Tuesday, April 10, 2012

Jenerali Ernest Mwita Kyaro Afariki Dunia


Picha kwa hisani ya Michuzi Blog

Rais Kikwete akimpa pole General Mwita hivi majuzi  huko Bugando Hospital (picha kwa hisani ya Maggid Mjengwa blog)

Nimepokea kwa masikitiko habari ya kifo cha Jenerali (General) Ernest Mwita Kyaro.  Kwa vijana wasiojua, Jenerali Kyaro alikuwa moja wa makamanda walioogoza vita dhidi ya Idi Amin mwaka 1979.   Enzi zile tulikuwa na viongozi wa jeshi wakali sana na akina Black Mamba!   Jenerali Kyaro alikuwa Mkuu wa Majeshi mwaka 1988-1994. Wanajeshi wetu walifukuza jeshi la Amin kwa staili ya aina yake. Walienda hadi Kampala! Idi Amin mbio...He was no more bigi kingi! ( Usemi wa Idi Amini ilikuwa, "They think me bigi kingi")

Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni.  Amen.

5 comments:

Anonymous said...

RIP Mkuu Mwita Kiaro Nakumbuka miaka ile ulivyompiga biti Raisi mwinyi wakati huo......kisa ilikuwa watoto wa mzee mwinyi kuwavimbishia vifua watoto wa Mkuu wa majeshi........ ! Jamani huu ni msiba mkubwa sana, huyu ni mpiganaji alieshiriki ukombozi wa nchi yetu dhidi ya uvamizi wa Ndili Idd na ukombozi mwingine ambao TZ ilishiriki wakati huo.

Anonymous said...

Hebu wabongo fungukeni macho uvamizi upi wa Amini,ule ulikuwa uongo wa Julius Nyerere kutaka sapoti ya kutumia majeshi ili kumrudisha rafiki yake Obote madarakani.Ambae aalirudi na kuchinja Waganda wengi kushinda hata Amini,hadi Museveni alipo amua kumpindua.Ukariri maneno ya Museveni kufuatia kifo cha Julius mahojiano na BBC.

Anonymous said...

“Jenerali Kyaro alistaafu akiwa amelitumikia jeshi kwa miaka 50, miezi 11 na siku 13,” alisema Mgawe na kufafanua kuwa jenerali huyo alizaliwa mwaka 1925, Kijiji cha Nyamwaga, Tarafa Igwe Tarime, mkoani Mara.

Wasifu wa marehemu
Akieleza wasifu wa marehemu kwa kifupi tangu alipoingia kazini, Mgawe alisema kuwa alijiunga na jeshi Aprili 19 mwaka 1943.

Alisema kuwa Jenerali Kyaro aliendelea kulitumikia jeshi hadi alipostaafu Machi 31 mwaka 1994 na kwamba katika utumishi wake aliwahi kutunukiwa nishani mbalimbali ikiwa ni pamoja na ya miaka 20 ya JWT, Utumishi Uliotukuka Tanzania na Utumishi wa Muda Mrefu Tanzania.
Alizitaja nyingine kuwa ni Medali ya Vita, Medali ya Kagera, Medali ya Uhuru na Medali ya Muungano.
Jenerali Kyaro ameacha sifa ya uaminifu ambayo haijavunjwa jeshini baada ya CDF pekee aliyewahi kurejesha masurufu aliyolipwa kwenda kutibiwa nje ya nchi, kutokana na kudai kuwa akila na kutibiwa bure bila kutumia fedha hizo.

Anonymous said...

Niliwahi kuambiwa jinsi Kyaro alivyokataa kununuliwa vitu vipya kwenye nyumba ya jeshi aliyoingia baada ya kuwa Mkuu wa Majeshi. Nilijisikia fahari kuwa na Mtanzania wa namna hii ambaye haoni thamani ya vitu bali utu wake na uzalendo wa taifa lake.

Hii habari hapa chini inaeleza pia alivyowahi kurejesha masurufu aliyopewa wakati akienda kutibiwa nje ya nchi. Nani anaweza kufanya hivyol leo?

Anonymous said...

Jenerali Ernest Mwita Kyaro alikuwa ni CDF nilipojiunga na JKT kwa mujibu wa sheria Julai 1988. Tulikuwa tukimtaja sana katika nyimbo zetu za route march wakati huo tukiwa makuruta ndani ya kaptula na T-shirt za kijani.