Friday, January 02, 2009

Salamu za Mwaka Mpya kutoka kwa Rais Kikwete

Kutoka Lukwangule Blog:

Rais kula sahani moja na mafisadi 2009!

RAIS Jakaya Kikwete ameagiza mtumishi yeyote wa Serikali ambaye atahusika na wizi au ubadhirifu wa fedha za umma kufikishwa katika vyombo vya sheria .

Katika salamu zake za mwaka mpya kwa taifa, Rais alisema bado hali si ya kuridhisha katika matumizi ya fedha za umma kumfanya afurahi na akaahidi kuwa mwaka huu utakuwa wa kubanana katika jambo hilo ili ufanisi uweze kufikiwa.

“Kuanzia mwaka ujao nitawaomba wakaguzi wa mahesabu ya Serikali kumkabidhi kwenye vyombo vya sheria mtumishi wa Serikali aliyehusika na wizi au ubadhirifu mara watakapougundua,” alisema Rais.

Aliongeza kuwa kwa sasa utaratibu hauko hivyo lakini akataka ofisi ya CAG itazame upya utaratibu wa sasa ili isaidie kujenga nidhamu hata kama ni ya woga wa kufungwa. “Itasaidia kunusuru fedha nyingi za umma zinazotumiwa isivyo.”

Ifuatayo ni hotuba yake kamili:

Salamu za Mwaka Mpya za Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa Wananchi, 31 Disemba 2008
Ndugu Wananchi;
Hatimaye imewadia ile siku ya kuuaga mwaka mmoja na kuukaribisha mwingine. Leo tunauaga mwaka 2008 na kuukaribisha mwaka 2009.
Kwanza kabisa, naomba sote tumshukuru Mwenyezi Mungu aliyetujaalia uhai na kutuwezesha kuiona siku hii adhimu salama. Ni wajibu wetu kumshukuru Muumba wetu kwani wapo wenzetu wengi hawakujaaliwa kuiona siku ya leo kwa vile wametangulia mbele ya haki. Wakati tukikumbushana wajibu wetu wa kumuomba Mwenyezi Mungu awape marehemu wetu hao mapumziko mema, tumuombe pia awape nafuu na kuwaponya wenzetu wote wanaougua maradhi mbalimbali ili wajumuike nasi katika shughuli za ujenzi wa taifa letu.
Ndugu Wananchi;
Mwaka wa 2008 tunaoumaliza leo ulikuwa mwaka wa aina yake kwa taifa letu na katika historia ya uongozi wangu. Ulikuwa ni mwaka ambao tumepata mafanikio mengi mazuri na mengine ya kihistoria katika nyanja mbalimbali za maisha ya wananchi wa Tanzania na taifa letu. Lakini, pia kulikuwepo na changamoto au matukio machache ambayo yalisababisha baadhi ya watu ndani na nje ya nchi yetu wapate shaka juu ya hatima ya umoja, amani na utulivu wa nchi yetu. Umoja, amani na utulivu ndiyo nguzo kuu na sifa kubwa inayoitofautisha na kutambulisha Tanzania miongoni mwa mataifa barani Afrika.
Ndugu Wananchi;
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwamba tumeumaliza mwaka huu kwa usalama, amani na utulivu. Tuzidi kumuomba baraka na rehema zake, katika mwaka 2009, ili nchi yetu iendelee kuwa na amani, utulivu na watu wake waishi kwa upendo, umoja, masikilizano, mshikamano na ushirikiano kama ndugu wa taifa moja.
Pamoja na kumuomba Mwenyezi Mungu, hatuna budi kutambua kuwa dhamana ya kuhakikisha kuwa nchi yetu inaendelea kuwa tulivu na yenye amani na upendo miongoni mwa watu wake ni yetu wenyewe. Ni ukweli ulio wazi kuwa katika mwaka huu tunaoumaliza sasa baadhi yetu tumekuwa tunafanya vitendo au kutoa kauli ambazo zilikuwa zinalielekeza taifa kubaya. Tena tulikuwa tunafanya hivyo kwa ajili ya kuendeleza manufaa binafsi ya kisiasa. Ni matumaini yangu kuwa tutajiepusha na mambo hayo katika mwaka 2009. Nawasihi viongozi wenzangu wa kisiasa na wa kijamii tubadilike, tuweke mbele maslahi ya taifa ili tuiepushe nchi yetu na mabalaa ambayo baadhi ya wenzetu yaliwakuta.
Hali ya Uchumi wa Nchi na Dunia
Ndugu Wananchi;
Kwa jumla hali ya uchumi wa nchi yetu kwa mwaka 2008 ilikuwa ya kiwango cha kuridhisha. Lakini, hali ingekuwa bora zaidi kama uchumi wa dunia usingepata misukosuko iliyoupitia sasa. Kwa sababu ya matatizo makubwa yanayoukabili uchumi wa dunia, baadhi ya malengo tuliyojiwekea kuhusu ukuaji na mwenendo wa uchumi wetu yameathiriwa.
Mfumuko wa Bei
Ndugu Wananchi;
Bei kubwa za mafuta zilizokuwepo kwa karibu miaka miwili mfululizo na hasa katika miezi kumi ya mwanzo ya mwaka huu zilipokuwa juu sana, imekuwa kichocheo kikubwa cha kupanda sana kwa mfumuko wa bei na ukali wa maisha hapa nchini. Aidha, kupanda sana kwa bei za vyakula tunavyoagiza kutoka nje kama vile ngano, mchele na vinginevyo viliifanya hali ya mfumuko wa bei kuwa mbaya zaidi.
Tulikuwa tumejiwekea lengo, kwa mfano, katika bajeti iliyopita kuwa tutateremsha mfumuko wa bei hadi kuwa asilimia 4.5 mwezi Juni, 2008 kutoka asilimia 5.9 ya mwezi Juni, 2007. Badala yake mfumuko wa bei ukawa asilimia 9.3 mwezi Juni, 2008 na kupanda hadi asilimia 12.3 ilipofika mwezi Novemba, 2008. Hivi sasa bei za mafuta zimeshuka kuanzia Oktoba, 2008 na hivi leo zimefikia dola za Kimarekani 38.4. Hali kadhalika, bei za baadhi ya vyakula nazo zimeshuka. Lakini, itachukua muda mpaka manufaa ya hali hiyo kuonekana kwa uchumi wa nchi yetu na wananchi wake.
Ndugu Wananchi;
Wakati mwingine hali huwa hivyo kwa sababu ya ukaidi na tamaa ya wafanyabiashara. Nimekwishawaagiza Mawaziri wahusika kuzibana mamlaka husika kutimiza ipasavyo wajibu wao kwa mujibu wa mamlaka waliyopewa kisheria kuwalinda wananchi dhidi ya wafanyabiashara wa aina hiyo. Wakati huo huo narudia kuwataka wafanyabiashara watoe ushirikiano unaostahili kwa maslahi ya wateja wao na taifa kwa jumla. Aidha, nazitaka mamlaka husika kutokuchelewa wala kuchelea kuchukua hatua zipasazo kwa wafanyabiashara wakaidi.
Ndugu Wananchi;
Kutetereka kwa mfumo wa fedha wa kimataifa na kuanguka kwa masoko ya hisa katika mataifa yaliyoendelea kumesababisha uchumi wa nchi hizo kudhoofika. Hali hiyo imekuwa na athari za namna na viwango mbalimbali kwa uchumi wa nchi zinazoendelea kama Tanzania.
Nilikwishalieleza siku za nyuma na napenda kurudia kusema kuwa sekta ya fedha hapa nchini bado ni tulivu. Haijaathiriwa na misukusuko inayoikumba sekta ya fedha ya kimataifa. Zipo sababu kuu mbili.
Kwanza, kwamba, sekta yetu ya fedha na soko la mitaji havijaunganishwa na mfumo wa fedha wa kimataifa na masoko ya hisa ya kimataifa. Hivyo basi, hakuna athari za moja kwa moja zinazotukuta hapa nchini kwa sasa.
Pili, kuna usimamizi mzuri wa soko na sekta ya fedha unaofanywa na Benki Kuu. Mpaka sasa, juhudi hizo za Benki Kuu zimesaidia. Hata hivyo, tunatambua haja na hoja ya kuendelea kuwa makini. Inaelekea matatizo ya mfumo wa fedha na uchumi katika nchi zilizoendelea yatachukua muda mrefu kutengemaa. Hatujui siku za usoni mambo ya yatakuwaje.
Serikali itaendelea kushirikiana na Benki Kuu kuzuia athari za soko la fedha duniani zisitufikie au kama zitatufikia, basi makali yake yawe nafuu. Kwa sasa mfumo wa ufuatiliaji (surveilance) na ule wa kutoa tahadhari ya mapema (early warning system) vinafanya kazi ipasavyo. Tuko tayari kuchukua hatua zaidi kama hapana budi.
Ndugu Wananchi;
Athari za hiyo Tsunami ya uchumi wa dunia, kama ilivyoitwa na baadhi ya watu, kwa uchumi wetu tumeanza kuziona kwa baadhi ya sekta. Tuchukue kwa mfano, sekta ya utalii. Katika mapumziko yangu ya mwisho wa mwaka huu nilitembelea mbuga zetu za hifadhi ya wanyama za Tarangire, Ziwa Manyara, Ngorongoro na Serengeti ya Kusini. Katika mazungumzo yangu na viongozi wa hoteli, hifadhi hizo na wale wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) nimeelezwa jinsi idadi ya watalii ilivyopungua na mapato yao kushuka kwa kati ya asilimia 7 na 18.
Aidha, nimezungumza na baadhi ya wamiliki wa viwanda vya kuchambua pamba na viongozi wa Bodi ya Pamba. Wote wamenieleza tabu wanayoipata ya kuuza pamba yao nje. Pia wanaelezea jinsi bei ya pamba ilivyoshuka katika soko la dunia. Katika kipindi cha mwezi Machi hadi Julai, 2008 bei ya pamba ilikuwa senti 82 za dola za Kimarekani kwa paundi na kushuka hadi senti 45 kwa paundi kwa sasa.
Hali kwa zao la kahawa nayo siyo nzuri. Nimeambiwa kuwa kati ya mwezi Agosti, msimu wa kahawa ulipoanza, na tarehe 18 Disemba 2008, bei ya kahawa ya Arabica kwenye soko la dunia, imeshuka kutoka dola za Kimarekani 158 hadi 104 kwa gunia la kilo 50. Hii ni sawa na anguko la asilimia 34. Katika kipindi hicho hicho, bei ya kahawa ya robusta imeshuka kutoka wastani wa dola za Kimarekani 93.6 hadi dola 65.46 kwa gunia la kilo 50. Hii ni sawa na anguko la asilimia 30.
Ndugu Wananchi;
Hata kwa mazao mengine nayo kwa jumla, hali ni hiyo hiyo ya kupungua kwa mauzo nje na kushuka kwa bei. Matatizo tunayoyapata sisi kwa mazao yetu ndiyo yaliyoikuta bidhaa ya mafuta. Kwa sababu ya uchumi kutetereka katika nchi za Marekani, Ulaya Magharibi, Japan, China na India mahitaji ya mafuta yamepungua na bei ya mafuta imeanguka kupita kiasi.

Ndugu Wananchi;
Kupungua kwa mauzo nje na bei ya bidhaa zetu pamoja na kupungua kwa watalii kuna athari kwa uchumi wa nchi yetu. Mapato yetu ya fedha za kigeni yatapungua jambo ambalo litapunguza akiba yetu ya fedha za kigeni, hivyo kuathiri uwezo wetu wa kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje. Aidha, mapato ya Serikali kwa kodi zitokanazo na mauzo hayo yatapungua, hivyo kuathiri uwezo wa Serikali wa kutimiza majukumu yake ya kiutawala na kiuchumi. Isitoshe ajira chache zilizopo katika sekta husika zitapungua na kusababisha watu hao kuwa na hali mbaya kiuchumi.

Ndugu Wananchi;
Hali mbaya ya uchumi wa dunia inasababisha uwekezaji wa kutoka nje nao kuathirika. Baadhi ya wawekezaji walioonyesha nia ya kuwekeza nchini wameahirisha nia yao. Ukiacha hofu inayotokana na hali mbaya ya uchumi wa dunia, wengine wamekuwa wanapata ugumu wa kupata mikopo kutoka katika mabenki. Mabenki yamekuwa yanasita kukopesha na pale yanapokopesha masharti yake huwa magumu kiasi cha kuwakatisha tamaa wakopaji.

