Wednesday, May 21, 2008

Habari zaidi kuhusu Kifo cha Balali

Hayati Dk. Daudi Balali (picha kutoka Michuzi Blog)

Written by KLHN/Tanzania Daima

Wednesday, 21 May 2008

KLH News imeweza kuthibitisha kwa uhakika kuwa misa ya kumuombea Marehemu Balali inatarajiwa kufanyika saa nne asubuhi katika Kanisa la Mt. Stephen Washington DC. Kutoa heshima za mwisho kutafanyika katika kanisa hilo hilo na itakuwa si kwa hadhara nzima.

Mwili wake unatarajiwa kulazwa kaburini kwenye makaburi ya "Gate of Heaven" huko hukoJamaa wa karibu wa Ballali walioko Dar es Salaam na Washington walilithibitishia Tanzania Daima kuhusu kutokea kwa msiba huo.

“Ni kweli amefariki nyumbani kwake Ijumaa usiku. Na sasa hivi tuko katika maandalizi ya kwenda funeral home (taasisi ya kuandaa shughuli zote za mazishi) kwa ajili ya kuanza kufanya maandalizi kwa ajili ya msiba,” alisema ndugu wa karibu wa Ballali kutoka Washington.

Habari zaidi zinaeleza kwamba, tayari familia ya gavana huyo wa zamani wa BoT imeshaitaarifu serikali kuhusu kutokea kwa msiba huo na kwamba taarifa rasmi kuhusu kifo hicho zitatolewa leo hii.Ndugu mwingine wa karibu wa Ballali aliyezungumza na Tanzania Daima majira ya saa 4:00 usiku jana alisema mazishi ya gavana huyo wa zamani wa BoT yanatarajiwa kufanyika Ijumaa hii huko huko Marekani.

Mmoja wa wanasiasa aliye karibu na familia ya Ballali aliyezungumza na Tanzania Daima jana alithibitisha pia kupokea taarifa za kifo cha Ballali kutoka kwa mkewe, Anna Muganda. Ndugu mmoja wa Ballali alipoulizwa na Tanzania Daima sababu za kushindwa kutangazwa kwa taarifa za kifo hicho mapema alisema walilazimika kufanya hivyo ili wapate fursa ya kuwasiliana na serikali kwanza na kisha ndugu, jamaa na marafiki wa familia yao kabla ya habari hizo kusambazwa.

Badhi ya jamaa za Ballali waliozungumza na Tanzania Daima walisema kulikuwa na wasiwasi kwamba kifo cha gavana huyo wa zamani wa BoT kikawa kikawa si cha kawaida.“Kuna wasiwasi kwamba huenda alilishwa sumu wakati akiwa nchini mwaka jana na hili limekuwa likizungumzwa sana ndani ya familia,” alisema mmoja wa jamaa za karibu wa Ballali aliyezungumza na Tanzania Daima jana.

Taarifa za kuwapo kwa wasiwasi wa Ballali kulishwa sumu zilipata kusikika mwaka jana na wakati fulani ilielezwa kwamba alipelekwa Marekani kwa matibabu kutokana na sababu hizo.

Habari za kifo hicho cha Ballali ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Jakaya Kikwete Januari mwaka huu zimekuja siku chache tu baada ya serikali kupitia Ofisi ya Rais Ikulu kutoa tamko la kutangaza kwamba ilikuwa haimtafuti gavana huyo wa zamani wa BoT.

Tamko hilo la serikali lilitolewa mbele ya waandishi wa habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salvatory Rweyemamu.Rweyemamu alisema kuwa serikali ina mkono mrefu na iwapo itafikia hatua ya kumtafuta gavana huyo wa zamani wa BoT ili aje atoe maelezo yake kuhusu wizi wa zaidi ya shilingi bilioni 133 uliogundulika katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) haitashindwa kamwe kumfikia alipo.

Alisema kutokuwepo nchini kwa Ballai, au kutojulikana alipo, si jambo linaloisumbua serikali kwa sasa kwa sababu hivi sasa yeye ni raia wa kawaida, hivyo anao uhuru wa kuishi popote anapopenda.“Serikali haimtafuti Ballali (kwa sasa), lakini ikiamua kufanya hivyo haitashindwa.

Kwanza ni private citizen (raia huru) siyo mwajiriwa wa serikali tena,” alisema Rweyemamu na kuongeza kuwa, mkono wa serikali ni mrefu hautashindwa kumpata Ballali iwapo itamhitaji. kifafanua zaidi, alisema baada ya kutenguliwa kwa uteuzi wake, serikali iliunda timu ya kuwachunguza watuhumiwa wa EPA, kuhakikisha fedha zilizoibwa zinarudi na kuwachukulia hatua waliohusika, akiwemo Ballali.

