Monday, February 11, 2008

Vituko Vya Michael Jackson

Michael Jackson kabla hajajiharibu kwa plastic surgery na vidonge vya kubadilisha rangi ya ngozi na dawa za kuogea za kubadilisha rangi.
Michael Jackson na mkwe wake wa wahakti huo, Debbie Rowe. Rowe alikuwa ni nesi wake na alimzalia watototo watatu. (Hao watoto ni wa Jackson kweli?)
Michael Jackson na watoto wake Prince na Paris wakiwa wamejifunika ushungi.
Watoto wa Jackson, Paris and Prince Michael walivyo leo.

Mke wa zamani wa mwimbaji maarufu Michael Jackson ambaye pia ni mama watoto wake, Debbie Rowe (49) amekasirika mno! Kisa, watoto aliyozaa na Jackson, wamepigwa picha bila kufunikwa ushungi.

Anasema kuwa walivyokuwa wadogo watu walitiisha kuwateka hao watoto. Sasa wanajua walivyo itakuwa rahisi wao kutekewa.

Baada ya kuwaona watu wanauliza kama hao kweli ni watoto wa Michael Jackson. Au ni kweli huyo Debbie Rowe alifanyiwa Artificial Insemination (kuchomwa sindano zenye shahawa/mbegu) ukeni. Si siri kuwa Jackson hakupenda weusi wake, pua kubwa, nywele za kipilipili, rangi yake. Ndo maana kajiegeuza kuwa kinyago.

Si ajabu Jackson alimchagua baba watoto wake na alinunua hiyo shahawa! Watu waliozoea kuona watu mixed wanajua kuwa lazima hao watoto watakuwa na rangi kiasi na curly hair. Hao nywele zao zimenyoka kizungu! Hebu cheki mifano ya watu mixed, kama Halle Berry, Shemar Moore, Barack Obama, na Derek Jeter. Wataalamu wa DNA wanasemaje hapo?

Kwa habari zaidi someni:

http://www.foxnews.com/story/0,2933,330232,00.html

http://breakingnews.iol.ie/entertainment/story.asp?j=245984520&p=z45985zz6

9 comments:

Anonymous said...

Siwezi kukukabali hata kidogo kuwa hao ni watoto wa Michael Jackson. Weupe mno. Kubadilisha rangi haibadilishi DNA.

Anonymous said...

Watoto wako normal. Lakini wanaonekana wazungu sana. Hapana DNA ya Michael Jackson hapa.

Anonymous said...

Jamani huyo mtoto wa kiume ni baba yake mtupu angalai hayo masiokio Po kama michael kabisa alipokuwa mdogo hata huyo wakike wamefanana naye macho. na huyo wakike na shngazi zake mugnu hakunyimi vyote akinyime akili na shahawa pia hapana jamani

Anonymous said...

Kama watu wana wasiwasi baba yao ni nani basi wapimwe DNA.

Anonymous said...

It will be interesting to hear what these kids have to say about their childhood when they grow up.

Anonymous said...

Waende kwa Maury Povich.

Anonymous said...

Niliwahi kusikia kwamba mwanzoni Michael na wazazi wake walikuwa waumini wazuri sana wa dini fulani.

Tafadhali naomba nijue ukweli kuhusu hilo, na je wazazi wake bado ni waumini wazuri?

Anonymous

Anonymous said...

Niliwahi kusikia kwamba Michael na wazazi wake walikuwa ni waumini wazuri sana wa dini fulani. Ningependa kujua ukweli wa jambo hilo. Je wazazi wake bado ni waumini wazuri kama hapo awali?

Anonymous said...

Chemi artificial insermination sio kuchomwa sindano ya shahawa bali ni kuwekewa shahawa ukeni kwa njia ya mpira(tube).