Ndugu Wananchi;
Nimezitaja baadhi tu ya athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa uchumi wa nchi yetu ili tutambue kuwa tupo kwenye mazingira magumu na hali ya baadae ni ya mashaka. Tunaweza kunusurika kwenye eneo moja lakini tukaathirika kwenye maeneo mengine kwa sababu uchumi wetu ni uchumi wa dunia ya utandawazi. Kutokana na athari hizo inakadiriwa kuwa hatutafikia malengo yetu ya kukua kwa uchumi mwaka huu 2008 na hata mwaka ujao wa 2009. Inakadiriwa kuwa uchumi utakua kwa asilimia 7.7 badala ya 7.8 mwaka huu na mwakani utakua kwa asilimia 7.3 badala ya asilimia 8 iliyokadiriwa.
Ndugu zangu;
Watanzania wenzangu;
Napenda sote tutambue kuwa kuna kila dalili kuwa mwaka 2009 huenda tutatumia muda mwingi na nguvu nyingi kukabili athari za machafuko ya uchumi wa dunia. Kwa ajili hiyo, hatuna budi kutambua hivyo mapema na kuwa tayari kusimama kidete kukabiliana na athari zake. Sisi katika Serikali tunafuatilia kwa karibu hali inavyoendelea duniani na hapa nchini na kuamua hatua za kuchukua. Tutaendelea kupashana habari. Maombi yangu kwenu wananchi wenzangu ni uelewa wenu na ushirikiano wenu. Umoja, mshikamano na ushirikiano wetu wakati huu ndivyo vitakavyotukinga na kutuvusha katika tatizo hili kubwa.
Ndugu Wananchi;
Yapo mambo kadhaa ambayo hatuna budi kufanya katika kukabiliana na hali hii tete hapa nchini. Miongoni mwa hayo lipo suala la kujenga uwezo wa ndani wa kujitegemea kwa mambo fulani fulani kama vile chakula na bidhaa muhimu kwa matumizi ya watu. Pili, linalolingana na hilo, ni suala la kukuza utalii wa ndani na kutafuta vyanzo vipya vya watalii kama vile Mashariki ya Kati na Asia. Tatu, kukuza masoko ya ndani kwa bidhaa zetu na masoko ya kanda kama vile SADC na EAC. Wakati mwigine tunahangaikia masoko ya mbali wakati soko lipo h apa ndani au nchi jirani.
Ndugu Wananchi;
Kwangu mimi kauli mbiu muafaka kwa mwaka 2009 ni “Mwaka wa Kuhami na Kukuza Uchumi wa Taifa”. Bahati nzuri kauli mbiu hii inawiana na mpango wangu wa kazi nilipoingia madarakani. Nilikuwa nimepanga kuwa, katika nusu ya kwanza ya kipindi changu cha uongozi tuelekeze nguvu zetu katika upatikanaji wa huduma za kiuchumi na kijamii, na nusu ya pili tushughulikie kukuza uchumi. Nafurahi kwamba, tumefanikiwa kuweka misingi madhubuti ya kisera na mipango ya uhakika ya utekelezaji kuhusu elimu, afya, barabara, maji na umeme vijijini. Utekelezaji wake unaendelea na changamoto yetu kubwa ni upatikanaji wa fedha za kutosha kutekeleza malengo tuliyojiwekea.
Nashukuru kwamba ufanisi mkubwa tulioupata katika ukusanyaji wa mapato ya ndani na misaada ya washirika wetu wa maendeleo tumeweza kupata mafanikio tuliyoyapata mpaka sasa. Hata hivyo mahitaji ya rasilimali bado ni makubwa. Ni wajibu wetu kuendelea kutafuta.
Ndugu Wananchi;
Kuanzia mwaka 2009 Serikali itaelekeza nguvu katika kukuza uchumi wa nchi kwa lengo la kuongeza mapato ya nchi na wananchi wake. Bahati mbaya au nzuri yanayotokea sasa duniani yanasisitiza haja na hoja ya kufanya hivyo. Pia, yameongeza jambo jipya la kufanya, nalo ni la kuhami uchumi usitetereke.
Kilimo Kipaumbele cha Kwanza
Ndugu Wananchi;
Katika agenda yetu ya kukuza uchumi, kilimo kimepewa kipaumbele cha kwanza. Tunafanya hivyo kwa sababu nzuri na za msingi kabisa. Kwanza, tunataka kuhakikisha kuwa tunajitosheleza kwa chakula na tunakuwa na ziada ya kutosha. Katika mazingira ya sasa ambapo bei za vyakula duniani ziko juu, kuwa na upungufu wa chakula na kulazimika kuagiza kutoka nje kutazua matatizo makubwa nchini. Mfumuko wa bei utatushinda kuudhibiti.
Pili, kilimo kitatupatia malighafi ya viwanda vya kusindika mazao ya kilimo na kuzalisha bidhaa kamili zinazotokana na mazao ya kilimo. Kuendeleza viwanda vya aina hii ni kipaumbele chetu cha pili katika agenda yetu ya kukuza uchumi wa taifa. Lazima tuanze safari ya kuuza nje mazao ya kilimo yakiwa yameongezewa thamani kuliko kuyauza yakiwa ghafi kama tufanyavyo sasa. Tutafanya kila liwezekanalo kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ili kufanikisha azma yetu hiyo.
Tatu, kilimo ni chanzo kikubwa cha mapato ya fedha za kigeni kwa nchi, mapato ya serikali kupitia kodi na ni tegemeo la watu wengi nchini kwa uhai wao. Asilimia 8.5 ya fedha za kigeni hutokana na mazao ya kilimo na asilimia 80 ya Watanzania wanaishi vijijini ambapo kilimo ndiyo shughuli yao kuu ya kuwapatia mapato na maisha yao.
Hali ya Chakula
Ndugu Wananchi;
Hali ya upatikanaji wa chakula nchini ni nzuri kwa miaka miwili mfululizo sasa, yaani 2007 na 2008, na tumekuwa tunapata ziada ingawaje ni kidogo. Napenda kuwahakikishia kuwa hakuna tishio la njaa nchini. Hata yale maeneo ambayo yamekuwa yanapata upungufu wa chakula tumeweza kuyahudumia kwa kutumia ziada hiyo na akiba kutoka katika Hifadhi ya Taifa ya Chakula (SGR). Kwa mfano, tathmini iliyofanywa mwezi Septemba, 2008 inaonyesha kuwa watu 240,544 katika Wilaya 20 nchini watakabiliwa na upungufu wa chakula kati ya Desemba, 2008 na Januari, 2009. Watu hao watahitaji tani 7,182 za chakula ambacho tayari kimekwishatengwa kutoka Hifadhi ya Taifa ya Chakula. Hifadhi hiyo sasa ina akiba ya tani 127,420.
Ndugu Wananchi;
Mvua za vuli hazikuwa nzuri kwa mikoa ya Pwani, Dar es Salaam, Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara. Lakini, zimekuwa nzuri kwa mikoa ya Kagera, Mwanza na Mara. Hivyo basi mavuno ya vuli hayatakuwa mazuri katika mikoa iliyoathirika. Hali hiyo inaweza kuongeza iadi ya watu watakaohitaji msaada wa chakula. Hata hivyo, hakuna shaka yoyote tutaweza kuwahudumia. Matumaini yetu na sala zetu kwa mikoa hiyo ni kuwa mvua za masika zitakuwa nzuri. Ikiwa hivyo mzigo utapungua. Bahati nzuri mikoa mingine inayopata mvua moja hali ya mvua ni nzuri, hivyo inatutoa hofu ya upungufu mkubwa wa chakula nchini. Tuzidi kumuomba Mungu mvua zinyeshe kama kawaida katika mikoa hiyo nayo.
Ndugu Wananchi;
Dhamira yetu katika kuelekeza nguvu zetu katika kuendeleza kilimo ni kuongeza tija. Bahati mbaya kwa sasa tija iko chini sana jambo linaloelezea hofu za upungufu wa chakula, mazao ya biashara na hali duni ya maisha kwa wakulima wengi. Kwa ajili hiyo Serikali imekusudia mwaka 2009 kutilia mkazo mambo matano:
a. Upatikanaji na matumizi ya mbegu bora;
b. Upatikanaji na matumizi ya mbolea;
c. Upatikanaji wa maafisa ugani;
d. Uendelezaji wa kilimo cha umwagiliaji pale inapowezekana; na
e. Upatikanaji na uimarishaji wa masoko ya mazao ya wakulima.
Ndugu Wananchi;
Mambo yote hayo na mengine ambayo sikuyataja si mapya. Tumekuwa tunayatekeleza katika miradi na programu mbalimbali za kuendeleza kilimo nchini kama vile DADP’s, PADEP na ASDP. Tunachokusudia kufanya mwaka ujao ni kutoa msukumo maalum wa kuendeleza kilimo kama tulivyofanya kwenye elimu na tunavyokusudia kufanya kwa upande wa afya.
Kuhusu upatikanaji wa mbegu, tumepanga kuimarisha vituo vyetu vya utafiti wa mbegu na kuongeza uwezo wetu wa kuzalisha mbegu hapa nchini. Kwa ajili hiyo nimewaagiza Jeshi la Kujenga Taifa na Jeshi la Magereza watumie sehemu ya mashamba yao kuzalisha mbegu. Nafuraji kwamba viongozi wa idara zetu hizo tayari wameshaelewana na wenzao wa Wakala wa Mbegu nchini kufanikisha mpango huo muhimu. Kwa upande wa mbolea nafurahi kusema kuwa kauli yangu niliyotoa Bungeni tarehe 21 Agosti, 2008 kuhusu pesa za EPA imeshaanza kutekelezwa. Shilingi bilioni 30 zimetengwa kwa ajili ya mbolea ya ruzuku na bilioni 10 kwa ajili ya madawa ya mimea. Madawa ya mifugo yametengewa shilingi bilioni 10 na mikopo ya kilimo TIB shilingi bilioni 10.
Ndugu Wananchi;
Nafurahi pia kuwa dhamira yetu ya kuzalisha mbolea hapa nchini inatekelezwa vizuri. Kiwanda cha kuzalisha mbolea ya phosphate pale Minjingu, mkoani Manyara kimekamilika na kimeshaanza kazi. Wakati huo huo mchakato wa ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha mbolea ya NPK hapo Minjingu umeshaanza. Aidha, uamuzi wetu wa kujenga kiwanda cha mbolea ya urea na ammonia kule Mtwara umefikia hatua nzuri. Kampuni ya kuwekeza imekwishapatikana na shughuli za mchakato wa ujenzi wa kiwanda hicho ziko mbioni.
Hatua hizi zote zitakapokamilika, ndani ya miaka miwili ijayo, zitaiwezesha nchi yetu kuwa moja ya wazalishaji wakubwa wa mbolea katika kanda yetu ya SADC na Jumuiya ya Afrika Mashariki. Tutatosheleza mahitaji yetu na kuwa na ziada ya kuuza kwa wengine nchi za nje na kujipatia fedha za kigeni.
Mifugo
Ndugu Wananchi;
Juhudi za kuongeza tija katika kilimo zitaelekezwa pia kwenye mifugo. Nia yetu ni kuboresha ufugaji wetu ili tupate mifugo inayotoa nyama nyingi, maziwa mengi na ngozi zilizo bora. Juhudi hizo zitajumuisha kuboresha aina ya mifugo yetu kwa kutumia madume bora na uhamilishaji. Pia itahusisha upatikanaji wa huduma za kinga na tiba ya mifugo, majosho, malisho, maji, masoko ya mifugo na mazao ya mifugo. Suala la kuwa na viwanda vya kusindika mazao ya mifugo nalo tutalipa uzito unaostahili.
Uwekezaji
Ndugu Wananchi,
Katika mwaka 2009, tutaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kuvutia wawekezaji wengi zaidi wa ndani na nje kuja kuwekeza nchini. Sifurahishwi na taarifa nizipatazo kuwa mazingira ya uwekezaji na kufanya biashara nchini bado hayajaboreka vya kutosha. Na, linalonisumbua zaidi ni kule kuanza kujengeka dhana kuwa Tanzania inaanza kupoteza sifa ya mahali rafiki kwa wawekezaji. Hii si dalili nzuri, lazima tuibadili haraka iwezekanavyo.
Ndugu Zangu;
Dunia nzima hata mataifa tajiri yanavutia wawekezaji seuze siye maskini? Uwekezaji ndiyo chachu ya kukua kwa uchumi. Bila ya uwekezaji uchumi haukui. Wote tunaowasifia kufanikiwa kiuchumi ni kutokana na uwekezaji. Hata China imeendelezwa na uwekezaji tena kutoka mataifa ya kibepari.
Tutayaainisha mambo yanayotufikisha hapo na kuyatafutia majawabu. Natambua kuwepo malalamiko kuhusu usumbufu na urasimu mkubwa katika kuwahudumia wawekezaji. Mlolongo na muda wa uamuzi ni mrefu, kuna usumbufu upande wa kodi na tuhuma za vitendo vya rushwa zinasikika. Wakati mwingine kauli za wanasiasa wetu zimekuwa zinawaogopesha wawekezaji. Yote haya na mengineyo ni mambo ambayo yapo kwenye uwezo wetu kuyarekebisha.
Tumedhamiria kuyakabili kwa dhati matatizo hayo ili tuifanye Tanzania kuwa nchi nzuri kuwekeza. Pamoja na kusimamia kwa karibu mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara Tanzania (BEST), nakusudia kuanzisha kitengo maalum cha kusikiliza malalamiko ya wawekezaji na kuyatafutia ufumbuzi (Investors Complaints Bureau). Kitengo hicho kitakuwa chini ya Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi na kazi yake itakuwa ni kutatua kwa haraka malalamiko ya wawekezaji.
Mikopo ya Wajasiriamali Wadogo na SACCOS
Ndugu Wananchi,
Miaka miwili iliyopita tulianzisha mpango wa mikopo kwa wajasiriamali wadogo wadogo ambao hawana sifa za kukopesheka katika mabenki kwa utaratibu wa kawaida. Tumefanya hivyo ili wanyonge nao wapate fursa ya kujiendeleza na kujikwamua. Kama tujuavyo, tulitenga shilingi bilioni moja kwa kila mkoa wa Tanzania Bara na shilingi milioni 100 kwa kila mkoa kwa mikoa minne ya Zanzibar na milioni 200 kwa mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja. Tulikubaliana kuwa mikopo hiyo itatolewa na Benki za CRDB na NMB na asasi ndogo za fedha kama vile Benki ya Posta, PRIDE, SELF n.k.
Taarifa zinaonyesha kuwa hadi Novemba 30, 2008 jumla ya shilingi bilioni 39 zimekopeshwa na NMB (16.1bn/=) na CRDB (22.9bn/=) na watu 48,339 wamenufaika pamoja na SACCOS 192 na vikundi 137. Benki na asasi nyingine 12 zimeshakopesha SACCOS 236 na shilingi 4.6 bilioni zimetumika katika wilaya 46 za Tanzania Bara.
Katika ziara zangu katika mikoa ya Bara nimepokea malalamiko ya watu kuhusu upatikanaji wa mikopo hiyo. Moja ya jambo nililojifunza ni kuwa, mahitaji ya mikopo ni makubwa na fedha zilizotolewa ni kidogo. Jawabu lake ni kuongeza fedha, jambo ambalo tuko tayari kufanya. Jambo la pili nililojifunza ni kuwa fedha zilizolipwa na wakopaji wa awali hazijazungushwa. Jawabu lake ni kuzizungusha ili wengine nao wakope. Tunazungumza na mabenki juu ya jambo hilo. Ni dhamira yangu mwaka ujao wa 2009 tufanye tathmini ya kina ya mpango huu ili tubaini mapungufu yake na mbinu za kuyarekebisha ili tuongeze fedha na kunufaisha watu wengi zaidi wa kipato cha chini wainue hali zao za maisha.
Kwa nia ile ile ya kuwasaidia watu wasiokuwa na sifa za kukopesheka moja kwa moja na mabenki wapate mitaji ya kufanyia shughuli zao za kujipatia kipato, tuliwahimiza wananchi waanzishe Vyama vya Kuweka na Kukopa. Tulipoingia madarakani kulikuwa na SACCOS 1,875 na sasa zipo 4,780 kutokana na msukumo maalum tulioutoa kwa uanzishwaji wake. Fedha nyingi za akiba zimewekwa na wanachama wa SACCOS hizo na mikopo mingi imetolewa kwa wanachama hao. Aidha, SACCOS kadhaa zimeweza kupata mikopo ya kawaida ya mabenki na kupitia mikopo ya wajasiriamali wadogo wadogo.
Pamoja na kujenga utamaduni mzuri wa watu kuweka akiba, SACCOS zimekuwa nyenzo muhimu ya kukuza uchumi na vyombo vya kutumainiwa na wananchi wa kawaida katika harakati zao dhidi ya umaskini. Napenda kuahidi kuwa ni makusudio yetu kuendeleza juhudi za kuimarisha na kuanzisha SACCOS nchini.
Huduma za Kiuchumi na Kijamii
Ndugu Wananchi;
Katika mwaka ujao tutaendeleza jitihada za kuongeza na kuboresha upatikanaji wa huduma muhimu za kiuchumi na kijamii hususan elimu, afya, maji, umeme na barabara. Kazi kubwa imefanyika na watu wengi sasa wanapata huduma hizo, lakini bado hazijatosheleza mahitaji na viwango vya ubora.
Tunatambua wajibu wa Serikali wa kuongeza fedha katika bajeti za sekta hizo ili miradi mingi zaidi itekelezwe na kukidhi mahitaji ya wananchi. Hiyo ndiyo dhamira yetu kufanya katika mwaka 2009 na miaka ijayo. Sekta ya maji na umeme vijijini tutazipa kipaumbele stahiki.
Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa elimu ya sekondari napenda kwa mara nyingine tena kuwashukuru na kuwapongeza sana wananchi kwa moyo wao wa kujitolea na kujituma. Moyo wao huo na ushirikiano wao na Serikali ndiyo siri iliyotufanya tuendelee kupata mafanikio makubwa katika upanuzi wa elimu ya sekondari nchini. Hivi sasa, nchini tunazo sekondari za Serikali 3,039 kutoka 1,202 mwaka 2005 na idadi ya wanafunzi imeongezeka kutoka 524,325 mwaka 2005 hadi 1,222,403 mwaka huu. Haya si mafanikio madogo katika kipindi kifupi hivi.
Naomba moyo huo wa kujitolea na ushirikiano viendelee kwa manufaa ya watoto wetu na wajukuu wetu waliopo sasa na wajao. Sisi katika Serikali tunaahidi kuendelea kutimiza wajibu wetu katika ushirikiano wetu huo. Tutaendelea kukabili changamoto za upatikanaji wa walimu, vitabu, vifaa vya kufundishia, maabara na nyumba za walimu. Tunatambua kuwa ni mzigo mkubwa lakini hatuna budi kuubeba kwa maslahi ya taifa letu.
Matokeo ya Darasa la Saba
Ndugu Wananchi;
Kwa miaka miwili mfululizo matokeo ya mitihani ya darasa la saba yamekuwa si mazuri. Mwaka wa jana kiwango cha kufaulu kilikuwa asilimia 54.2 na mwaka huu ni asilimia 51.2. Hali hii si nzuri na hatuwezi kuacha iendelee. Hatuna budi kujiuliza kulikoni na kutafuta majawabu muafaka. Nimeiagiza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini kasoro zilizopo na kupendekeza hatua za kuchukua. Aidha, nimemuagiza Waziri Mkuu kulisimamia suala hili kwa ukamilifu.

