Saturday, April 07, 2012

Kifo cha Kanumba - Eti ilikuwa Ugomvi wa Kimapenzi!

Duh! Yaani nashangaa mambo nayosoma kwenye mtandao.  Inaelekea iliktokea ugomvi wa kimapenzi kati ya Kanumba na mpenzi wake Lulu.  Kanumba alianguka na kugonga kichwa chake! Alikufa kwenye saa 8 na nusu usiku wa kuamkia leo (jumamosi April 7) WIVU KITU KIBAYA SANA JAMANI!

******************************************************

HII IMEANDIKWA NA MILLARD AYO
Taarifa nilizozipata sasa hivi kutoka kwa mwigizaji Dino, ni kwamba kweli mwigizaji STEVEN KANUMBA amefariki dunia na inaaminika chanzo cha kifo chake ni baada ya kuanguka na kuanza kutoa mapovu hapohapo nyumbani kwake, alikua akiishi na mdogo wake anaitwa Fetty aliekua chumba kingine ambae amethibitisha kweli kwamba alimkuta kaka yake akiwa ameanguka.
Polisi wameondoka nyumbani kwa Kanumba muda mfupi uliopita baada ya kuwachukua waliokua wanaishi na Kanumba akiwemo mdogo wake Fetty ili kwenda kusaidia maelezo ya kilichotokea.
Bado watu wanazidi kuongezeka nyumbani kwa Kanumba ambapo tayari idadi kubwa ya wasanii wenzake wamefuka pamoja na watu mbalimbali, millardayo.com itaendelea kukufahamisha kinachoendelea kadri taarifa zitakavyozidi kupatikana.
Ila kumekua na taarifa nyingine ambazo hazijathibitishwa kwamba Kanumba alianguka na kuumia kichwani baada ya mpenzi wake ambae anatajwa kuwa ni mwigizaji LULU kumsukuma na kuanguka wakati wanagombana.
‘Inasemekana’ Kanumba wakati akijiandaa kutoka saa sita usiku aliingia bafuni kuoga, alipotoka alimkuta Lulu akiongea na mwanaume mwingine kwenye simu ndipo alipokasirika na ugomvi kuanza.
Alipelekwa hospitali Muhimbili ambako muda mfupi baadae alifariki dunia, mwili wake bado uko katika chumba cha kuhifadhia maiti Muhimbili hospital.
Hapo chini ni baadhi ya kauli nilizokutana nazo kwenye facebook wakati huu na chini yake ni maneno ya mwisho STEVEN KANUMBA kuyaandika kwenye kurasa zake za facebook na twitter.


BOFYA HAPA KWA HABARI ZAIDI!

2 comments:

Anonymous said...

rip steven kanumba wengi tulimpenda lakin mungu kampenda zidi lakin pengo lange alitafutika kamwe mungu ailaze roho ya marehemu mahara pema peponi ameni atuna jinsi ishakuwa

Anonymous said...

Laiti tungekuwa tunajua siku au saa tungekuwa tunajiandaa na hali ya umauti, lakini hakuna hata binadamu mmoja nayejua siku yake ya kuiaga dunia, Mungu atakupumzisha mahali pema, tutaendelea kukuezi kwa kuangalia kazi zako amabzo naamini zinakuweka katika hali ya kutosahaulika hapa diniani daima.

Ualale mahali pema peponi
AMINA