Friday, February 29, 2008

Maiti ya SuperModel kutoka Guinea yakutwa mtoni Ufaransa



Habari kutoka Ufaransa zinasema kuwa maiti ya supermodel, Katoucha Niane, (47) umepatikana katika mto Seine. Mrembo Katoucha alikuwa hajaonekana tangua mweza January na jitihada zilifanywa za hali ya juu kumtafuta.

Katoucha ni kati ya wanawake wa kwanza kutoka Afrika kutamba katika dunia ya u-model. Alizaliwa Guinea.
Katoucha aliwahi kutamba na madesigner wakubwa kama Yves Sain Laurent, Christian Lacroix, Paco Rabanne na Thierry Mugler.
Katoucha alikuwa pia ni mpigania haki za wanawake. Alilaani vikali kitendo cha kuketa wasichana huko kwao. Yeye mwenyewe alikeketwa akiwa na miaka 9. Alikimbia kwao akiwa na miaka 17 na alienda Ufaransa. Alisema kuwa hawezi kusahau maumivu makali ambayo alisikia kutokana kutokana na kitendo hicho.

Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.
Kwa habari zaidi someni:

1 comment:

Anonymous said...

Oh how sad! Natoucha wa so beautiful! In the 80's she was in her prime. She blew the lid off African stereotypes. May she rest in peace.