Barabara
Ndugu Wananchi;
Katika mwaka huu tunaoumaliza leo, tuliendelea kutoa kipaumbele cha juu kwa sekta ya miundombinu. Tumeongeza bajeti ya miundombinu na sasa ni ya pili kwa ukubwa baada ya elimu. Kiasi cha shilingi bilioni 973.3 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu nchini katika mwaka wa fedha 2008/09. Tumeendelea kujenga barabara mpya za lami, za changarawe na za udongo. Pia tumekarabati na kuimarisha barabara zilizopo.
Lengo letu la kuunganisha Makao Makuu ya Mikoa yote kwa barabara za lami sasa lina muelekeo mzuri. Mipango kwa kuunganisha mikoa ya Lindi, Mtwara, Rukwa na Ruvuma imefikia mahali pazuri. Hivi sasa nguvu zetu tunazielekeza kwa mikoa ya Kigoma na Tabora ambapo naamini mpaka katikati ya mwaka 2009 sura kamili inaweza kuwa imejitokeza. Nafurahi hata hivyo kwamba, taratibu za ujenzi wa daraja la Mto Malagarasi zimefikia hatua za mwisho.
Tunasikitika kwamba misukosuko ya mfumo wa fedha wa kimataifa umetulazimisha kuahirisha kutekeleza mpango wetu wa kupata fedha kwa kutumia hati fungani (soverign bounds) kwa ajili ya kujenga kwa kiwango cha lami barabara zetu kuu nyingi hapa nchini. Ni matumaini yetu kuwa hali ikitengemaa tutautazama upya mpango huo.
Bandari, Reli na ATCL
Ndugu Wananchi;
Katika mwaka 2009 tutaendelea kufuatilia na kusimamia kwa karibu hali katika mashirika ya reli, bandari na shirika la ndege. Hali ya huduma hizo muhimu hairidhishi hata kidogo. Yapo matatizo ya uendeshaji ambayo yamesababisha huduma zitolewazo kuwa za kiwango kisichoridhisha. Tutafanya kila tuwezavyo kurekebisha mambo ili huduma hizo ziboreke na kuwafanya watumiaji kufurahi.

Mapato ya Serikali
Ndugu Wananchi;
Kama ilivyo ada mwaka ujao tutaendeleza juhudi za kuhakikisha kuwa mapato ya Serikali yanaendelea kuongezeka. Tutaendelea kuimarisha Mamlaka ya Mapato na kuziba mianya inayopoteza mapato ya Serikali.
Napenda kutumia nafasi hii, kuwapongeza sana viongozi na watumishi wa TRA kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kukusanya mapato ya Serikali. Pamoja na matatizo ya hapa na pale hali ya mapato ya Serikali imeimarika. Mara mbili katika mwaka huu wamevunja rekodi ya ukusanyaji wa mapato ya Serikali. Mara ya kwanza ilikuwa mwezi wa Juni walipokusanya shilingi 346.7 bilioni na mara ya pili ilikuwa mwezi wa Septemba walipokusanya shilingi 420.8 bilioni. Tunatambua na kuthamini juhudi zao na nakusudia kuwatunza kwa mafanikio hayo mwishoni mwa mwaka huu wa fedha.
Nidhamu ya Matumizi
Ndugu Wananchi;
Sambamba na juhudi za kuongeza na kuimarisha mapato ya Serikali hatuna budi kuhakikisha kuwa kunakuwepo na nidhamu na uaminifu katika matumizi ya fedha na rasilimali za Serikali. Nimelisisitiza sana jambo hili na kuwataka viongozi wenzangu na watumishi wa Serikali kusoma na kuzingatia maoni na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali yaliyomo katika taarifa zake za kila mwaka. Nimeagiza Viongozi na Watendaji Wakuu wa Wizara, Idara, Mikoa, Wilaya na Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji kusimamia kwa karibu utekelezaji wa Sheria ya Fedha na mali za Serikali na Kanuni zake. Kuna dalili za mabadiliko chanya, lakini hali bado si ya kiwango cha kutufanya tufurahi sana. Mwaka ujao tutaendelea kubanana katika jambo hili ili tufikie ufanisi unaotakiwa.
Ndugu Wananchi;
Kuanzia mwaka ujao nitawaomba wakaguzi wa mahesabu ya Serikali kumkabidhi kwenye vyombo vya sheria mtumishi wa Serikali aliyehusika na wizi au ubadhirifu mara watakapougundua. Najua utaratibu wa sasa hauko hivyo. Nataka tuutazame upya utaratibu wetu wa sasa ili isaidie kujenga nidhamu hata kama ni ya woga wa kufungwa. Itasaidia kunusuru fedha nyingi za umma zinazotumiwa isivyo.
Ni matumaini yangu pia kwamba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ataendeleza kwa kasi na nguvu zaidi kazi waliyoianza ya ukaguzi wa thamani ya fedha zilizotumiwa na kulinganisha na kazi iliyofanyika (value for money audit). Ukaguzi wa asili umekuwa unahusu uandishi wa vitabu kwa mujibu wa kanuni za fedha. Lakini, inawezekana kabisa vitabu vya hesabu vikaandikwa vizuri lakini pesa zikatumika vibaya au hata kuibiwa. Tunataka ulinganifu sawia wa fedha zilizotumika na kazi iliyofanywa.
Ndugu Wananchi;
Nimewaelekeza wenzetu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kufanya kazi kwa karibu na ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kusaidia kupambana na wasiozingatia nidhamu ya matumizi ya fedha na mali za umma hususan wezi na wabadhirifu wa fedha za umma. Bahati nzuri Sheria ya Mwaka 2007 iliyounda PCCB mpya imetoa mamlaka ya kufanya hivyo. Nimewataka wawe wakali kwa wala rushwa kama wafanyavyo sasa, lakini pia wawe wakali kwa wale wote wanaokiuka kanuni za fedha za Serikali. Vitendo hivyo siyo tu vinaitia hasara Serikali bali pia vinapunguza uwezo wa Serikali kuwahudumia wananchi walioiweka madarakani. Nimewataka waitumie vyema sheria mpya na fursa waliyonayo ya kuwaongezea uwezo wa rasilimali tuliyowapa kwa kutumiza ipasavyo wajibu wao. Nimewasihi pia kwamba katika kufanya hivyo wasionee wala kupendelea watu bali watende haki.
Ulinzi na Usalama
Ndugu Wananchi,
Tunaumaliza mwaka wa 2008 hali ya ulinzi na usalama wa nchi ikiwa ya kuridhisha. Mipaka ya nchi yetu ni salama na nchi ni tulivu. Hatuna budi kutoa pongeza maalum kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa kazi nzuri waliyoifanya na wanayoendelea kuifanya. Uhalifu wa makosa makubwa ya jinai kama vile mauaji, unyang’anyi wa kutumia silaha na unyang’anyi wa kutumia nguvu umepungua. Taarifa za Januari hadi Novemba, 2008 zinaonyesha kuwa kulikuwa na matukio ya aina hiyo 8,330 ukilinganisha na matukio 10,381 katika kipindi kama hicho mwaka 2007. Huu ni ushahidi kuwa Polisi wanafanikiwa kudhibiti uhalifu, hata hivyo bado juhudi ziongezwe ili matukio ya uhalifu yapungue zaidi. Nafurahi pia kwamba hata ajali za barabarani zimepungua mwaka huu ukilinganisha na mwaka wa jana. Mwaka wa jana kulitokea ajali 16,196 kati ya Januari na Novemba, wakati mwaka huu zimetokea ajali 5,500. Hata idadi ya watu waliopoteza maisha imepungua kutoka 2,757 mwaka 2007 hadi 1,270 mwaka huu.
Ndugu Wananchi;
Wakati tunawapongeza wadau na Jeshi la Polisi kwa maendeleo hayo bado naamini kuwa ajali za barabarani pamoja na idadi ya watu wanaopoteza maisha au kujeruhiwa na mali kuharibiwa vinaweza kupungua zaidi. Ajali nyingi za barabarani husababishwa na makosa ya madereva kutokuheshimu sheria ya usalama barabarani. Lakini, pia kuna mchango wa Jeshi la Polisi hasa wale wa usalama barabarani kutodhibiti ipasavyo madereva wazembe. Tatizo hili lipo kwenye uwezo wa Polisi na wadau kulidhibiti.
Madereva wakubali kuzingatia na kuheshimu sheria ya usalama barabarani. Wenye magari wahakikishe wanaajiri madereva wenye sifa nzuri. Aidha, madereva wa mabasi ya abiria watambue kuwa wanabeba binadamu wenzao ambao kwa kipindi chote cha safari usalama wao uko mikononi mwao. Makosa madogo ya dereva yanaweza kuwapotezea watu uhai au kuwapa vilema vya maisha. Lazima watambue umuhimu wa wao kuwa waangalifu. Polisi nao lazima watimize ipasavyo wajibu wao. Polisi lazima wawe wakali kuhakikisha sheria za usalama barabarani zinafuatwa. Naamini Polisi wakiwa wakali tofauti itaonekana.

