Thursday, June 25, 2009

Gavana wa South Carolina Atoroka na Kimada

Governor Mark Sanford (South Carolina)

Bila shaka mmesikia habari za Gavana wa South Carolina kupotea kwa siku kadhaa. Alivyotokea alisema kuwa eti alienda kutembea (hiking) kwenye milima ya Appalachian. Kumbe kuna mtu alimwona kwenye uwanja wa ndege akitokea Argentina na kampiga picha!

Hapo sasa ilibidi gavana aseme ukweli. Alienda Argentina kumfuata kimada wake. Kimada mwenyewe ni mwanamke kutoka huko Argentina. Anasema kuwa alimjua huyo mwanamke kwa miaka minane, lakini alianza uhusiano wa kimapenzi naye mwaka jana. Alisema alienda Argentina mara tatu kumwona. Gavana Sanford ana mke na watoto wanne wa kiume, lazima wameaibika.

Habari zinasema kuwa mke wake aligundua habari ya mume wake kutembea nje ya ndoa na kamfukuza ndani ya nyumba yao kama wiki mbili zilizopita! Na pia eti hizo safari za Argentina zimelipiwa na walipa kodi wa South Carolina! Hmmm, naona itabidi jamaa ajiuzulu.

Hapa Marekani ingawa watu wengi wanatembea nje ya ndoa zao ni mwiko na jambo la aibu. Inaweza kumwangusha mtu mkubwa mwenye cheo. Siyo kama nchi zingine amabako dume akitembea nje ya ndoa eti ni jambo lakujivunia na inaonyesha eti ni mwanaume!

Cha kuchekesha zaidi jamaa ni Republican. Hao Republican wanajidai watakatifu, wapenda familia wasio na makosa...kazi kusema wenzao! Kumbe wao ndo mabingwa wa kutembea nje, na uhuni mwingine!

Kwa habari zaidi someni:

http://www.cnn.com/2009/POLITICS/06/25/sanford.fallout/index.html

http://www.washingtonpost.com/wp-dyn/content/article/2009/06/24/AR2009062402504.html

http://www.mercurynews.com/politics/ci_12678735


******************************************************************

Kusoma habari ya e-mails za mapenzi kati ya Gavana na kimada soma hapa:

http://www.thestate.com/sanford/story/839350.html

http://www.cnn.com/2009/POLITICS/06/24/south.carolina.governor.emails/index.html

"I could digress and say that you have the ability to give magnificent gentle kisses, or that I love your tan lines or that I love the curve of your hips, the erotic beauty of you holding yourself (or two magnificent parts of yourself) in the faded glow of the night's light -- but hey, that would be going into sexual details ..."
"...while all the things above are all too true -- at the same time we are in a ... hopelessly impossible situation of love...." he added.


DUH!!!!!

4 comments:

Nautiakasi said...

Da Chemi mie huwa wanimaliza kwa maelezo yako tu...! Yaani nawamiss sana wamama wale mashankunaku wa mtaa Tandale kwa mtogole..Unasound kama wao wakati wakiwa kwenye baraza ya Mzee Kidire wakichapa soga na umbea jioni! Ole wako ukatize mitaa hiyo, utaanza kunangwa kuanzia viatu hadi unywele.. utajuuuuuuuta kupita!
Da Chemi keep it up wanipa raha mtoto wa mwanamke mwenzio!

Chemi Che-Mponda said...

Nautiakasi, umenifurahisha. Imebidi niji-imagine napita huko Tandale mitaani na khanga zangu tena ina bonge la fumbo. Nikisikia wananisema naongeza mbwembwe za kutembea huko nikisema...'mlie tu'!

Anonymous said...

hehe....nimejikuta nacheka bila kujizuia, nilidhani da chemi anataka kusema ''napita huko tandale mitaani na khanga zangu tena nina bonge la matako''...samahani lakini, usikwazike...ndiyo picha iliyonijia mara ya kwanza.
Da Chemi anajua sana udaku, kwa sisi tulio nje ya bongo huwa unatukumbusha home...Big love da Chemi

Anonymous said...

Inawezekana kifaa cha Argentina kilikuwa moto wa kuotea mbali ndo maana mzee mzima akawa hatulii USA. Ni masuala ya mapigo au?