Alisema: “Ninachofahamu ni kwamba, timu iliyopewa kazi kuhusu ubadhirifu wa EPA inaendelea na kazi yake na tunaona jinsi fedha zinavyorudishwa.”Mkurugenzi huyo pia alikiri kwamba serikali haifahamu hospitali aliyokuwa akitibiwa Ballali, licha ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo, kukaririwa akisema alimtafuta Ballali bila mafanikio alipokuwa jijini Washington, Marekani.

“Kwa kweli sifahamu hasa Ballali alikuwa akitibiwa katika hospitali gani, lakini najua alikuwa nchini Marekani katika Jimbo la Boston, ila hospitali kwa kweli siijui.“Lakini huyu ni mtu huru hivyo anaweza kuishi popote… huyu ana nyumba yake nchini Marekani… yupo huko anaishi na familia yake,” alisisitiza Rweymamu katika ufafanuzi wake.

Wiki iliyopita, ikiwa ni siku chache tu baada ya taarifa hiyo ya Ikulu, vyombo kadhaa vya habari viliandika habari zilizokuwa zikieleza kuwa makachero kutoka hapa nchini, walikuwa wamekwenda nchini Marekani katika miji ya Boston na Washington kufuatilia nyendo na maisha ya gavana huyo wa zamani.

Kwa mujibu wa habari hizo, ambazo zilikariri taarifa za ndani kutoka serikalini, makachero hao walikuwa wamekwenda huko ili kujua mahali anakoishi ili wakati wa kumhitaji utakapofika iwe rahisi kumpata. Ballali aliondoka nchini, Agosti mwaka jana kwenda Marekani kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kwa matibabu, na tangu wakati huo taarifa zake zilikuwa ni zenye utata mkubwa.

Mara ya mwisho kwa Ballali kuonekana hadharani ilikuwa ni Julai 12 mwaka jana alipozungumza na wanahabari na akasema alikuwa hatarajii kujiuzulu wadhifa wake kutokana na kukabiliwa na tuhuma za ubadhirifu.

Katika mkutano huo, Ballali alisema madai ya ubadhilifu yanayotolewa dhidi yake ni uzushi na uongo mtupu.Huku akionekana kujiamini alisema; “Niko Comfortable, moyo wangu mweupe, ari yangu ya kazi iko juu kwani tuhuma hizo ni uongo na uzushi mtupu na siwezi kujiuzulu kwa tuhuma zisizo na ushahidi.

“Tuhuma zote dhidi yangu ni za uongo mtupu. Kwanza sijui zimetoka wapi, nani mtunzi na kwanini amefanya hivyo. Hilo tunawaachia wanaofanya uchunguzi na naamini siku moja atajulikana na ukweli utajulikana, lakini mimi siwezi kujiuzulu kwa mambo ya uzushi,” alisisitiza.

Kashfa ya BoT kupitia mtandao wa Internet, uliibuliwa mara ya kwanza Bungeni na Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbroad Slaa (CHADEMA).Akichangia maoni ya kambi ya upinzani wakati wa mjadala wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya Fedha, Dk. Slaa alisema kambi ya upinzani imefarijika baada ya Waziri wa Fedha kukiri kufahamu taarifa aliyoitoa Bungeni kuhusu ubadhirifu mkubwa ndani ya BOT unaomgusa Ballali, pamoja na wafanya biashara wengine wakubwa akiwemo Mbunge wa Kwela, Dk. Chrisant Mzindakaya (CCM), kupitia kampuni anayoimiliki.

Dk. Slaa alisema Dk. Mzindakaya alichukua mkopo kwa shughuli za kampuni yake ya SAAFI wa sh 6.217 bilioni, uliogawanyika kama ifuatavyo. Alisema aliomba ‘Overdraft facility ya 450 millioni zitakazolipwa kwa miaka 5; mkopo wa shs 2.8 bilioni zitakazolipwa katika miaka mitano; na Dola za Marekani 2.528. Jumla yote ni Bilioni 6.217.

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, fedha zote zilikopwa Benki ya Standard Charter na Benki Kuu ilitoa (Guarantee) mdhamana wa asilimia 100. Mwaka huu wa 2007 Benki kuu kutokana na Mdhamana huo tayari imelipa kiasi cha sh 8.1 Billion kwa niaba ya Mzindakaya na fedha hizo pamoja na riba zinakisiwa kufikia 9.7 billioni hadi sasa (Hati ref. CIBD-14662 ya tarehe 24 May, 2007, na mkopo kutolewa 2005.