Mauaji ya Albino
Ndugu Wananchi;
Suala la mauaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi, yaani albino nimekwishalisemea mara mbili tatu mwaka huu, na mara ya mwisho wakati wa Baraza la Idd tarehe 8 Desemba, 2008. Ni mauaji na mateso ambayo hayana sababu ya kutokea kwa sababu chanzo chake ni cha kipuuzi. Imani kwamba kiungo cha albino kinampa mtu utajiri ni jambo la kijinga. Nirudie kuwasihi wenzetu hawa wanaotafuta utajiri wa haraka haraka kuwa juhudi na maarifa yao ndiyo siri ya kufanikiwa kwao na si vinginevyo. Lakini, kwa vile wapo watu wanaoamini kuwa wakipata viungo vya albino watatajirika na wapo waganga na wauwaji, Serikali haina budi kuchukua hatua za kuwabana watu wote hao na kulitokomeza kabisa tatizo hili.
Tumeunda kikosi-kazi kinachojumuisha Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa cha kuendesha mapambano haya. Hivi sasa wanaendelea na uchunguzi wa kina nchi nzima kuwatambua wahalifu na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria. Mpaka sasa watu 91 wamekamatwa na kufikishwa mahakamani na mapambano yanaendelea.
Kwa nia ya kuongeza kasi na nguvu ya mapambano haya, mapema mwaka ujao tutaendesha zoezi la kura ya maoni nchi nzima. Tutawataka wananchi wawataje watu wanaowajua kuwa wanajihusisha na mauaji au kukata viungo vya albino. Wawataje waganga wanaohusika, wauawaji wa albino, wauzaji wa viungo vya albino na wafanyabiashara wanaotumia viungo hivyo. Taarifa hizo zitasaidia kuwafuatilia na kuwakamata watu hawa waovu. Utaratibu kama huu ulitusaidia katika mapambano dhidi ya ujambazi nchini. Naamini utasaidia kwa hili. Tunafanya matayarisho ya zoezi hilo. Wakati utakapowadia watu wataarifiwa namna ya kushiriki. Naomba ushirikiano wa hali ya juu wa wananchi wakati huo. Jitokezeni kuwataja ili isaidie kukomesha aibu hii kwa taifa letu.
Hitimisho
Ndugu Wananchi,
Tunaumaliza mwaka nchi ikiwa na sifa kubwa katika medani ya kimataifa. Uhusiano wetu na mataifa yote duniani ni mzuri. Hatuna adui. Hali kadhalika uhusiano wetu na mashirika ya kimataifa ya kisiasa na kiuchumi ni mzuri. Nchi yetu inaheshimika na kutumainiwa katika diplomasia ya kimataifa. Tumepokea wageni wengi mashuhuri na wengine ni wa kihistoria kama ziara ya siku nne ya Rais wa Marekani, Mheshimiwa George W. Bush. Tumekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kwa mwaka huu. Pamoja na ugumu wake lakini tumeifanya kazi hiyo vizuri na yapo mambo kadhaa mazuri ambayo nchi yetu itakumbukwa nayo. Miongoni mwa hayo ni amani ya Kenya, kurejesha umoja wa taifa la Comoro, kuongoza vyema mijadala kuhusu masuala magumu kama yale ya uundaji wa Serikali ya Umoja wa Afrika na kuyafikisha mahali pazuri.
Mwaka 2009 nchi yetu itakabidhi uongozi wa Umoja wa Afrika kwa heshima na upendo mkubwa kutoka kwa wanachama wenzetu na mataifa mengine duniani.
Ndugu Wananchi;
Tunaumaliza mwaka nchi ikiwa tulivu. Hii inathibitisha kuwa nchi inaweza kuwa tulivu isipokuwa pale ambapo baadhi yetu tutakapokuwa tumeamua kuwa isiwe hivyo. Naomba mwaka 2009 uwe tofauti. Tuache vitendo vya kuchochea ghasia kwa kisingizio chochote kile. Vitendo hivyo havitavumiliwa hata kidogo. Ni vizuri tukaambiana mapema tusije tukalaumiana. Naomba Watanzania wenzangu wote na hasa wanasiasa wenzangu tuyatambue hayo na tujiepushe nayo. Naomba makundi ya kijamii yatambue ukweli huo na waache kuwaendekeza wanasiasa hasidi.
Ndugu Wananchi;
Naomba nimalize kwa kuwakushukuru kwa mara nyingine tena Watanzania wenzangu wote kwa ushirikiano wenu na uelewa wenu na msaada wenu kwangu na kwa wenzangu wote serikalini katika kipindi chote cha mwaka huu tunaouaga leo. Tumepita vipindi vya raha na vigumu kwa pamoja na tunaumaliza mwaka tukiwa wamoja na watu wenye mshikamano. Naomba tuingie mwaka mpya na moyo huo na tuendelee hivyo.
Nitakuwa mtovu wa fadhila kama sitamshukuru Mwenyezi Mungu kwa wema na upendo wake na kutuvusha salama mwaka 2008. Tuzidi kumuomba atuongoze na kutuvusha salama mwaka ujao na miaka ijayo. Mimi si Sheikh na wala si mwanazuoni, mimi na mfuasi tu. Lipo wazo nimekuwa napewa mara kadhaa kuwa pengine si vibaya kila mwishoni au mwanzoni mwa mwaka tungekuwa na siku ya maombi ya pamoja watu wote wote wa dini tukiongozwa na viongozi wa dini zetu kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa mwaka tulioumaliza na kuliombea taifa mema kwa mwaka unaofuata. Ni wazo linalovutia wengi lakini sidhani kuwa ni ni jambo la kufanywa kwa amri ya Serikali. Nawaachia viongozi wa dini zetu watuongoze.
Naomba tutakiane heri na fanaka tele katika mwaka mpya, 2009.
Mungu Ibariki Afrika
Mungu Ibariki Tanzania
Ahsanteni kwa kunisiliza.

Queen Latifah Aiibiwa Hotelini Tobago


Mwimbaji maarufu na mcheza sinema, Queen Latifah, ameibiwa pete, bangili na vitu vingine vyenye thamani ya dola $10,000 huko Tobago! Yuko huko kwenye likizo. Hoteli aliyofika ni ya ghali chumba huko ni dola $1,000 kwa siku!

Habari zinasema kuwa Queen Latifah alitoka kwenye kula brunch, alivyorudi alikuta ameibiwa.

Wenye hoteli na polisi wa Tobago wanasema wanafanya juu chini ili wamrudishie Queen Latifah mali yake.

**************************************************************************

Latifah's Jewelery Stolen In $10,000 Holiday Heist

2 January 2009

Queen Latifah has become the victim of thieves, who stole more than $10,000 (GBP6,990) in jewellery from her luxury villa in Tobago.

The actress/singer, real name Dana Owens, was holidaying at the $1,000 (GBP700)-per-night Stone Haven Villas in Black Rock, Tobago with a female friend when burglars struck on Monday.

Latifah, who checked in under the name Cynthia Hadden, reportedly returned from a barbecue brunch held in her honour by the establishment's management to discover a bracelet, two gold rings, a gold chain and a silver ring were missing.

Police were called to the resort after staff security conducted a search of the estate.

Police Commissioner James Philbert tells Trinidad and Tobago's Newsday, "Several searches are being carried out and the police are trying to have the jewellery returned to Queen Latifah. Investigators said the larceny seems to be an inside job and efforts are being made round the clock to make a breakthrough."
Kwa habari zaidi someni:

Thursday, January 01, 2009

Heri ya Mwaka Mpya - 2009




Nawatakia wadau wote heri ya mwaka mpya! Ninaomba 2009 iwe mwaka mzuri kwa wote. Pia ninaomba mungu apumzishe kwa amani roho za wasioweza kuona mwaka 2009. AMEN.
Hapa Boston tumeanza mwaka mpya na baridi kali na theluji mwingi. Baridi kama Alaska. Upepo umekuwa -15 degrees!

Tuesday, December 23, 2008

Heri ya Krismasi!



Wadau,

Ninawatakia sikukuu ya Kirismasi Njema! Pamoja na shamrashamra, mapochopocho na zawadi tukumbuke kuwa ni siku ambayo tunasherekea kuzaliwa kwa bwana Yesu Kristo. Na hapa Boston kama mmesikia kwenye taarifa ya hbari tumepigwa na Snow/Theluji kibao! Watu wanaomba summer ije haraka!

Heri ya Krismasi! Merry Christmas!

Monday, December 22, 2008

Mwalimu Nyerere Dodoma 1995

Da Subi ametuletea hii:

J.K.Nyerere, Dodoma - Tanzania 1995

Marehemu Baba wa Taifa la Tanzania, Mwl. Julius Kambarage Nyerere alipozungumza na WanaCCM mwaka 1995 katika ukumbi wa Chama cha Mapinduzi huko Dodoma (nadhani ilikuwa ni Chamwino) kwenye mchakato wa kumtafuta mgombea wa kiti cha uraisi kwa tiketi ya CCM, Mwalimu alisema yafuatayo:http://nukta77.blogspot.com/2008/12/jknyerere-dodoma-tanzania-1995.html

Subi

Ilitokea kweli - No. 1

Hapo zamani za kale, wabongo walichukuliwa kwa wingi na serikali ya USSR (Soviet Union) Urusi, kwenda kusoma huko.

Sasa si mnajua ubaridi wa kule. Yaani baridi hasa. Theluji na barafu kibao. Sasa kuna mBongo fulani, mwanaume alipenda sana kunywa vodka ya Urusi. Yaani baada ya kazi ngumu ya kubukua kazi kunywa vodka.

Siku moja baada ya kunywa alitoka na kawa anatembea barabarani. Theluji ilianguka kwa wingi mpaka jamaa akaona taabu kutembea. Aliamua kusimama na kupumzika kidogo mtaaani huko theluji inazidi kuanguka kwa wingi. Mwisho kalala hapo hapo alipokuwa.

Asubuhi yake, warusi walikuwa wanasafisha mitaa na kuzoa ile theluji iliyoanguka. Wakakuta maiti ya mwafrika mle kwenye snowbank (mlima wa theluji). Wakaita gari la kuja kuchukua maiti. Ile gari likaja na wakatia maiti ya mwafrika mle.

Kufika mortuary, wakailaza maiti mapokezi. Kumbe ile joto ndani ya gari la maiti na ndani ya jengo ilikuwa inafanya mambo. Jamaa ambaye alidhani maiti kakaa wima halafu kaongea Kiswahili! Wacha wazungu wakimbie!

Wataalam wanasema na sikumbuki vizuri lakini ilikuwa kama ile pombe ilipunguza metabolism sijui na ile theluji ilikuwa insulation ndo maana hakufa.

Nafurahi kusema jamaa alimaliza masomo yake Urusi na alirudi Bongo miaka ya 90.

Kipanya Asema

Translation:

Sign on the Desk: Big Shots

Kipanya (rat character): All of them are at the witchdoctors getting their fortunes told!

African Bash huko Italia


Shujaa wa Taifa - Major Alex Nyirenda Afariki Dunia


Kutoka Michuzi Blog:

MAJOR ALEX GWEBE NYIRENDA, SHUJAA ALIYEPANDISHA MWENGE WA UHURU JUU YA KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO SIKU YA MKESHA WA UHURU WA TANZANIA BARA, HATUNAYE TENA.

HABARI ZILIZOINGIA SASA HIVI TOKA KWA FAMILI YAKE ZINASEMA MAJOR NYIRENDA ALIFARIKI JANA SAA MOJA JIONI KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI ALIKOLAZWA. ALIKUWA NA UMRI WA MIAKA 72.

ALIKUWA AKISUMBULIWA NA MARADHI YA KANSA KWA MUDA MREFU NA AMESHAKWENDA MARA KADHAA NCHINI INDIA KWA MATIBABU.

KWA MUJIBU WA HABARI HIZO ZA KIFAMILIA, MAZISHI YATAFANYIKA DAR JUMATANO KATIKAMAKABURI YA KINONDONI. MSIBA UKO NYUMBANI KWA MAREHEMU MBEZI BEACH, FLETI ZA NATIONAL MILLING, KUCHEPUKA NJIA YA KWENDA AFRICANA, DAR.

GLOBU YA JAMII INATOA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA, NDUGU, JAMAA NA RAFIKI WA MAJOR NYIRENDA AMBAYE ATAKUMBUKWA DAIMA KWA HISTORIA ALIYOIWEKA SIKU YA MKESHA WA KUPATA UHURU DESEMBA 9, 1961.

SOMA MAHOJIANO ALIYOFANYA NA BONGO CELEBRITY HIVI KARIBUNI KWA KUBOFYA HAPA:
************************************************************
Wadau,
Mnakumbuka ule wimbo wa halaiki, maneno sikumbuki vizuri hivyo naomba mnisahishe:
Sisi tumeuwasha Mwenge
na kuiweka Mlima Kilimanjaro
Kuwasha Mwenge
Kuwasha Mwenge

Na kuiweka Kilimanjaro

Saturday, December 20, 2008

Nifahamishe.com

WWW.NIFAHAMISHE.COM ni website mpya ambayo inakuja na mambo mbalimbali kwaajili ya watanzaniaBaadhi ya vipengele vilivyopo kwenye nifahamishe.com ni kama ifuatavyo:

* Breaking news za bongo na duniani
* Habari mbali mbali za Tanzaniana za kimataifa
* Habari katika picha na video
* Live radio
* Online Games
* Habari za burudani na wasanii wa bongo*

Utaweza kusikiliza nifahamishe nonstop bolingo na lingala mix->Kuuza kwa kuweka tangazo lako bure au kununua nyumba,magari,vitu vyaelectronics na kadhalika->Kushare picha na watanzania duniani KARIBU NIFAHAMISHE.COM

Thursday, December 18, 2008

Tatizo la Maji DSM - Maoni ya Mdau

Tanzania sijui ni Shida sijui ni Umaskini sijui ni nini?

Baada ya wiki nzima ya mateso ya kukosa maji leo asubuhi maji yametoka hapa jijini Dar es saam na umeme ukakatika kwa hivyo vimepokezana,na kutoka kwenyewe yaani yale sio maji ni mchanganyiko wa udongo yaani kama maji ya Cocoa vile.Nikisoma baadhi ya maoni ya wabeba mabox hapa kwenye kijiji chetu cha jamii,uwa wanasema wao wanakunywa maji moja kwa moja toka bombani na bila kudhurika,nikasema lo! Wenzetu wanafaidi sana,na wanapunguza gharama za kuchemsha maji ya kunywa kwenye mkaa,maana ukidhubutu kunywa maji ambayo hayajachemshwa hapa bongo ni kujitakia kupelekwa hospitali ya rufaa kwa kipundupindu na hata kuweza kupoteza maisha kabisa.

Je vipi kuhusu mbanano wa ndani ya mabasi, imagine umepanda basi la kivukoni mbagala au Kariakoo-Mbagala,mwanangu iyo harufu ya samaki na mchanganyiko wa jasho la siku nzima kama ni mgeni lazima utazimia tu,najiuliza ni kwa nini Serikali yetu kama wao hawawezi wakaruhusu wawekezaji wakaja kuwekeza kwenye usafiri wa jumuia hapa mjini ili kuepukana na hii adha ya usafiri ambayo inaweza ikakuambukiza magojwa ya ngozi,mafua,TB na magonjwa mengine ya kuambukiza kwa hewa na mgusongamano?.

Pia uwa najiuliza wapanga miji wako wapi,wewe Mtanzania unayeishi Masaki,Mikocheni,Osterbay Mbezi beach n.k,je umewahi fika maeneo kama ya mburahati ndani ndani ukaona wenzako wanavyoishi huko,choo bado ni passport size,mifereji ya kupitisha maji taka hakuna,mvua ikinyesha vyoo vinatapishwa,unaambiwa utakuta watoto wanaogelea juu ya vinyesi vya binadamu maana ya hapo nenda sasa Amani hosp utakutana na watoto kibao wanapoteza maisha kwa kipundupindu, Tena maeneo kama hayo ukipita usithubutu kifungua kifurushi kilichofungwa cheusi cheusi hivi,wewe yaani kwa jina lingine vinaitwa vibomu huko uswahilini,basi utakutana na kinyesi nyumba zima wamejiachia humo,hii inatokea pale choo kimejaa na hakuna mvua kwa muda kuwezeka kukifungua choo kiondoke mtaani.

Yaani unaweza kusema kipindupindu ni ugonjwa wa maskini,maana idadi kubwa ya wagonjwa ni hao ni wakipato cha chini mno,

Vipi kuhusu Uchafu barabarani na barabara mbovu sizizo na mpangilio hapa town,yaani ni balaa tupu,mimi niliwahi kukaa pale Upanga toka nizaliwe hadi leo,unaambiwa hata siku moja sijaona wakiweka barabara ya rami,kipindi cha kiangazi ni vumbi hadi chumbani,kipindi cha mvua ni kukanyaga maji ya mvua nje yaliyochanganyika na maji taka yaliyoziba kwa sababu ya uchakavu wake ,maana nahisi toka wahindi waijenge enzi hizo hadi leo haijaweza kurekebishwa na watu ndo ivyo wanazidi kuongezeka,Sasa hapo Serikali za mitaa zinafanya nini au ziko kwa ajili ya nini.

