Thursday, February 07, 2008

Baraza la Mawaziri Lavunjwa!!!!


Rais Jakaya Kikwete, kaonyesha waTanzania kuwa hana mchezo. Amevunja Baraza la Mawaziri!

Pia amekubali ombi la kujiuzulu uwaziri mkuu, Mheshimiwa Edward Lowassa.

Kuona Baraza la Mawaziri lilliyovunjwa bofya HAPA:

Cheche zimetembea Bungeni tangu ripoti ya Mheshimiwa Dr. Harrison Mwakyembe kusomwa Bungeni jana. Ripoti ilihusu sakata la umeme na kampuni tapeli la Richmond.

Kusoma Ripoti hiyo bofya HAPA:

Mwalimu Nyerere aliwahi kuvunja Baraza lake la Mawaziri.

5 comments:

Anonymous said...

Ahsante kwa habari hizo.Mh.Lowassa na wote waliohusika sio kwamba wanapaswa wajiuzulu bali wanapaswa kukamatwa moja kwa moja kutoka jumba la bunge nakufikishwa katika vyombo vya sheria.Accounts zao kuzuiwa pia mali zao wakati sheria inachukua mkondo.Hii itafanya kwa kila kiongozi yeyote kua makini anapokua madarakani,kwani ikiishia kujiuzulu tu kutampa nafasi kiongozi yeyote kujichotea mapesa na baadaye kujiuzulu na kuendelea kutumbua pesa zake alizozipata kwa ufisadi.KUJIUZULU HAKUTOSHI,MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Anonymous said...

http://tinyurl.com/26nc2u

'Nuff said.

Anonymous said...

Da Chemi hii imekufikia?

Hotuba ya Rais JKM, February 7, 2008 - Dreams of a fool


----- Forwarded Message ----
To: list@tanzanet. org
Sent: Thursday, February 7, 2008 9:02:31 AM
Subject: [tanzanet] Hotuba ya Rais JKM, February 7, 2008 - Dreams of a fool

Ndugu Spika, ndugu wabunge, ndugu wananchi.

Leo asubuhi nimepokea barua ya Waziri Mkuu ya kujiuzulu kwa masikitiko makubwa kwani tumefanya naye kazi muda mrefu na nilitegemea atumie vipaji vyake vingi kuongoza serikali yangu kwa muda mrefu. Wengi mtakumbuka enzi za Boyz2Men. Nasikitika sana kwa hatua taifa letu lilipofikia.

Aidha, nimepokea na kusoma ripoti ya Dr Mwakyembe kwa masikitiko maradufu ya yale yaliyonipata kwa barua ya ndugu Lowassa. Sina mengi ya kusema, ila jioni hii naomba wananchi mnipe ridhaa yenu kuanza mchakato wa kina wa kuondoa taifa hili kwenye dimbwi la ufisadi, ubadhirifu, wizi, utawala wa ki-imla, na kutojali matakwa na malalamiko ya wananchi.

Awali ya yote nikiri kwamba kwa miaka yote niliyokuwa kwenye shughuli na uongozi wa uma, lazma kuna nyakati chache ambazo nami niliwahi kuterereka kimaadili. Pale matendo yangu hayakukidhi mategemeo ya wananchi naomba msamaha wao. Hata hivyo inafika wakati nchi kusafishwa kwa manufaa ya umma. Bila hivyo nchi yetu itasambaratika kama majirani zetu na nchi nyingine kama USSR , Yugoslavia nk. Nimenuia kuiokoa nchi yetu toka kwenye hatma hii, na kwa hili nitaomba na kuhitaji msaada wenu. Hatua za awali.

Kwanza, nakataa kujiuzulu kwa Waziri Mkuu kama hakuandamani na kujiuzulu kwa baraza lote la Mawaziri ili nianze upya kuomba kibali cha kuwaongoza wananchi bila fununu za ufisadi na bila dharau kwa serikali yao .

Pili, natangaza kugandisha (to freeze) akaunti zote za mali za wale waliohusika na shutuma za Richmond , na BoT, pamoja na kushika rehani mali zao zote zisizohamishika kwa nia ya kurudishia serikali mali yoote ambayo inaweza kuwa iliibiwa na washutumiwa. Ili wasife njaa serikali itaendelea kuwalipa nusu mshahara hadi uchunguzi au mashtaka kumalizika.

Tatu, nawahimiza viongozi wote waliojihusisha na ufisadi wowote wa kimsingi kama kwenye mikataba ya madini, Netgroup Solutions, Uuzaji wa Mashirika na Raslimali za Umma, Ununuzi wa rada na ndege ya Rais, Ununuzi wa vifaa vya Jeshi, Mikataba na TANESCO kama IPTL, Kiwira, nk, wakiri kwangu kimaandishi kushiriki kwao na kuorodhesha mali walizopata kutokana na matendo hayo. Wakifanya hivyo sitawachukulia hatua za kisheria ila nitawasimamisha kazi ya umma na kurudisha mali ya wananchi panapohusika.

Wasiojitokeza kwa hiari naagiza vyombo vyote vya uchunguzi vya dola kufuatilia kwa undani na waletwe mbele ya sheria mara moja.

Ndugu wananchi, hii vita dhidi ya wabadhirifu itahitaji ushirikiano wenu na naomba mniunge mkono kwa kila namna.

Nimeagiza vyombo husika kuhakikisha watuhumiwa hawawezi kutoroka au kutorosha mali hadi uchunguzi umalizike. Aidha nimeagiza vyombo vya dola viwe macho kudhibiti wakorofi wachache watakojaribu kuleta ghasia.

Mungu ibariki Tanzania .

Asanteni.

(Anavua miwani, anafuatwa kwenye jukwaa na Makamu wa Rais, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Katibu Mkuu wa CCM, Chadema, CUF, UDP na kuzingirwa na Chief Justice, Mkuu wa Majeshi, Mkuu wa Usalama wa Taifa, Mkuu wa Polisi na Mkuu wa Magereza. Wanatoka nje ya Bunge kwa hatua kakamavu za kijeshi. Wabunge wanasimama na kumshangilia kwa nderemo na vifujo)!!!!! !


mchilyi3.0
ps! Saa ya ukombozi ingeanza vivyo!

Anonymous said...

Afadhali Tanzania inaelekea kwenye uwazi na ukweli, Ameonyesha ujasiri kwa kujiuzuru na natumaini Waziri wa fedha na katibu mkuu wake wajiuzuru kutokana sakata la BOT. Naunga mkono comments above that these people needs to be in court and finale JAIL, MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Anonymous said...

LOWASSA NA WENZAKE WAPELEKWE KORTINI KUJIBU HIZO TUHUMA PAMOJA NA WAZIRI WA FEDHA NA WENZAKE KUHUSU AIBU YA BOT,MUNGU IBARIKI TANZANIA.