Kutokana na tuhuma hizo, Meghji wakati akifanya majumuisho ya hoja yake, alisema Serikali imeagiza kuanza kufanyika kwa uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha katika akaunti ya madeni ya biashara ya nje zinazoikabili Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Alikiri serikali kupata taarifa za kuwapo kwa vitendo vya rushwa na nyingine za matumizi mabaya ya fedha katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Waziri Meghji alisema, tayari alikuwa ameshamwagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Fedha za Serikali, kuanza uchunguzi kuhusu tuhuma hizo.Meghji alisema, serikali ilikuwa ikitarajia kukamilisha kazi hiyo na taarifa kamili ya uchunguzi huo kutangazwa ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Mbali ya BoT kutuhumiwa kutumia fedha nyingi kuliko inavyostahili katika ujenzi wa majengo yake mapya ya ‘minara miwili pacha’ (Twin Towers), kiasi cha Dola za Marekani milioni 30.8 sawa na shilingi bilioni 40 kinatuhumiwa kufujwa katika akaunti ya madeni ya biashara ya nje.

Taarifa zinaonyesha kuwa, wakopeshaji wa kimataifa kutoka nchi 12 waliingia mkataba wa kusimamia akaunti hiyo na kampuni ya Kitanzania ijulikanayo kwa jina la Kagoda Agriculture Ltd kati ya Septemba na Novermba mwaka jana.Uchunguzi wa awali wa wakaguzi wa nje wa mahesabu ya akaunti hiyo unaonyesha kuwapo kwa mazingira yenye utata mkubwa unaozingira makubaliano kati ya wakopeshaji na kampuni hiyo iliyolipwa dola milioni 30.8.

Akichangia hotuba ya Waziri Mkuu, Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe (CHADEMA) alihoji kwa nini Serikali ilikalia kimya suala la kashfa ya BoT mara baada ya habari za kashfa kutangazwa kupitia mtandao wa internet tangu Novemba 2006 na kuonya kuwa hali hiyo inaathali kubwa kiuchumi iwapo kashfa kama hizi zinaachwa bila ya ufuatiliaji wa serikali.

Taarifa za awali za uchunguzi huo zinaonyesha kuwa, BoT ilifikia hatua ya kuipa kampuni hiyo fedha zote hizo ikidai kuingia mkataba na wakopeshaji hao katika mazingira ambayo nyaraka zilizopatikana zinaonyesha kuwa na hitilafu nyingi.Miongoni mwa hitilafu zilizobainishwa katika uchunguzi wa awali ni, kukosekana kwa karatasi rasmi zenye majina ya makampuni hayo ya kimataifa.

9 comments:

Anonymous said...

I know exactly what my fellow tanzanians are thinking on mindboggling issues like this one.Some may not believe he is gone and are angry,some will believe but still angry and everyoneelse will be in between.Balali amejitakia mwenyewe he bought too much time contemplating when,whether or not and how to tell the truth.All he had to do is walk down to media offices with his two best lawyers and dish all the dirt out about who,when,how and how much as well as his position on the dirt.Instead he had to get a visa,get on the plane then go see kidosho WASHINGTON dc,then see mama watoto,then anazidiwa and kuacha kinote kwa mwanafamilia wa karibu.Yaani ameiface hii issue cowardly and childish.
Anyway my heart and prayers goes out to his family during this hard time and may he rest in peace
Mziwani pumbuj4
columbus.

Anonymous said...

REST IN PEACE GOVERNOR BALALLI!

Anonymous said...

noBiblia inasema

"Roho, nafsi itendayo dhambi, itakufa" (Ezek. 18:4)

Anonymous said...

Biblia inasema

"Roho, nafsi itendayo dhambi, itakufa" (Ezek. 18:4)

Anonymous said...

kalale pema peponi kamandaaa....

Anonymous said...

HABARI YA KAZI.

YAMESEMWA MENGI HAPA, KILA MTU AMEONGEA LAKE. LAKINI MI NIMESIKITISHWA NA WALA SITAKI KUAMINI HAYA MAMBO WATU WANAYOTAKA WATU WENGINE WAYAAMINI.

ETI KIFO CHA BALALI NI KUZIMA ISHU YA EPA? KAMA KWELI KUNA WATU WAMEFANYA HIVO WAKIAMINI KIFO CHAKE NDIO MWISHO WA EPA NAWAONEA HURUMA? NA WALA SITAKI WATANZANIA WENZANGU WAAMINISHWE HIVO.

NASEMA HIVI KWA SABABU ZANGU(INGAWA WENGINE HUENDA WASIKUBALIANE NAMI).