Achana na hilo,hadi leo tumekosa kabisa wazoa taka wa kuweza kusema taka zinazolewa hakuna,magari ni mabovu yaani sio Gari la takataka ni Gari taka.na wale wanaozoa wenyewe hawana groves,mabuti wala mask za kuzuia harufu ya uchafu,na utakuta wanakaa juu ya uchafu.

Elimu yetu je ikoje,leo hii ukitaka kuomba kazi lazima waandike uwe unajua kiingereza safi cha kuandiaka na kuongea,mimi kajamba nani vyeti ninavyo lakini School bus huko sekondari na primary sijapanda(yaani sijasoma shule ya kizungu)hivyo kiingereza changu si salama sana. Na watu kama mimi hapa bongo tuko wengi kuliko hao waliopanda School bus,sasa hapo hauoni wametutenga?.

Mimi nasema viongozi wetu wanabahati sana,wanatoa ahadi na hawatekelezi vilevile lakini wananchi wao tumetulia tuli kama maji mtungini tukiomba ipo siku tutakuwa kama angalau mazingira kama Ulaya(Lol)

Umewahi kutembelea mbuga za wanyama kama mkiwa group hivi mmetoka Dar mnakwenda huko,labda vyumba mlivyofikia jirani na vyumba vya wazungu watalii,basi mkiongea na kucheka kwa nguvu,wahudumu wanawafuata,nyie mbona mnapiga makelele kuna wageni watawashangaa.mnyamaze au tutawahamisha,lakini huko mnawasikia hao wageni wazungu wakiongea na kupiga makelele kweli,wangine wanaimba na kucheza hadi usiku kweli,tena nyie mlionyamaza sasa hata usingizi mnakosa kuwasubiri hao wageni hadi nao wachoke walale.Sasa sielewi makelele ya wazungu watalii ni mazuri kuliko makelele ya Wa Tz watalii.

Kuna vitu vingi sana vinaumiza Bongo,kama Rushwa,Kodi kubwa zinazomuumiza mTanzania,Mikataba inayonufaisha wachache n.k

Wadau mimi nafikiri hii Blog inasomwa hata na Serikali yetu sasa tunaweza labda kuwapa maoni wafanye nini ili na sisi tuwe na unafuu hapa Nchini kwetu.

Mdau Dar es Salaam

Tatizo la Maji Dar!


Hivi jamani, kwa nini baada ya siku kumi maji bado ni tatizo mjini Dar es Salaam. Na ni miaka mingapi baada ya Uhuru? Ni aibu kwa Dar kuwa na tatizo la maji kama Harare au Monrovia enzi za vita! Aibu kubwa sana.

Wale wataalam wa maji waliosomeshwa na Chuo cha Maji nk. wako wapi? Kuna nini hasa kinachofanya maji yaye ya shida hivyo wakati tumebarikiwa ma maziwa makubwa kama Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa na mito kibao!

Nakumbuka enzi zile sisi tuliokuwa tunaishi Chuo Kikuu cha DSM tulikuwa tunachekwa kwa sababu ya matatizo ya maji. Walikuwa wanashindwa kuyapandisha mlimani eti.

Serikali infanya nini kutatua matatizo ya maji? Wasipofanya kitu tutasikia watu wanaugua kipindupindu na magonjwa mengine ya kuharisha.


*****************************************************

Kutoka ippmedia.com

Dar vendors pray for prolonged water scarcity

2008-12-18
By Correspondent Gadiosa Lamtey

An acute water shortage that had hit Dar es Salaam and its outskirts for the past ten days, had turned into a blessing in disguise for others.

Vendors selling the precious liquid have been making lucrative business, praying for the scarcity to continue a little bit longer.

A vendor, Hamisi Majaliwa, said God had listened to their prayers as they could now afford to celebrate the year end festivals.

``The scarcity guarantees my daily bread. I no longer worry about celebrating Christmas because I have earned quite a sum over the past few days,`` said Majaliwa.

A survey conducted by The Guardian across the country`s commercial hub found out that the scarcity was getting worse, with a 20-litre gallon of tap water selling at between 800/- and 1,000/- respectively.

The high prices have forced some low income earners in the city to resort to drawing water from the drainage system, thus inviting grave health risks.

Margaret Richard, a resident of Ubungo suburb, said she resorted to buying bottled water as it was safe to cook and brush her teeth with.

``I am skeptical with the water sold by street vendors,? said Margaret.

She said the scarcity had made vendors fetch water from any place for the sake of money, while ignoring all the health risks.

``Worse still, their prices are unfair,`` she said. Margaret, however, wondered how the unemployed and housewives afford buying water from street vendors.

``I can`t blame vendors because survival is for the fittest. Everyone must earn their bread. However, I call upon Dawasco to speed up their efforts to restore water supply.

Dar es Salaam is densely populated. No one will survive should it happen that there is a cholera outbreak,`` said Margaret.

Alfa Laizer of Kinondoni said some people had already suffered after consuming salty water drawn from shallow wells.

Laizer said: ``Salty water is only good for washing clothes and house cleaning, but you can`t use it to cook or drink. Some people are already becoming allergic from bathing salty water.``

``We are not comfortable with what is going on, although we are aware what the problem is.

The authorities should find a solution before the situation gets worse, especially for children,`` he said.

A resident of Chang`ombe, Fatuma Kamugisha, said water had become as precious as gold but the digging of boreholes had in a way helped to avert the problem.

When contacted for comments, Dawasco public relations officer Mary Lyimo said their engineers were busy working on a defective transformer.

``Since last Saturday, our engineers have been tirelessly working on the transformer and by tomorrow (yesterday) things will be back to normal,`` she confidently said.

Last week, Dawasco announced that the city would temporarily go without water because of a defective transformer that supplies power to water pumps at Lower Ruvu.

As we went to press, Dawasco public relations officer Mary Lyimo said water supply had been restored in several Dar es Salaam suburbs, except Magomeni, Sinza, Mwenge and Ilala.

She said problems affecting such areas would be sorted out within the shortest possible time
``It will not take long to normalize the city supply. The delay has been caused by low pressure from our pumping machines,`` she said.

SOURCE: Guardian

Watoto wafa Nigeria baada ya Kupewa Dawa enye Sumu!

Hao watu wanaofikiria pesa kabla ya usalama wa watoto wana dhambi ile mbaya. Kuna habari kutoka Nigeria kuwa wataoto karibu 30 wamekufa baada ya kupewa Gripe water enye sumu. Sumu enyewe ni 'anti freeze' ambayo tunaweka kwenye magari yetu hapa Marekani wakati wa msimu wa baridi!

Nina wasiwasi na Tanzania itakumbwa na mkasa kama huo tusipokuwa makini, kwani wanasema kuwa ni counterfeit/fake dawa ambayo tayari imekuwa tatizo.

Mungu alaze roho za watoto waliokufa mahala pema mbinguni. AMEN
.

**********************************************************************************

LAGOS, Nigeria (CNN) -- Nneka and Chimezie Ononaku unwittingly poisoned their own four-month-old son Chinonso. Giving him what they thought was a baby teething medicine, they were in fact dosing him with anti-freeze.

The bottle had been contaminated with a toxic chemical called diethylene glycol.

More than 30 Nigerian children are thought to have died recently after taking the medicine. Nneka is angry.

"It's not easy carrying a pregnancy for nine months, [and] after that getting a drug from a pharmacy to kill your own child," she says.

When Nigeria's Agency for Food and Drug Administration and Control (NAFDAC) tested the medicine, "My Pikin," the results were terrifying.

It found the medicine contained almost 90ml of diethylene glycol per 100ml.

"It's a bottle of poison," the NAFDAC laboratory said.

The "My Pikin" factory's managing director and eight others have been charged with negligence. The company could not be reached for comment.

Undercover NAFDAC officers have taken to the streets in order to combat unregistered and often harmful drugs. Hawkers are charged with selling counterfeit drugs and forced to pay a fine.

NAFDAC claims most of the counterfeit drugs come from India and China.

And it's big business -- America's Centre for Medicines in the Public Interest predicts counterfeit drug sales will reach $75 billion in 2010.

NAFDAC's director-general Dora Akunyili warns counterfeiting is not just a Nigerian problem.

"These criminals are cooperating, so we too need to cooperate if we can face them. Not only in Nigeria but internationally, because drug counterfeiting involves a trans-national criminal network and can only be dismantled through international co-operation."

Wednesday, December 17, 2008

Rest in Peace - Prof. Aggrey Nzali

Marehemu Prof. Aggrey Nzali

Nimepokea habari hii leo kwa masikitiko mno. Prof. Nzali alifariki mwezi Oktoba baada ya kupata ajali ya gari.

Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. AMEN.
Kwa habari zaidi tembelea Jamii Forums:
http://www.jamiiforums.com/matangazo-madogomadogo/19728-prof-nzali-afariki-dunia.html
*******************************************************
Wadau,

Nimesoma habari ambayo kwa kweli ni vigumu kuamini.

Ninaomba sana mwenye taarifa juu ya Prof. Aggrey Nzali wa Department of Engineering UDSM anitumie e-mail chemiche3@yahoo.com.

Prof. Nzali alikuwa rafiki wa marehemu mume wangu Prof. Henry Kadete, tulikuwa naye Uholanzi mwaka 1986 na alisimamia ubatizo wa mwanangu.

Casting Call - Beauty and the Geek

Boston Casting Inc. is looking for Men 21-30 ETHNICALLY OPEN with high IQ's for the hit reality show "Beauty and the Geek".

Spend the month of January in L.A. living in a mansion with beautiful girls and a chance to win a cash prize of $250,000.

Auditions are taking place thurs.12/18 and friday 12/19.

EMAIL: Ashley@bostoncasting.com

Kipanya Asema

Translation:

President Bush: Duh! So shoes are also weapons. From now on when I give a speech, people in the hall must be naked!

Casting Call - Uingereza

Actors needed

TimeLine Media are looking for both male and female actors to play different roles in upcoming Tanzanian Film based in England.

Applicants must be black or mixed race with the ability to speak and understand Swahili. East African Swahili can also be considered.20-35 playing age.

We have huge demand for NEW talent including extras in a wide variety of roles for this film.
If you would like the opportunity to audition you could either attend auditions on 21st December 2008 at:

Tropicana Club53 Cheapside LutonBedfordshire LU1 2HN
Or you could contact Nassir Mohammed on 07971224493 for more information or send your details to nassirmo@gmail.com

Please don’t hesitate to contact us for more information if you could not attend the date mentioned above.

NOTE: Experience preferred but not needed.

Filamu na Tamthiliya zinapotosha Waadili

(Pichani l-r Kathy Flewellen, Geri Augusto, naWalter Bgoya 1974)

Nakubaliana nao kabisa. Mnakumbuka miaka ya sabini Mwalimu alipopiga maarufuku mtindo wa 'Jiving' na kuimba nyimbo za kizungu. Alisema kuwa si maadili yetu na pia alitaka tukuze utamaduni wa Tanzania. TV na filamu za nje zilikuwa marufuku. Mnakumbuka kulikuwa na censorship board chini ya Tanzania Film Company.

***************************************************************
Na Beda Msimbe (Lukwangule Entertainment Blog)

TAMTHILIYA zinazoonyeshwa katika vituo mbalimbali vya televisheni, zimeelezwa kuwa ndiyo chanzo cha kuharibu jamii na kusababisha wanajamii wengi kuiga utamaduni wa magharibi badala ya ule wa Tanzania na Afrika.

Hayo yalisemwa na Godfrey Mngereza, kutoka Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA wakati akichangia mada kwenye mkutano wa sita wa Sekta ya Utamaduni, unaoendelea kwenye Hoteli ya Oasis mjini Morogoro.

“Ikifika nyakati za usiku, watoto wetu hasa wasichana wamekuwa wakiangalia tamthiliya ambazo nyingi zinakuwa haziko katika maadili ya Kitanzania, hizi ndizo zinasababisha kuporomoka kwa maadili ya kitanzania.

Mngereza alisema kuwa kuna kila sababu ya televisheni mbalimbali kuonyesha tamthiliya zenye kuonyesha maadili na utamaduni wetu. “Mfano, tunataka kuona televisheni ya taifa, TBC1 inapigania maadili mazuri ya utamaduni, lakini si kuwa mfano mbaya katika ujenzi wa maadili,” alisema.

Alisema pia kuwa vibanda vya mitaani vinavyoonyesha sinema, vimekuwa chanzo cha kumomonyoka kwa maadili kwa kuonyesha filamu za ngono. “Utashangaa watoto hawaendi kulala na utasikia wanakwenda kwenye pilau…wenyewe wanaziita hizi filamu za ngono pilau, sasa huwezi kuelewa, lakini wenyewe wameshazipa jina,” alisema.

Naye mtunzi na mchapishaji wa vitabu, Walter Bgoya alisema kuwa Tanzania imeendelea kuwa jalala la filamu za Kinaijeria hata kama hazina ubora na nyingine hazifundishi.
Alisema wasanii wa Tanzania hawana mbinu wala hawawezi kutengeneza filamu bora ndiyo maana kumekuwa na kumwagika kwa filamu hizo. Hata hivyo, alisema kuwa wasanii wa Tanzania wanatakiwa kujifunza zaidi mbinu za kisasa na kuweza kutengeneza filamu bora.

Bgoya alisema kuwa wasanii wa Tanzania hawataki kusoma na kuongeza wigo wa kujifunza. Hii ni wazi kuwa wanatakiwa kusoma sana ili kuweza kutengeneza mwongozo bora utakaotoa filamu bora.

Akizungumzia utandawazi, Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa Tanzania , BASATA, Ghonche Materego alisema kuwa Watanzania wameathiriwa na utandawazi na sehemu kubwa huendesha utamaduni kwa kuangalia umagharibi.

“Hata wasanii wa bongo fleva, wamekuwa wakifanya kazi zao kwa kuangalia mitindo ya mataifa ya Magharibi, hatuwezi kukwepa utandawazi, utaendelea kuharibu jamii ya wasanii kwa kuiga.

