Monday, April 09, 2012

Mama Bishanga na Ohio Wamlilia Kanumba

MAMA BISHANGA NA OHIO WAMLILIA KANUMBA

Nimeguswa na kuumizwa sana na msiba  wa ghafla wa msanii wenzangu wa tasnia ya filamu,  Steve Kanumba, ndugu yetu, kijana wetu, rafiki yetu na mtanzania mwenzetu alietuachia pengo lisilozibika. Itatuchukua muda mrefu sana kusahau msiba huu wa taifa zima kutoka na umahiri wake, juhudi zake na kazi nzuri alizozifanya kwa kipindi kifupi cha uhai wake. 

Nachukua nafasi hii pia kuwapa pole wazazi wake, mimi kama mzazi niko nanyi katika kipindi hiki kigumu sana, nimekuwa nawakumbuka sana katika sala tangu jana nilipopata habari hizi. Poleni sana.

STEVE TULIKUPENDA, TUNAKUPENDA NA TUTAENDELEA KUKUPENDA, MUNGU AKUPOEE KWA AMANI NA MWANGA WA MILELE AKUANGAZIE KATIKA JINA LA YESU KRISTO BWANA NA MWOKOZI WETU, AMEN

MRS CHRISTINA INNOECENT MAROLEN
MAMA BISHANGA
OHIO/ USA

No comments: