Monday, February 11, 2008

Mh. Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda

Mh. Rais Jakaya Kikwete na Mh. Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda
Mh. Rais Kikwete akisalimiana na baba mzazi wa Mh. Pinda, Mzee Xavery Kayanza Pinda, na mama mzazi, Bi Albetina Kasanga.Mke wa Waziri Mkuu, Mh. Pinda, (kushoto) Tunu Rehani Pinda akiongea na mbunge wa Viti Maalum Martha Mlata mara baada ya sherehe za kumwapisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda zilizofanyika ikulu ndogo ya Chamwino Dodoma.

(picha asante Michuzi blog)

Sijui ni furaha gani wazazi wa Mh. Pinda walionayo kumwaona mwanao anakuwa Waziri Mkuu. Mungu awabariki.

Na nasema hivi, jumatatu ya wiki iliyopita, Mh. Pinda alijua atakuwa Waziri Mkuu? Kweli huwezi kujua mipango ya Mungu.

Na wameumbua skandali ya Richmond, je wataumbua skandali ya machimbo ya madini?

3 comments:

Anonymous said...

Da Chemi, hiyo picha ni bora kuliko ile ya mwanzo ulibandika ya Mh. Pinda. Sura bado mbaya lakini.
Huyo mke wake ajifunze kuvaa sasa.

Anonymous said...

Wabarikiwe wote. AMIN.

Anonymous said...

Raisi anatoka Bagamoyo,Makamu wa raisi Pemba,Waziri mkuu Sumbawanga patamu hapo,hapalogeki!