Monday, December 15, 2008

Funga Mwaka Arusha


MWANAFA, AY NA C4 DJS UNIT KUFUNGA MWAKA ARUSHA

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Ambwene Yesaya (AY) na Hamis Minyijuma (MwanaFA) wanaotesa katika anga ya muziki kwa sasa, wanatarajia kutoa burudani ya aina yake kwenye uzinduzi wa kundi la C4 DJs linaloundwa na wachezeshaji muziki ambalo linatarajiwa kuzinduliwa rasmi katika mkesha wa sikukuu ya Krismas ndani ya Ukumbi wa Triple ‘A’ jijini Arusha. Kundi hilo linaundwa na Ma-DJ wenye uzoefu wa siku nyingi wakiwemo DJ Joe, DJ Peter, DJ Gerry na DJ A-Plus. Pia kutakuwa na Madj wengine wakali kusindikiza uzinduzi huu wa aina yake.

Aidha maandalizi kwa ajili ya uzinduzi huo na sherehe za funga mwaka yanaendelea vizuri hivyo mashabiki wakae tayari kupata burudani ya aina yake. Uzinduzi huu ndiyo mwanzo wa mfululizo wa burudani ndani ya Ukumbi wa Club Triple ‘A’ hadi mwaka 2009.

MaDJ hao wa kitanzania waliobobea katika fani hiyo wameamua kuzindua umoja huo ili kuonyesha kwamba wapo pamoja na watatoa kipaumbele kwa wahusika wote katika tasnia hii. Baada ya uzinduzi kutakuwa na program ya burudani kabambe ndani ya Ukumbi wa Triple ‘A’.
Siku ya Krismasi kundi la C4 litaandaa onyesho litakalofahamika kama ‘White Party’ambapo wateja watakaopendeza ndani ya mavazi meupe watapewa zawadi kemkem za papo kwa papo.
Na kwa mara ya kwanza katika historia ya burudani katika Ukumbi wa Triple ‘A’ Arusha kutakuwepo na shindano la kumsaka malkia wa Desemba (Miss Desemba). Shoo hiyo itafanyika usiku wa tarehe 26 Desemba. Shoo hii ya aina yake itawahusisha warembo kumi wenye vipaji mbali mbali.

Burudani ya Funga Mwaka katika jiji la Arusha inatarajia kuleta mageuzi makubwa katika fani ya muziki na burudani nchini Tanzania.

Funga mwaka hii itatoa fursa kwa C4 DJs kupata fursa ya kuonyesha umahiri wao katika kupangilia muziki ikiwa ni moja ya lengo la kuendeleza fani hiyo ya muziki ambao ulishika chati zaidi katika miaka ya 80 na 90 kabla muziki wa dansi haujateka soko na watu kuwapa kisogo maDJ.

Katika kuhitimisha Funga Mwaka Kundi la C4 limeandaa bonge la Bethdei party kwa ajili ya kusherehekea mafanikio ya Club Triple ‘A’ zaidi ya miaka kumi.

JOSEPH NAMALOWE (DJ JOE)
MRATIBU

Rais Bush arushiwa Viatu


Jana Rais Bush, alienda kutembea Iraq kimya kimya bila kuaga hapa Marekani. Tulivyosikia habari kuwa yuko Iraq walisema kuwa eti alienda kuaga huko kwa hiyo siku zake za kuwa rais karibu zinaisha.

Kufika jioni tukasikia kuwa rais Bush alikuwa kwenye mkutano na waandishi wa habari wa Iraq na mojawao alimrushia viatu vyake kwa hasira na kumtuka Bush kuwa eti ni mbwa! Kwa kweli watu wengi hapa walicheka. Mbavu hawana. Kisa huyo Bush hapendwi kwa jinsi alivyoharibu nchi na kuchafua jina la Marekani kwa nchi za nje. Kati ya marais wote 43 wa Marekani yeye Bush Jr. ndo hapendwi kuliko wote katika historia ya Marekani.

Watu wengine wanasema kuwa bado ana siku 37 za kukaa kama rais, na tutasikia vituko vinginwe. Mambo Bado. Sijui Letterman, Leno na Saturday Night Live watasema nini kuhusu hii tukio la viatu.

Kwa habari zaidi someni:

Saturday, December 13, 2008

Kesho nitakuwa kwenye TV show - Brotherhood


Wadau,
Kesho jumapiili Desemba 14, 2008, nitakuwa kwenye TV Show iitwayo Brotherhood. Inaonyeshwa kwenye Showtime. Nimejiona kwenye trela ya kipindi cha kesho saa 2 jioni (8:00pm Eastern). Baada ya kesho itakuwa kwenye cable kwenye On Demand.
Mimi ni 'extra' (background) hivyo siongee. Nitakuwa kwenye scene ambayo mafioso Nozzoli anaongea na Tommy mhusika mkuu wa Brotherhood kwenye mgahawa. Nimekaa nyuma ya Nozzoli nakunywa kahawa, nimevaa koti ya jeans.

Friday, December 12, 2008

Zilipendwa ziko kwa Da Subi

Zilipendwa za RTD hizi hapa...

Zimepatikana zile za enzi ile ya External Service of RTD, Kijaluba hoyeee, (na watangazaji mahiri Mikidadi Mahamoud, Uncle J Nyaisanga...) na matangazo ya Vicks Kingo na sijui Meza Action mara ukiumwa na misuli tumia Salimia Liniment... tangazo la Revola (Vipi Mama Mariam! mbona unalalamika hivi? Ah, nguo hizi, kila ninapokazana kuzifua, hazitakati sijui nitumie nini?)...., zile hadithi za Bi Deborah Mwenda za Ua Jekundu, Binti Chura, Mbalamwezi Nyota Begani nk..... kiasi zipo: http://nukta77.com/burudani.aspx ama http://nukta77.blogspot.com/ (mwisho wa ukurasa).....Wikiendi njema! -Subi

Asante sana Da Subi!

Msimu wa Mafua


Wadau samahani kwa kuwa mvivu wa kuposti wiki hii. Nimekumbwa na mafua. Kichwa kinauma. Macho yanawasha. Nakohoa. Ofisini karibu kila mtu anakohoa na kupiga chafya ovyo. Tunamlaumu aliyetulea huu ugonjwa, tunamhisi mtu aliyeipata kutoka kwa mtoto wake ambaye yuko vidudu. LOL! Huenda kuna mtu kambukizwa kwenye treni (subway) utajuaje? Mafua ni malaria ya Marekani.

Tuesday, December 09, 2008

Machifu wa Kingoni walivyonyongwa 1906




Wadau, niliwahi kuanzisha mada hapa kuhusu machifu wa Kingoni walionyongwa na Mjerumani hapo zamani za kale. Niliona hii article kwenye Habari Leo. Ushenzi wa Mkoloni!

*********************************************************

Mashujaa ya Kingoni Walizikwa bila Sanda katika Kaburi Moja
Juma Nyumayo
Daily News; Sunday,August 10, 2008

Wiki iliyopita tuliona vivutio mbalimbali vilivyopo mkoani Ruvuma, kama vile mto Ruvuma, Ziwa Nyasa, Mlima Matogoro na mji mdogo wa kihistoria wa Peramiho. Pia, tuliona kwa ufupi juu ya Jumba la Makumbusho lenye sanamu za machifu 12 wa Kingoni. Leo tunaendelea na sehemu ya mwisho ya simulizi hii.Upande wa kulia wa Jumba hilo la Makumbusho, kuna majina ya mashujaa waliopigana Vita ya Maji Maji mwaka 1905-1907na majina yote hayo yanaanza kufutika.

Katika jumba hilo kwa nyuma, kuna kaburi la pamoja ambalo walizikwa mashujaa 57.Miongoni mwa mashujaa hao 57, kulikuwa na Chifu mmoja na machifu wasaidizi (Nduna) saba.Chifu Songea Mbano alizikwa kaburi la peke yake.Mashujaa wengine 10 kati ya hao 57, majina yao hayakupatikana, hivyo majina yaliyopo ni 47 tu.

Mashujaa hao wa Kingoni pia walipigana Vita ya Maji Maji mwaka 1905 – 1907 na walinyongwa jirani na eneo hilo.Eneo hilo kuna miti mitatu na kamba walizonyongewa, kwa ajili ya kumbukumbu. Katika eneo hilo, kuna ukumbi maarufu mjini Songea wa Songea Club.Baada ya kunyongwa katika eneo hilo, mashujaa hao walizikwa bila sanda katika kaburi la pamoja kwenye jumba hilo la makumbusho.

Mashujaa hao walinyongwa Februari 27, 1906, ambapo Februari 27 kila mwaka, Mkoa wa Ruvuma huwa na sikukuu ya mashujaa ya kuwakumbuka mashujaa hao wa Kingoni.Kwa mujibu wa Kitabu cha Harakati za Ukombozi wa Mkoa wa Ruvuma, mashujaa hao walikuwa wakibatizwa kabla ya kunyongwa. Lakini, Chifu Mpambalyoto alikataa kubatizwa, akidai kuwa haina maana yoyote kubatizwa halafu nanyongwa. Padri aliyekuwa akibatiza mashujaa hao wa Kingoni, aliitwa Yohanes.

Katika eneo hilo walikonyongewa mashujaa hao, huimbwa nyimbo mbalimbali za maombelezo katika maadhimisho ya kuwakumbuka mashujaa hao. Nyimbo hizo huimbwa kwa lugha ya Kingoni.Nyimbo hizo za maombolezo ni kama zile nyingine zinazoimbwa kwenye misiba mingine.Kitabu hicho kinasema kuwa mashujaa hao waliaga kabla hawajanyongwa, kwamba wataonana ng’ambo.

Wengine waliomba wavute kwanza ugoro (tumbaku) kabla hawajanyongwa.Katika mashujaa hao wa Kingoni, wanne walinyongwa kwa mkupuo jirani na eneo lililoitwa Boma la Wajerumani, ambako leo ndiko kuna ofisi za Mkoa wa Ruvuma.Leo hii hakuitwi Bomani tena, bali Mkoani; wakati na eneo ambako walinyongewa mashujaa wengine wengi, kunaitwa Songea Club.

Hata hivyo, jumba hilo la makumbusho liko katika hali mbaya, kwani rangi iliyopo kwenye sanamu ya askari aliyeshika bunduki, imechujuka.Jumba hilo la mashujaa limezungushiwa wigo na ndani yake kuna majengo matatu, yaani jengo kubwa na mengine mawili madogo.Jengo kubwa ni la ghorofa moja na liko katikati. Majengo madogo mawili yako pembeni mwa jengo hilo kubwa. Majengo yote hayo matatu, yamejengwa kwa mtindo wa mviringo, kama nyumba nyingi za watu wa mkoa huo zilivyokuwa zikijengwa.

Mwenyekiti Kamati ya Utendaji ya Baraza la Makumbusho, Said Mkeso, anasema kwamba jengo kubwa ni maalumu kwa ajili ya kuhifadhi utamaduni wa kabila la Wangoni, ambao maskani yao ni Songea mjini.Jengo moja dogo ni kwa ajili ya kuhifadhi utamaduni wa kabila la Wamatengo, ambao maskani yao ni wilaya ya Mbinga.Jengo dogo la mwisho ni kwa ajili ya kuhifadhi utamaduni wa kabila la Wayao, ambao maskani yao ni wilaya ya Tunduru.

Mkeso anasema jengo linalotumika ni moja tu kubwa, linalohifadhi utamaduni wa kabila la Kingoni.Majengo mawili madogo, yameachwa tupu, baada ya kukosekana vifaa vya makumbusho vya makabila ya Wayao na Wamatengo.Jumba hilo la makumbusho liligunduliwa mwaka 1962 na Mkuu wa kwanza wa mkoa wa Ruvuma, Martini Haule. Aliligundua likiwa limejaa nyasi. Haule alifariki Januari 17, 1993 mkoani Morogoro na kuzikwa eneo la Mahenge mkoani Ruvuma.

Jirani na eneo hilo, kulikuwa na makaburi mengine 65 ya Wajerumani waliouawa kwenye Vita ya Maji Maji. Makaburi hayo yalikuwa yakitunzwa vizuri na kulindwa, ambapo baada ya Tanzania kupata Uhuru Desemba 9, mwaka 1961 ndugu zao walikuja kuyafukua na kuchukua miili waliyokwenda kuizika kwao.

Nje na ndani ya jumba hilo, kuna mambo mengi ya kuvutia, ikiwemo sanamu 12 za machifu wa Kingoni jamii ya Njelu.Majina ya sanamu za machifu hao, waliowahi kutawala Songea miaka ya 1902 ni Mpambalyoto Soko bin Msarawani, Nduna Songea Mbano bin Luwafu, Nduna Chabruma Gama bin Hawayi, Zimanimoto Gama Bin Fusi, Nkosi Mputa Gama bin Gwazerapasi, Nduna Zamchaya Gama bin Gwazerapasi.

Wengine ni Mtepa Ntara bin Kanyoka, Nduna Usangira Gama bin Mharule, Magodi Mbano bin Mbamba, Njorosa Mbano bin Mbamba, Masese Parangu Mbano bin Songea, Nyunyusea Mbano bin Njenje na Njorosa Mbano bin Mbamba.Ndani ya jumba hilo la makumbusho kuna picha kubwa ya Rais wa kwanza wa Zanzibar, hayati Abeid Amani Karume ambaye Februari 5, 1977 Chama chake cha ASP kiliungana na TANU na kuunda Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Pia, kuna picha ya Mwalimu Julius Nyerere akikabidhiwa hati ya Muungano na Rais Abeid Amaan Karume. Pia, kuna picha kubwa ya Nyerere akiapishwa kuwa Waziri Mkuu.Aidha, katika jumba hilo la makumbusho kuna picha kubwa ya mkutano wa wajumbe walioanzisha chama cha TANU Julai 7 1954.Ipo pia picha kubwa ya mnara wa kumbukumbu ya Azimio la Arusha. Kuna pia picha kubwa ya Mwalimu Nyerere akipelekwa mahakamani, kufuatia harakati zake za kudai uhuru.

Eneo jingine linalovutia ni misitu ya miyombo, yenye wanyama na wadudu mbalimbali. Misitu hiyo imeenea na kuunganisha Hifadhi ya Selous na ile ya Niasa nchini Msumbiji ambapo katika eneo la Kilimasera kuelekea Tunduru, kuna ushoroba (corridor) wanayopita wanyama kutafuta chakula. Wanyama hao ni pamoja na tembo wanaovuka kwa makundi makubwa.

Katika wilaya ya Tunduru kuna maeneo ya uwindaji wa kitalii. Uwindaji huo hufanywa zaidi na wageni. Wawindaji wa ndani ya nchi wanatakiwa wahamasishwe ili kufaidi raslimali za nchi.Mbuga ya Mwambesi tarafa ya Lukumbule katika wilaya hiyo ya Tunduru, kwenye bonde la Mto Ruvuma, ni eneo maarufu kwa uwindaji huo.

