Saturday, April 07, 2012

TAARIFA YA RAIS KIKWETE KUZINDUA TUME YA KATIBA IJUMAA APRIL 13, 2012


UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete atazindua rasmi Tume ya Kukusanya na Kuratibu Maoni ya Mabadiliko ya Katiba na kuapisha wajumbe wa Tume hiyo Ijumaa ijayo, Aprili 13, mwaka huu, 2012.
Tume hiyo itazinduliwa na wajumbe wake kuapishwa kulingana na matakwa ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 iliyounda Tume hiyo. Aidha, Tume hiyo itazinduliwa rasmi wiki moja baada ya kuwa imetangazwa rasmi. Rais Kikwete alitangaza Tume hiyo jana, Ijumaa, Aprili 6, 2012, kwenye mkutano wa wahariri uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Tume hiyo itakayoongozwa na Mwenyekiti Jaji Joseph Sinde Warioba akisaidiwa na Makamu Mwenyekiti Jaji Mkuu Mstaafu, Jaji Augustino Ramadhan ina wajumbe 30, ikiwa ni wajumbe 15 kutoka kila moja ya pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wajumbe wa Tume hiyo kutoka Tanzania Bara ni Profesa Mwesiga L Baregu, Ndugu Riziki Shahari Mngwali, Dkt. Edmund Adrian Sengodo Mvungi, Ndugu Richard Shadrack Lyimo, Ndugu John J Nkolo, Alhaji Saidi El Maamry na Ndugu Jesca Sydney Mkuchu.
Wajumbe wengine wa Tume hiyo kutoka Bara ni Profesa Palamagamba Kabudi, Ndugu Humphrey Polepole, Ndugu Yahya Msulwa, Ndugu Esther Mkwizu, Ndugu Maria Malingumu Kashonda, Mheshimiwa Al-Shaymaa J Kwegyir, Ndugu Mwantumu Jasmine Malale na Ndugu Joseph Butiku.
Wajumbe wa Tume hiyo kutoka Tanzania Visiwani ni Dkt. Salim Ahmed Salim, Ndugu Fatma Saidi Ali, Ndugu Omar Sheha Mussa, Ndugu Raya Suleiman Hamad, Ndugu Awadh Ali Saidi, Ndugu Ussi Khamis Haji na Ndugu Salma Maoulidi.
Wengine kutoka Visiwani ni Ndugu Nassor Khamis Mohammed, Ndugu Simai Mohammed Said, Ndugu Muhammed Yussuf Mshamba, Ndugu Kibibi Mwinyi Hassan, Ndugu Suleiman Omar Ali, Ndugu Salama Kombo Ahmed, Ndugu Abubakar Mohammed Ali na Ndugu Ally Abdullah Ally Saleh.
Shughuli za Tume hiyo zitaratibiwa na Sekretarieti ambayo Katibu wake atakuwa Ndugu Assaa Ahmad Rashid na Naibu Katibu atakuwa Ndugu Casmir Sumba Kyuki.
Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
07 Aprili, 2012

No comments: