Thursday, July 10, 2008

Familia ya watumwa Marekani - 1862


Familia ya watumwa South Carolina, 1862.
(Picha iko kwenye maktaba ya Library of Congress)
Kuna kitu ambacho nalalamika sana hapa Marekani. Ni kwamba wengi wa waMarekani weusi wamesahau au hawataki kutambua asili yao ya Afrika. Ninfanya utafiti kwa ajili ya screenplay ambayo naandika. Nikaona hii picha iliyopigwa 1862, yaani miaka 146 iliyopita.
Ukitazama vizuri unaweza kusema ni waafrika kabisa. Naona hao walikuwa bado hwajachanganya damu na wazungu. WaMarekani weusi wengi ni weupe weupe shauri ya kuchanganya damu na wazungu. Leo utasikia waMarekani weusi wanatania, "She/He black like coal" Yaani mweusi kama mkaa. Na hao weusi tii wanadhauruliwa ile mbaya.

Kwa nini waMarekani weusi wengi wamechanganya damu? Wazungu walitembea sana na wanawake weusi na kuzaa nao enzi za utumwa. Enzi hizo uliweza kukuta Mzungu (Master) ana familia ya watoto wa kizungu na mke wake, na hapo kwenye backyard kazaa watoto kibao mashombe na mtumwa/watumwa wake. Wengine walitunza hao watoto vizuri kidogo kwa kuwapa nguo na chakula zaidi ya wengine. Master wengine waliona hao watoto sawa na watumwa wengine na kuwauza na kuwapiga na kuwatesa.
Si siri kuwa wazungu walitumia wanawake weusi kwa ajili ya raha zao za ngono na pia kujifunzia habari za ngono. Wanawake weusi wengine waliona sifa kuzaa na wazungu kuliko mweusi mwenzake maana alidhani mtoto atakuwa na maisha bora. Master wengine walisema kuwa wataua wanawake ambao hawazai watoto waliochanganya damu. Kweli ilikuwa balaa enzi hizo.

8 comments:

Anonymous said...

Dada Chemi, huyo aliyeshika mtoto anafanana sana na dada fulani nilisoma nae Kisutu.

Subi Nukta said...

Asante kwa kutusimulia kidogo ulichokipata katika fukua fukua zako kwenye maktaba. Elimu haina mwisho!

Simon Kitururu said...

Hata Afrika WEUSI ti , maeneo fulani wanaonekana wako kushoto.

Unafikiri kwanini kuna MKOROGO?

Mama yangu mwenyewe alibaguliwa enzi hizo alipopelekwa na baba kwenye familia yao ambao walikua wanajihisi wao weupe. Tatizo kwa baba likawa kwanini anataka kuoa mwanamke mweusi na wa kabila tofauti!Halafu hapo naongelea baba Mpare na mama Mjita na akija hata Muarabu anaweza kutoona tofauti katika rangi.

Wamarekani wengi rafiki zangu nachojua ,wanakwepa kujifanya Waafrika kwa sababu ya picha na televisheni zionyeshavyo Afrika.

Lakini nawajua mpaka WAETHIOPIA ambao hawataki kujulikana kama WAETHIOPIA kutokana na sifa ya ETHIOPIA kuwa karibu na kufakufa na NJAA.

Afrika inatangazwa kama sehemu ya shida na waafrika mapaka leo hii hatukawii kufananishwa na NYANI!

Si mpaka wiki hii tu bado tunapigania mpaka KATUNI za MEXIKO ziache kuchora WAAFRIKA kama NYANI?

Lakini Wamarekani WEUSI wengi ,Ukianza tu kuongelea mambo ambayo dunia nzima inatambua kwa MAZURI na kuheshimu kama Mandela, wote hujifanya kuwa wanauhusiano nayo.

Anonymous said...

Da Chemi, ni hadithi nzuri kweli kweli. Ila jambo moja umeshindwa kunishawishi, kwamba wazungu walikuwa wanawatumia wanawake wa kiafrika kujifunza ngono, No! wanawake wa kiafrika wanalipa, wana joto la kuridhisha, sio kama wanawake wa kizungu, ndio maana wanawake wa kiafrika wanapapatikiwa. Ila sema tu wanaona soo, lakini hata wewe hapo Marekani, usione hivyo kuna mizungu inakutamani na moyoni iansema "Ningelipata hili limama ingelifaudu" Bado mapenzi ya wazungu ni artifial sana na hata wanawake wa kizungu akipatwa na mwanaume wa kiafrika wanapenda sana. Sasa hivi kuna wimbi kubwa sana la wanawake wa kizungu kuja Afrika "kubakwa". Niposema kubakwa ni kwamba wanaume wa kiafrika hawaitaji starter wala nini, moto mara moja! Muulize dada Sudi

Anonymous said...

lakini mpaka leo tunaona ujanja kuwa na mzungu kumbe ni viumbe washenzi.kama ujakaa nao hutawajua maana wakija kwetu tunaona miungu watu na $ zao kumbe ni chui waliojivika ngozi ya kondoo

Anonymous said...

inasikitisha kusikia mtu mweusi anaona fahari kuwa mweupe kidogo,yaani yeye ndio bora kuliko watu weusi tii

Anonymous said...

asante kwa kutukumbusha kidogo tulikotoka, wengi wetu historia imepotea kabisa na kusahau taabu zilizowapata mababu zetu.

pia nimeshangaa jana rais wa fifa anasema kuwa wachezaji mpira wa miguu wanafanywa kama watumwa wa siku hizi. alikuwa anamzungumzia mchezaji nyota wa manchester united anaelilia ruhusa ili ajiunge na real madrid. sasa ni vizuri huyo rais na ronaldo wajue nini maana ya utumwa maana naona wanawakebehi mababu zetu.
ronaldo analipwa zaidi ya £120,000= kwa wiki na man united na anaishi jumba la kifahari, juzijuzi alikuwa holiday, wiki hii kafanyiwa op. ya mguu huko uholanzi na dokta bingwa duniani -bili kwa man united!!
babu zetu walikuwa wanalipwa kiasi gani na waliishi ktk mazingira gani? walipata muda wa holiday? walikuwa wanapata matibabu ya dokta bingwa? nani aliwalipia bili kama hiyo? huyu blatter na ronaldo wanatania kabisa, hawajui nini maana ya utumwa!!

anyway ...

(msomaji wako)

Anonymous said...

Huyo ni Mzee Musa wa Ilala fleti! Yaani wamefanana!