Wiki iliyopita tuliona vivutio mbalimbali vilivyopo mkoani Ruvuma, kama vile mto Ruvuma, Ziwa Nyasa, Mlima Matogoro na mji mdogo wa kihistoria wa Peramiho. Pia, tuliona kwa ufupi juu ya Jumba la Makumbusho lenye sanamu za machifu 12 wa Kingoni. Leo tunaendelea na sehemu ya mwisho ya simulizi hii.Upande wa kulia wa Jumba hilo la Makumbusho, kuna majina ya mashujaa waliopigana Vita ya Maji Maji mwaka 1905-1907na majina yote hayo yanaanza kufutika.

Katika jumba hilo kwa nyuma, kuna kaburi la pamoja ambalo walizikwa mashujaa 57.Miongoni mwa mashujaa hao 57, kulikuwa na Chifu mmoja na machifu wasaidizi (Nduna) saba.Chifu Songea Mbano alizikwa kaburi la peke yake.Mashujaa wengine 10 kati ya hao 57, majina yao hayakupatikana, hivyo majina yaliyopo ni 47 tu.

Mashujaa hao wa Kingoni pia walipigana Vita ya Maji Maji mwaka 1905 – 1907 na walinyongwa jirani na eneo hilo.Eneo hilo kuna miti mitatu na kamba walizonyongewa, kwa ajili ya kumbukumbu. Katika eneo hilo, kuna ukumbi maarufu mjini Songea wa Songea Club.Baada ya kunyongwa katika eneo hilo, mashujaa hao walizikwa bila sanda katika kaburi la pamoja kwenye jumba hilo la makumbusho.


Mashujaa hao walinyongwa Februari 27, 1906, ambapo Februari 27 kila mwaka, Mkoa wa Ruvuma huwa na sikukuu ya mashujaa ya kuwakumbuka mashujaa hao wa Kingoni.Kwa mujibu wa Kitabu cha Harakati za Ukombozi wa Mkoa wa Ruvuma, mashujaa hao walikuwa wakibatizwa kabla ya kunyongwa. Lakini, Chifu Mpambalyoto alikataa kubatizwa, akidai kuwa haina maana yoyote kubatizwa halafu nanyongwa. Padri aliyekuwa akibatiza mashujaa hao wa Kingoni, aliitwa Yohanes.

Katika eneo hilo walikonyongewa mashujaa hao, huimbwa nyimbo mbalimbali za maombelezo katika maadhimisho ya kuwakumbuka mashujaa hao. Nyimbo hizo huimbwa kwa lugha ya Kingoni.Nyimbo hizo za maombolezo ni kama zile nyingine zinazoimbwa kwenye misiba mingine.Kitabu hicho kinasema kuwa mashujaa hao waliaga kabla hawajanyongwa, kwamba wataonana ng’ambo.

Wengine waliomba wavute kwanza ugoro (tumbaku) kabla hawajanyongwa.Katika mashujaa hao wa Kingoni, wanne walinyongwa kwa mkupuo jirani na eneo lililoitwa Boma la Wajerumani, ambako leo ndiko kuna ofisi za Mkoa wa Ruvuma.Leo hii hakuitwi Bomani tena, bali Mkoani; wakati na eneo ambako walinyongewa mashujaa wengine wengi, kunaitwa Songea Club.

Hata hivyo, jumba hilo la makumbusho liko katika hali mbaya, kwani rangi iliyopo kwenye sanamu ya askari aliyeshika bunduki, imechujuka.Jumba hilo la mashujaa limezungushiwa wigo na ndani yake kuna majengo matatu, yaani jengo kubwa na mengine mawili madogo.Jengo kubwa ni la ghorofa moja na liko katikati. Majengo madogo mawili yako pembeni mwa jengo hilo kubwa. Majengo yote hayo matatu, yamejengwa kwa mtindo wa mviringo, kama nyumba nyingi za watu wa mkoa huo zilivyokuwa zikijengwa.

Mwenyekiti Kamati ya Utendaji ya Baraza la Makumbusho, Said Mkeso, anasema kwamba jengo kubwa ni maalumu kwa ajili ya kuhifadhi utamaduni wa kabila la Wangoni, ambao maskani yao ni Songea mjini.Jengo moja dogo ni kwa ajili ya kuhifadhi utamaduni wa kabila la Wamatengo, ambao maskani yao ni wilaya ya Mbinga.Jengo dogo la mwisho ni kwa ajili ya kuhifadhi utamaduni wa kabila la Wayao, ambao maskani yao ni wilaya ya Tunduru.

Mkeso anasema jengo linalotumika ni moja tu kubwa, linalohifadhi utamaduni wa kabila la Kingoni.Majengo mawili madogo, yameachwa tupu, baada ya kukosekana vifaa vya makumbusho vya makabila ya Wayao na Wamatengo.Jumba hilo la makumbusho liligunduliwa mwaka 1962 na Mkuu wa kwanza wa mkoa wa Ruvuma, Martini Haule. Aliligundua likiwa limejaa nyasi. Haule alifariki Januari 17, 1993 mkoani Morogoro na kuzikwa eneo la Mahenge mkoani Ruvuma.

Jirani na eneo hilo, kulikuwa na makaburi mengine 65 ya Wajerumani waliouawa kwenye Vita ya Maji Maji. Makaburi hayo yalikuwa yakitunzwa vizuri na kulindwa, ambapo baada ya Tanzania kupata Uhuru Desemba 9, mwaka 1961 ndugu zao walikuja kuyafukua na kuchukua miili waliyokwenda kuizika kwao.

Nje na ndani ya jumba hilo, kuna mambo mengi ya kuvutia, ikiwemo sanamu 12 za machifu wa Kingoni jamii ya Njelu.Majina ya sanamu za machifu hao, waliowahi kutawala Songea miaka ya 1902 ni Mpambalyoto Soko bin Msarawani, Nduna Songea Mbano bin Luwafu, Nduna Chabruma Gama bin Hawayi, Zimanimoto Gama Bin Fusi, Nkosi Mputa Gama bin Gwazerapasi, Nduna Zamchaya Gama bin Gwazerapasi.

Wengine ni Mtepa Ntara bin Kanyoka, Nduna Usangira Gama bin Mharule, Magodi Mbano bin Mbamba, Njorosa Mbano bin Mbamba, Masese Parangu Mbano bin Songea, Nyunyusea Mbano bin Njenje na Njorosa Mbano bin Mbamba.Ndani ya jumba hilo la makumbusho kuna picha kubwa ya Rais wa kwanza wa Zanzibar, hayati Abeid Amani Karume ambaye Februari 5, 1977 Chama chake cha ASP kiliungana na TANU na kuunda Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Pia, kuna picha ya Mwalimu Julius Nyerere akikabidhiwa hati ya Muungano na Rais Abeid Amaan Karume. Pia, kuna picha kubwa ya Nyerere akiapishwa kuwa Waziri Mkuu.Aidha, katika jumba hilo la makumbusho kuna picha kubwa ya mkutano wa wajumbe walioanzisha chama cha TANU Julai 7 1954.Ipo pia picha kubwa ya mnara wa kumbukumbu ya Azimio la Arusha. Kuna pia picha kubwa ya Mwalimu Nyerere akipelekwa mahakamani, kufuatia harakati zake za kudai uhuru.

Eneo jingine linalovutia ni misitu ya miyombo, yenye wanyama na wadudu mbalimbali. Misitu hiyo imeenea na kuunganisha Hifadhi ya Selous na ile ya Niasa nchini Msumbiji ambapo katika eneo la Kilimasera kuelekea Tunduru, kuna ushoroba (corridor) wanayopita wanyama kutafuta chakula. Wanyama hao ni pamoja na tembo wanaovuka kwa makundi makubwa.

Katika wilaya ya Tunduru kuna maeneo ya uwindaji wa kitalii. Uwindaji huo hufanywa zaidi na wageni. Wawindaji wa ndani ya nchi wanatakiwa wahamasishwe ili kufaidi raslimali za nchi.Mbuga ya Mwambesi tarafa ya Lukumbule katika wilaya hiyo ya Tunduru, kwenye bonde la Mto Ruvuma, ni eneo maarufu kwa uwindaji huo.

Ni Dhambi kula kwa Mama Ntilie?

Jamani! Hivi ni dhambi kula kwa Mama Ntilie? Ni lazima kula chakula cha kizungu kwenye hoteli za kifahari ili uonekane mtu? Khaa! Sielewi kwa nini magazeti wanamchora mrembo Miriam Odemba kwa kula kwa Mama Ntilie. Nakumbuka nilivyokuwa Daily News kulikuwa na Mama Ntilie waliokuwa na chakula kizuri kweli kweli tena kitamu! Of course usafi ni muhimu, na wengi walijitahidi kwa usafi kuliko hata ungekula hotelini.

Wadau mnaonaje?

Uhuru 9-12-61

Bendera ya Tanganyika


Uhuru wa Tanganyika ulikuwa Disemba 9, 1961. Ni miaka 47 iliyopita. Pichani ni mezi kadhaa kabla ya uhuru mwaka 1961, Mwalimu akiwa na Mama Barbro Johansson nyumbani kwake Kahororo, Bukoba. ( Picha kwa hisani ya Maggid Mjengwa Blog)

Ufisadi Marekani - Gavana wa Illinois Akamatwa!

Gavana wa Illinois, Rod Blagojevich

Ni aibu kweli hapa Marekani kusikia kuwa Gavana mzima kakamatwa kwa kuomba rushwa! Yaani ni jambo la aibu sana.

Habari zinasema kuwa Gavana wa Illinois, Rod Blagojevich alikuwa anauza nafasi ya uSenator ambayo iko wazi kwa vile aliyekuwa na kiti hicho, Barack Obama ni rais mteule. Gavana ndiye ana wajibu wa kumteua mtu wa kuchukua nafasi aliyoacha Obama.

Wanasema pia kuwa alikuwa anamtafutia mke wake kazi nono.

Kwingine, haya ni mambo ya kawaida, lakini kwa Marekani haya makosa ni makubwa kweli kweli. Itabidi ajiuzulu kama wa ushahidi kuwa ni kweli kaomba rushwa!

Kwa habari zaidi someni:

Monday, December 08, 2008

Vifaa Vya Jikoni


Badala ya kwenda SEARS, Best buy, Ikea, Pier 4 etc. kununua vifaa vya jikoni, nyumbani tunaenda dukani au gengeni kupata mahitaji yote!

Kipanya Asema

Top Left - Kipanya (Rat Character): You are a Minister and a crook, JK must imprison you!

Top Right- Minister: I agree that I will go to jail but do you remember when I was the Minister of Finance?

Botton Left- Minister: I forgave your taxes on that business of yours, so you are a tax evader!

Botton Right: Kipanya: Okay it's over with let's start afresh.

Ndugu wa Marehemu Nampelenga Wanatafutwa!


MAREHEMU ANTHONY EMMANUEL NAMPELENGA


JUMUIYA YA WATANZANIA WAISHIO ITALY INASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA NDUGU YETU ANTHONY EMMANUEL NAMPELENGA KILICHOTOKEA SIKU YA JUMATANO KATIKA HOSPITALI YA PINETA GRANDE CASTELVOLTUNO CASERTA, ITALY.

MAREHEMU ANTHONY AMBAYE PIA ALIJULIKANA KWA JINA MAARUFU LA MMACHINGA, ALIZALIWA TAREHE 12/07/1963 HUKO MKOANI LINDI.

SABABU YA KIFO CHA MAREHEMU INASEMEKANA ALIANGUKA NA WASAMARIA WALIOKUWA KARIBU WAKAITA GARI LA WAGONJWA NA AKAPELEKWA HOSPITALI AMBAKO ALIFANYIWA OPERESHENI YA KICHWA.

TANGU SIKU YA JUMATATU 1/12/2008 ALIYOANGUKA ALIKUWA KATIKA KITENGO CHA WAGONJWA MAHUTUTI AMA ICU, HADI JIONI YA JUMATANO WAKATI MWENYEKITI WA JUMUIYA ALIPOPATA SIMU KUTOKA HOSPITALI HAPO NA KUPEWA TAARIFA YA KIFO CHA MMACHINGA.

TUNAOMBA YEYOTE MWENYE MAELEZO YA ANUANI YA NDUGU ZAKE ATULETEE HARAKA ILI HATUA MUHIMU ZA MSIBA HUU ZICHUKULIWE.
IMETOLEWA NA:
JUMUIYA YA WATANZANIA ITALY

Saturday, December 06, 2008

Kweli Kabisa!



Kama umewahi kuingia kwenye elevator na mzungu ni lazima muangalie hii:

http://www.youtube.com/watch?v=p95zWsAmTyw

Friday, December 05, 2008

Miss Uganda

(Pichani ni Miss Uganda 2008)

Wadau, hivi kwenye mashindano ya Miss Tanzania kuna kigezo cha Urefu? Katika Miss Uganda kuna kigezo kuwa mshiriki ni lazima awe na urefu wa futi 5'7" na zaidi.

http://missugandapageant.com/

Askari




Bila shaka wengi wenu mna ndugu ambao walikuwepo vikosi vya askari. Hii picha ya kikosi cha askari kilipigwa enzi za mkoloni (mjerumani) mwaka 1914. Sijui ni Mirambo Barracks, Tabora hapo?

Ni Binadamu au Sokwe!


Jamani kuna wazungu wana manywele mwili mzima Duh! Huyu ni mcheza sinema maarufu, Andy Garcia!

Wednesday, December 03, 2008

Safari Food




Waheshimiwa Yona na Mramba watoka jela

Hatimaye mawaziri wa zamani, Mh. Basil Mramba na Mh. Daniel Yona, wamefanikiwa kutoka jela kwa dhamana. Tuone kesi itaishaje.

*******************************************************************
Kutoka ippmedia.com

Mramba, Yona warejea uraiani

2008-12-03
Na Hellen Mwango na Joseph Mwendapole

Mawaziri waandamizi wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona ambao wanakabiliwa na kesi ya kutumia madaraka vibaya jana waliachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kutimiza masharti.

Hata hivyo, watuhumiwa hao walizongwa na wananchi wenye hasira baada ya kuachiwa, huku wengine wakitoa maneno ya kuwakejeli na hata kudiriki kuzonga magari yao walikuwa wamepanda.

