Wednesday, February 13, 2008

Ukatili wa Polisi Florida!

Deputy Charlette Marshall-Jones (mugshot)








Huko Tampa Florida, polisi wa kike, deputy Charlette Marshall-Jones, 44, alimwaga chini mwanaume aisyejiweza na anayetumia wheelchair.

Huyo Marshall-Jones alimwambia Brian Sterner (32), asimame ingawa alimwona yuko kwenye wheelchair. Sterner alimwambia kuwa hawawezi kusimama ndipo huyo katili Charelette Marshall-Jones, alimwaga chini! Alitenda maovu yaka January 28, 2008 lakini jana ndo waandishi wa habari walizipata na kusambaza habari. Wakuu wa polisi eti hawakuwa na jabari mpaka walipoambiwa na waandishi wa habari!

Sterner ni Quadraplegic. Alipata ajali miaka 14 iliyopita akiwa anacheza wrestling na kuumia shingo. Hawezi kutumia viungo vyake chini ya kifua ndo maana anatumia wheelchair. Hatua ya kishenzi ya huyo mama zingeweza kumwua mgonjwa kama huyo. WaBongo waliopitia home health aide wanajua jinsi ya kuwageuza na kushugilia wagonjwa kama huyo. Ajabu ukiona hiyo video polisi wengine wanacheka!

Kisa cha Sterner kupelekwa Polisi - alikuwa anatuma gari maalum kwa ajili ya maquaraplegic, ilmgomea barabarani. Alikuwa anashitakiwa kwa kuzuia magari kupita.

Kwa sasa watu wanaoiona hiyo video wamechukia mno! Wanataka hatua kali zichukuliwe dhidi ya huyo polisi mshenzi, msimamizi wake na polisi wengine waliokuwepo huyo mama alivyofanya ushenzi wake! Habari zinasema polisi wanne wamesimamishwa kazi kuhusiana na tukio huo. Huyo mama anastahili afukuzwe kazi na afunguliwe mashitaka!

Yaani nchi hii inaoza mpaka watu wanakosa huruma!

Kuna Video ya tukio bofya hapa:

Kwa habari kamili ya tukio soma:





2 comments:

Anonymous said...

Jamani! Hii kali. Kweli ni ukatili! tuone kama huyo polisi atashugulikiwa.

Anonymous said...

Huyo Charlette si binadamu. Nimesoma story eti alikuwa anacheka baada ya hapo. Mkatili huyo. Navyofahamu USA wabaguzi wako tayari kumnyonga.