex Turnpike #130
Burlington, MA 01803

Sunday March 20th
10am- 3pm
VFW Lowell
190 Plain Street
Lowell, MA 01852

Saturday March 26th
10am- 3pm
South Shore Casting Studio
Hanover Mall
1775 Washington Street
Hanover, MA 02339

Please do not call venues directly, all questions should be directed to Ashley at Boston Casting 617-254-1001 ext. 3

LUKU Za TANESCO Zina Mambo!

Haya ni maoni ya mdau:

Nasikia "wajanja" wa Tanesco wana-program LUKU, wewe unalipa Shs 1,000 kwa mwezi lakini unapata umeme wa kuweza kuwasha tanuru (kama unalo).
Malipo tofauti mnalipana chembaz na programmer.

Habari hizi umeshazipata au wewe hawakukufundisha hii programming pale Chuo cha Tanesco.

Sasa kama Tanesco wananunua umeme Dowans na kukuuzia wewe, hasara na faida tunajua napata nani :-)

Maelezo zaidi kuhusu THAMANI na BEI utatupiga "tuisheni" baadaye :-)

Halafu mnataka kutulaumu sisi tulioko Florida ........ati makosa yetu hatukusomea Chuo cha Tanesco.

Hebu DM atufafanulie kama anaujua huu mpango wa ku-program LUKU za Tanesco ili kujipatia umeme wa chee.
Huu ndiyo mpango wa UMEME KWANZA kwani KILIMO KWANZA ni kwa ajili ya Ng'wakitolyo
Uchakachuaji hadi kwenye LUKU.
Tanesco pandisheni bei ya umeme, watumiaji tuna mbinu zetu .....mechi droo.
Sijui "kisowia" ni nani kati ya Tanesco na wateja?? :-)

Mdau O.S. M.