Umati mkubwa uliokuwa nje ya Mahakama, ulikuwa ukizomea kwa kuwaita `wezi hao...`wezi hao` na kugonga gonga vioo vya magari yaliyowabeba washitakiwa hao, ambayo yaliondolewa kwa kasi kutoka eneo hilo la Mahakama.

Mara baada ya kuachiwa, Mramba alipanda Land Cruizer GX namba T521 AFS ambalo lilikuwa limeegeshwa mbele ya mlango wa kuingia kwenye mahakama hiyo na Yona alipanda gari aina ya Suzuki Vitara T822 ANR lililokuwa limeegeshwa mbele ya gari la Mramba.

Mpaka kufikia jana, washitakiwa hao walikuwa wamekaa gereza la Keko kwa siku saba baada ya shauri lao la dhamana kuwa gumu.

Tafrani hiyo ilitokea nje ya mahakama hiyo mara baada ya Hakimu Mkazi Hezron Mwankenja kukubali hati za dhamana za washtakiwa na kutangaza kuwa, watakuwa nje kwa dhamana mpaka Januari 2, kesi hiyo itakapotajwa.

Mshitakiwa wa kwanza, Mramba alifanikiwa kupata dhamana baada ya kuwasilisha hati za mali zenye thamani ya Sh. bilioni 3.1, na Yona zilikuwa na thamani ya Sh. bilioni 3.063.

Washitakiwa hao walitakiwa kujidhamini kwa kutoa fedha taslim Sh. bilioni 2.9 kila mmoja au mali zenye thamani kama hiyo.

Walifikishwa mahakamani hapo jana saa 1:20 asubuhi, lakini shauri lao lilianza kusikilizwa na Hakimu Hezron Mwankenja saa 5:00 asubuhi katika ukumbi namba mbili wa mahakama hiyo.

Mawakili wanaowatetea washtakiwa, waliwasilisha hati za mali mbele ya hakimu huyo ambaye baada ya kuzipitia, alisema hana shaka nazo.

Hakimu Mwankenja alisema amezipitia hati hizo kwa msaada wa waendesha mashitaka na mawakili na kubaini kuwa hazina kasoro.

Alisema kila mshitakiwa ametekeleza masharti yote ya dhamana aliyopewa na mahakama hiyo na kwamba hati hizo zitatunzwa na mahakama hadi mwisho wa kesi hiyo.

Baada ya kusema hayo, Hakimu Mwankenja aliwaamuru washitakiwa kusimama na waliposimama, alitangaza watakuwa nje kwa dhamana.

Baada ya hakimu kutangaza washitakiwa watakuwa huru, baadhi ya ndugu na jamaa walisikika wakimshukuru Mungu na wengine wakisali.

Baada ya mahakama kumaliza kazi zake, askari Magereza walianza kuwafukuza watu waliokuwa wamefurika katika ukumbi huo ili waweze kuwapitisha washitakiwa kuelekea nje ya Mahakama.

Hata hivyo, watu hao badala ya kwenda nje ya Mahakama kama walivyoamriwa, walibaki katika viambaza vya mahakama hiyo wakisubiri kuwaona washitakiwa kwa karibu zaidi.

Baada ya nusu saa hivi, washitakiwa walitolewa nje ya Mahakama wakiwa chini ya ulinzi mkali wa askari Magereza wakiwa wamezungukwa na mawakili wao.

Walipopanda kwenye magari yao, baadhi ya watu waliokuwa nje ya mahakama hiyo, walianza kupiga kelele za `wezi hao`...`wezi haoo`, huku wengine wakigonga gonga vioo vya magari hayo.

Hata hivyo, washitakiwa hao hawakupata madhara yoyote kwani madereva waliyaondoa magari hayo kwa kasi ili kuepusha vurugu zaidi.

Washitakiwa hao wanadaiwa kutumia madaraka yao vibaya na kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7.

Kusoma story nzima BOFYA HAPA:

Sasa Aninitwa ' Hasheem the Dream'

Wadau, kijana wetu Hasheem anapanda kwenye charts za Basketball hapa Marekani. Naona karibu tutamsikia kwenye NBA!

*************************************

Kutoka Sports Illustrated.com


Hasheem The Dream

The odyssey of Hasheem Thabeet began in one of the most remote hoops hinterlands. Soon, perhaps, it will take the UConn 7-footer to an unimaginably big stage -- bigger even than the first round of the NBA draft.

Living up to a name that means "destroyer of evil" in Arabic, Thabeet is a record-breaking shot blocker.

Thabit Manka is up on the back step of his house in Dar es Salaam, Tanzania, for good reason: If he posed on level ground with his eldest son, their height difference would be accentuated to the point of absurdity. Even like this, in the last photo they would ever take together, the top of Thabit's kufi only meets the giant boy's shoulders. It's April 2004, and the son, 17-year-old Hashim Thabit Manka, as his name was written then, is seven feet of limbs drowning in baggy jeans and a retro Philadelphia 76ers shirt, staring straight into the camera with only the faintest hint of a smile. The father's billowy kanzu and the gray edges of his facial hair give him a regal air at the age of 56; he is grinning, with his gaze fixed slightly off to the left.

Thabit was an architect, educated in England at the University of Bath and Oxford. He was a lover of soccer, world geography and English Scrabble, all of which he taught to Hashim. Thabit was also a diabetic, and when he fell ill in the days after the photo was taken, complications led him to be hospitalized and, in a week's time, took his life.

Hashim kept the picture in a scrapbook under his bed during his freshman year at Connecticut but has since returned it to his mother, Rukia, for safekeeping in Tanzania. He remembers his father now for his wisdom. Thabit had showed him maps of his travels through Africa, Europe and Australia, and said that their family identity -- being Tanzanian, Swahili-speaking, Muslim -- should never be a limitation. "You can live anywhere as long as you can get along with anybody," he told the boy. "You just have to adapt and overcome."

Four years ago Thabit couldn't have foreseen the odyssey in store for Hashim, who was in just his third year of organized basketball in soccer-mad Tanzania, which had never sent a soul to the NBA, much less the NCAA. Who could concoct a narrative that begins with a boy doing runway modeling in Dar es Salaam to earn money for his fatherless family, continues with him trying to get a basketball scholarship by e-mailing U.S. colleges he randomly Googled in an Internet café and ends with him in Storrs, Conn., as the starting center on a Top 5 team?

E-mail was not the solution; it wasn't until Hashim left Makongo High in Dar es Salaam to take a scholarship at Laiser Hill Academy in Nairobi, Kenya, that he was noticed by someone with international basketball connections. French businessman Oliver Noah, who organized the NOGA African All-Stars AAU team, saw Hashim play and offered to take him to the U.S., and, with Rukia's blessing, handled the paperwork for an I-20 visa.

Seven-foot-three Hasheem Thabeet -- the new, Americanized name on his passport -- arrived wide-eyed in Los Angeles in January 2005 and was placed at Stoneridge Prep, where neither the housing conditions (four players were packed into coach Ron Slater's home) nor the transcript situation (they designated him as an 11th-grader, rather than a 12th-) was ideal. By April he was on the move again, to Picayune, Miss., to live with a host family and attend a public high school. Transcript issues arose once again, prompting a move in June to Houston, where Mark McClanahan, a coach Thabeet had met at the Kingwood (AAU) Classic in Houston that spring, found him another host family and a spot as a senior on the Cypress Christian School team for the '05-06 season. By the following summer Thabeet was at UConn, where he is now a junior majoring in geography. The bedroom walls of his campus apartment are decorated with SpongeBob SquarePants dolls, and his dresser doubles as a trophy stand for being last season's Big East Defensive Player of the Year and NABC Defensive Player of the Year.

In Arabic, Hashim means "destroyer of evil," and the shot blocking that earned those awards (147 swats as a sophomore, breaking Alonzo Mourning's Big East single-season blocks record) is an instinctual talent. The crash course in post offense that Thabeet received at UConn has helped him grow from a comedic liability to someone who, says Huskies graduate assistant Justin Evanovich, "is conscious of his ability to dunk everything." Huskies coach Jim Calhoun laughs at his first memory of Thabeet ("He would get a rebound in Houston, throw it and then watch nine guys run") and beams with pride when he says that "no player I've ever had at UConn has improved to the level that Hasheem has improved."

Since his father's passing, all Thabeet has done is change cities five times, countries twice and his name once. He basically learned how to play offense from scratch while establishing himself as the nation's premier defensive game-changer. Thabeet has adapted, and he has overcome.

If Uconn, which finished 24-9 last season, were to win a national championship in April, it would be the first basketball team to visit the White House under Barack Obama, whose absentee father was an economist in the Kenyan Ministry of Finance -- only nine miles from the Nairobi school where Thabeet was discovered. The gravity of this African connection is not lost on Thabeet, but it wouldn't be his first presidential encounter, either.

On Sept. 21 he arrived at the Intercontinental Hotel in New York City wearing a Euro-cut suit, and he joined Tanzania's president, Jakaya Kikwete -- who was in town for the opening of the U.N. General Assembly -- in breaking Ramadan fast. This was their third meeting, and it came with a reminder from Kikwete "to keep representing the country well." At their first meeting, in Boston when Thabeet was a freshman, he showed up in a fitted New York Yankees hat, brown sweater and jeans. ("I wasn't grown up yet," he says sheepishly.) When a photo of him appeared on Michuzi, the highest-trafficked Tanzanian blog, he was lambasted by some Swahili-speaking commenters for being disrespectful and undeserving of such attention.

Kusoma story nzima BOFYA HAPA:

Tuesday, December 02, 2008

Vilio Uwanja wa Ndege Dar

Nami nilivyokuwa Bongo 2006 na 2007 niliona mbinu huko Airport. Yaani wafanyakazi wengine hawana haya kabisa! Ni kama mradi vile kufanya kazi pale.

********************************************************************
Kutoka Michuzi Blog:

Michuzi,

Pole kwa vacation na pia kwa kukosa ndege. Nipe nafasi kidogo niongelee wizi mdogo mdogo hatimae mkubwa katika Julius Nyerere International Airport maana inakera na inauma ile mbaya Ni kwamba kuna utaratibu kwenye viwanja vya ndege kuzuia abiria kubeba vichupa vyenye vimiminika zaidi ya ml100. Kwa hiyo inalazimu abiria kulazimisha kupima mzigo hata kama una 6kg ili mradi kusalimisha mafuta na vi-manukato kwa namna moja ama nyingine.

Kitu kilichojitokeza pale ni kwamba kampuni ya kupakia na kupakua mizigo ya Swiss port imeshindwa kudhibiti wafanyakazi wake na hivyo kupoteza hadhi ya kuchukua dhamana ya mizigo ya abiria. Nilichokiona mimi ni kwamba wale jamaa wanaobeba mizigo hufungua zipu na kukagua kilichomo ndani. Wakiona kitu cha thamani wanaweka mifukoni mwao.

Na kinachoumiza ni kwamba kama kuna vitu vilikuwa kwenye mifuko midogo ndani ya begi ambavyo labda ulitaka visigusane na vingine basi utavikuta tofauti, maana wanachana vimifuko ili kutafuta wanachokitafuta wao (WIZI MTUPU), ustaarabu hakuna hata kidogo.

Sasa nataka kuuliza kuna usalama gani kama mtuu amepima mzigo ili kufuata sheria za usalama wa usafiri wa anga na hatimae wajinga wachache wapitie vitu vya thamani kwenye mizigo yake? Na je, hii itatoa picha gani kwa abiria wapendao kutumia viwanja vyetu kusafiri kwa kuchukulia kuwa ni salama kwa kwa mali na mizigo yao.
MIMI NI MDAU NA NIKO AIRPORT.

Naomba kuuongezea machache.Ni kweli kabisa,ni kweli tupu kuhusu huo wizi hapa Uwanja wa DIA...

Kweli huwa mabegi yanafunguliwa tena wana utaalamu kuliko unavyodhani wanafungua zipu bila kuiharibu,na wanatoa vile wanavyovitaka wao kama Camera,Simu ,I-pod ,Laptop... na biashara kubwa ya kuviuza inafanyika huko NJIA PANDA sehemu ya kwenye Bar na Makazi ya watu....na huwa wanajisifu sana, na isitoshe ni kweli wana maisha mazuri sana LOADER AMA PORTER WA BONGO NI SAWA NA PORTER AMA LOADER WA ULAYA nikiwa namaana ya kwamba maisha yao yako juuu na ni matawi kuliko hata Maboss wao waliopo maofisini ,maana wao hupata Pesa kila aingiapo Shift.

Kulikuwa na utaratibu wa kuwapekua wakati wakitoka kazini,lakini sasa hakuna ila hata hivyo ni wajanja sana mara nyingine wanauza humu humu jengoni.na tunapata sana malalamiko mengi kutoka kwa wageni wetu watakao na kuingia nchini.Binafsi inaniuma sana maana ni juzi tu nilitumiwa na ndugu yangu mzigo wa Camera na wakailamba.
Na Juzi kuna wawili walijaribu kuiba mzigo wa mama mmoja Mmalawi waliushusha kwenye Air Malawi wakadai kuwa unaenda na Precision Air lakini Askari aliwashuku na kuwakamata sasa sijui kesi imeendaje.... WIZI WIZI WIZI KILA KONA......

Nini kwenye mabegi ya abiria, na wizi wa mafuta ya ndege je??? tena hiii ni issue sana kubwa maana hadi baadhi ya watu ambao hawastahili kuwepo wanashiriki kwenye hiii....jaribuni kufuatilia.

USHAURI WANGU kwa TAA na SWISSPORT wangetengeneza bango kubwa kuwasaidia wageni wanaondoka Departure liwekwe Getini pale nje kabla ya security liandikwe kwa kiingereza na kiswahili hata french kuwa ABIRIA ASIWEKE CAMERA, SIMU, LAPTOP AMA HELA MAANA NASIKIA KUNA WATU HUWA WANAWEKA HELA KWENYE MABEGI...PLEASEACHENI AIRPORT IMEKUWA MBAYA..

NA ABIRIA WA KUTOKA NJE WATAJUA HILI SUALA TARATIBU TUWASAIDIE HAWA WAONDOKAO....

Monday, December 01, 2008

Philips


Wadau mnakumbuka hii tangazo?

" Philips ndio enyewe....Sauti safi sauti kubwa!"

Enzi hizo wewe mtu kama una redio kama hii, short wave, universal etc.! LOL!

SIKU YA UKIMWI DUNIANI




Leo ni siku ya UKIMWI duniani (World AIDS Day). Tukumbuke waliopoteza maisha yao na waliothairika na ugonjwa huo. Pia tumwombe Mungu kuwa tiba utapatikana siku za karibuni.