Tuesday, February 12, 2008

Flaviana Matata


Picha Asante Michuzi Blog

Miss Universe Tanzania, 2007, Flaviana Matata (20), alienda Budapest, Hungary hivi karibuni kwenye sherehe ya Budapest Opera Ball. Ni sherehe inayofanyika kila mwaka na ni tafrija yenye hadhi kubwa nchini Hungary. Wanasiasa, wakuu wa nchi, mabalozi na watu mashuhuri kutoka nchi hiyo na jirani barani Ulaya huhudhuria. Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mrembo kutoka Afrika kuhudhuria hafla hiyo.

Sasa kuhusu ombi la Michuzi kwa msaada kwa Flaviana kuendelea na Modelling. Namshauri apeleke habari zake, Trump Model Management. Sasa hivi wanae MSudani Artong Arjok.

Hiyo kazi ya modelling ni know-who na namshauri pia afanye networking kali akiwa safarini. Hao warembo wenzake wanaweza kumsaidia pia.

Namshauri pia ajifunze lugha mbalimbali pia kama Kifaransa, Kispanish, Kijereumani. Sijui ana kipaji gani cha Kiingereza, maana kwenye Miss Universe waliweka Sub-titles alivyokuwa anaongea.
***********************************************************************************
OMBI LA KAKA MICHUZI
Mrembo wetu hivi majuzi alialikwa hungary kuhudhuria hafla maalumu ambapo warembo wa dunia nzima walialikwa kushiriki. hizi ni baadhi ya picha za safari hiyo inayoonesha kwamba bado flaviana anatambulika kama mmoja wa warembo bomba duniani baada ya kushika nafasi za juu miss universe mwaka jana. tatizo hadi leo anasota waya bongo wakati wenzie wote wamepata nafasi za kufanya kazi na kampuni kubwa za mitindo. mdau mwenye uwezo ajitokeze amsaidie kuendeleza kipaji chake. unaweza kuwasiliana nami kupitia issamichuzi@gmail.com nitafikisha ujumbe. hima wadau na tumsaidie mrembo wetu huyu aliyelera sifa kwa nchi hii. asije akaishia hapo alipo kwani umri wake bado wa miaka 20 unadai kabisa kufanya maajabu zaidi kwenye ulimbwende.

1 comment:

EDWIN NDAKI (EDO) said...

hongera sana Flavian kwa mafanikio uliyo fikia.

Hakina kama Da Chem alivyokushauri ujitajihi kutafuta information kwenye vyanzo mbalimblia nami naungana mkono na ilo.

Pia nimeona hii hili tangazo natumaini litakufaa..

We Want You...
Outlaws Model Agency is looking for new faces for its local and international portfolios...(MWISHO WA KUNUKUU)

Webpage yao ni ..http://www.outlawsmodels.co.za

...Ila nakupa tahadhari uwe makini maana kuna watu wanaitw "baby hunters" usije ukadondokea kwenye mikono isiyo salama.Jitahidi makubaliano unayoingia nayo yawe "clear" sio ubabaishaji.

Watu wamemaliza Rich -monduli(Richmond) sasa wanataka kufisadi hadi miili ya watu.

Ene wei tutafik atu