KWANZA
MIMI SIAMINI KAMA BALALI NDIO ALIKUA FUNDI MKUU(CHIEF ARCHITECT) WA MPANGO MZIMA WA MADUDU HAYA, LAZIMA KUNA WATU.(MIMI NAAMINI BALALI ALIKUA (MRATIBU)COORDINATOR TU.
KWA MAANA HII WATANZANIA HAWANA HAJA YA KUHANGAIKAKUKAUSHA MATE KUTAKA MAITI YA BALALI LEO. WATANZANIA TUNATAKIWA KUSONGA MBELE, KWA KUTAFUTA HAWA WAHUNZI WA MPANGO HUU MZIMA? NA HII WALA HAIHITAJI SHAHADA.

PILI,
BALALI ALIKUA SIO MUANDIKA HATI ZA MAOMBI YA MALIPO YA FEDHA HIZI (ZA EPA) KUNA WATU WALIANDIKA TENA KWA MADODOSO YALIYOSHEENI UJIVUNI WA TAALUMA ZAO.WATU HAO NDO ADUI WA TANZANIA KULIKO HATA MAITI HII TUNAYOIGOMBEA.

TATU,
SIAMINI NA WALA SITAKI KUKUBALI KWAMBA FEDHA (ZETU) HIZI ZOTE ZIPO KWA BALALI. KUNA WATU WANAZO TENA NYINGI. KAMA INGEKUA NI KAMPUNI KUTOLEA MFANO BASI DALALI AAH KUMRADHI BALALI YEYE ALIPATA GAWIO LA GHARAMAZA KIUTAWALA TU (MANAGEMENT COST).NA MARA NYINGI GAWIO HILI HALIZIDI ASILIMIA KUMI.

MWISHO,
WASIWASI WANGU NI KWAMBA INAONYESHA KUNA MBINU ZINAFANYIKA ZA KIUFUNDI ZA KUTAKA KUWAPOTEZA WATANZANIA NJIA YA MAPAMBANO KWA KUTAKA KUWAAMINISHA WATANZANIA KUW ABALALI NDIO ALIKUA KILA KITU. LAKINI WATANZANIA WAJIULIZE KWANI HUYU BALALI ALIKUA WAPI NA NANI NA ALIKUA NAMAADILI GANI KABLA HAJAKUTANA NA GENGE HILI LA MAFUNDI WAZIMA WA MPANGO HUU WLAIOUPA JINA LA EPA? JE BALALAI SI KWAMBA AMEJIKUTA AMEWEKWA KATI KIASI KWMABA KUTOKANA NA IMANI YAKE KUWA HABA AKAWEZA KUVUTIKA?

NITOE MFANO JINSI NINAVOOONA SUALA LA BALALI KUINGIA KATIKA JANGA HILI. NI SAWA NA BABA KATIKA FAMILIA ALIYEJIKUTA AMEINGIA KATIKA MTEGO WA HOUSEGIRL ANAYEMFANYIA VISA ATEMBEE NAE, NA BABA YULE PAMOJA NA KUJITAHIDI KUIZUIA TABIA ILE CHAFU ANAJIKUTA UZALENDO UMEMSHINDA NA BAADAE KUINGIA KWENYE MTEGO.

NAWASILISHA

Anonymous said...

Kifo cha Balali sio kweli.

Anonymous said...

may god rest your soul in peace.by the way your the scapegot of bot scandal,tunajua ni wengi wamehusika,ila kosa lako marehemu nawe hukutaka,kujiondoa even through media,umeaondoka na ulale salama uliko.pamoja na siri nyingi umezijua.bila kutufichulia ukweli ,lakini spirit yako itawasumbua wengi wahusika wa kashafa hiyo,akiwemo rais,mawaziri wake,wadosi wafanya biashara,waarabu,poleni ndugu wa marehemu,yaliompata peku hata ungo yatamfika, asanteni mafisadi kwa kuumua balali,ili asifichue ukweli wenu,nanyi mungu atawadhibu hapa hapa duniani,na mali hizo za walala hoi zitawatokeeni puani.mwenye uchungu
mwanachi, long live julius nyerere,umetuachia majanga kwa kutuachia mafisadi.

Anonymous said...

Nani ana uhakika kuwa alilishwa sumu jamani? Hizi speculations zisizo kichwa wala miguu na lifestyles hizi walizonazo wakubwa wakifa basi wamelishwa sumu au wamefanyiwa sijui nini, lakini angkuwa mtu mdogo asiye na cheo ukweli ungesemwa wazi. I doubt hiyo story ya sumu ni cover up ya maradhi mengine kabisa. Sometimes ni better kunyamaza kuliko kusingizia vitu vinavyoweza kufanya watu wakaanza kuspeculate lifestyle yako kwa undani.

Poleni wana familia kwa msiba.