Thursday, June 25, 2009

Tanzia - Michael Jackson

Michael Jackson 1958-2009

Wadau, watu wanashangaa na kulia. Michael Jackson amefariki dunia leo! Alikuwa anajiandaa kwa ajili ya concerts na watu walikuwa wanasubiri albamu yake mpya.

Taarifa ya habari inasema kuwa alifariki saa sita na dakika 20 (Pacific) mchana. Alikuwa ametoka kwenye mazoezi, ndipo alianguka. EMT's/911 waliitwa na walikuta hapumui na moyo umesimama. Walijitahidi kwa kila mbinu waliokuwa nayo kumfufua lakini wapi.

Michael atakuwa na imani sasa, maana maisha yake kwa kweli yalikuwa ya ajabu. Muziki wake ulipendwa lakini watu walibakia kushangaa jinsi alivyokuwa anaogea madawa ya bleaching (kujikrimu) mpaka kawa kama mzungu. Alifanya surgery usoni na kuchonga pua. Alikataa asili yake ya uafrika. Alisema kuwa anajitengeneza kuwa kama Mwenyezi Mungu alivyotaka awe. Na watu walisema, Michael, Mungu alikuumba alivyotaka yeye.

Tuache utani, na kumlaani sasa. Amefariki na familia yake, marafiki na mashabiki wake wamebakia na majonzi. Muziki wake utakumbukwa daima.

REST IN ETERNAL PEACE MICHAEL JACKSON
Kwa habari zaidi someni:

1 comment:

Fadhy Mtanga said...

Apumzike kwa amani mwanamuziki Michael Jackson. Amina.