Sunday, April 08, 2012

Mazishi ya Marehemu Steven Kanumba Yatakuwa Jumanne

 KUTOKA HARTMANN ONLINE TZ BLOG:

MAREHEMU STEVEN CHARLES KANUMBA KUZIKWA JUMANNE 10 APRIL 2012…!!!

 Habari zilizotufika hivi punde kuhusiana na mazishi ya aliye kuwa muigizaji nguli wa Filamu Tanzania marehemu Steven Kanumba ‘The Great’ ni kwamba Jumanne tarehe 10 April 2012 kuanzia saa 4 (nne) asubuhi mpaka saa 9 (tisa) mchana mwili wa marehemu Steven Kanumba utakuwa viwanja vya Leaders (Leaders Club) kwa ajili ya kuagwa na baada ya hapo mwili wa marehemu utaelekea katika makaburi ya Kinondoni ambapo ndo safari yake ya mwisho itakapo ishia. Mazishi yatafanyika saa 10 jioni (kumi) makaburi ya Kindondoni.

7 comments:

Anonymous said...

Inahuzunisha na inatia uchungu kupita kiasi jamani, Kanumba kaka yetu daima tutakukumbuka.

Pili nawashauri wasanii muwe karibu na Mungu zaidi kuliko mambo ya kidunia, leo ni Kanumba kesho atafuata nani? Je tumejifunza nini kutokana na kifo cha The Great?

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU STEVEN KANUMBA MAHALI PEMA PEPONI AMINA.

Anonymous said...

Kikubwa ni kumuombea JEMBE WA TAIFA LETU LA TANZANIA Marehemu STEVE’KANUMBA May his soul R.I.P!. 2hamini kuwa mungu alitwaa na yeye ndo amechukua’ AMEN!!!

Anonymous said...

Kuna Prof.wa UDSM Faculty oF Geology pia amekufa leo but hakuna hata chombo kimoja cha habari hapo Bongo kilichoripoti.Swali ni Je,huyu msela Kanumba na huyo Prof.nani muhimu?Wabongo wenzangu kwa mtaji huu hatutoki hata miaka elfu1.Yani hizi ndio zile zama zilizotabiriwa kwamba ujinga ndio utakua werevu na werevu kua ujinga.Binafsi sioni haja ya watu km hawa kupewa thamni kubwa katika jamii zaidi ya watu wanaotoa elimu za manufaa na zakuendeleza nchi.Yes kwakua ni mtu naskitikia kifo chake.

Anonymous said...

R.I.P The Greåt Steven Kånumbå…
Its so Suddenly … Realy we whr stil need ur contributiön on the film industry…
We will Miss ¥ou…
Allåh Bless ¥our wåy…

JFK said...

KANUMBA ALIKUWA BONGE LA MWIGIZAJI KWAKWELI ANAPASWA KUENZIWA, MASHABIKI WOTE WA BONGO MOVIE TULIMKUBALI KWA KAZI YAKE NDIYO MAANA KAACHA PENGO LISILOZIBIKA. LKN YALIYOPITA SI NDWELE, TIMUOMBEE KWA MWENYEZI MUNGU AMPOKEE ALALE SALAMA.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE AMENI.

Anonymous said...

kifo cha kanumba nakifananisha na kifo cha dandu na kifo cha amina chifupa

ni vijana wadogo tuliowategemea sana kutuletea mengi kwa faida ya nchi yetu

mungu amewachukua wakiwa ndio kwanza taa imewaka kuashiria mwanzo wa sherehe

daima tutawakumbuka mchango na jitihada zao katika kuleta maendeleo ya nchi ya tanzania

kazi ya mungu haina makosa na tukumbuke ule usemi usemao KIZURI HAKIDUMU.

m,mungu ilaze roho ya marehemu pema peponi ameen.

Anonymous said...

WAANDISHI WA HABARI WAJARIBU KUANGALIA NA UPANDE WA PILI KWA HUYU PROF.OF GEOLOGY WA UDSM KUTANGAZA MSIBA WAKE KWANI WOTE NI MUHIMU KATIKA JAMII