Tuesday, February 19, 2008

Jambo Forums - Vipi Tena?????



Walioshikiliwa waachiwa

Written by Mwanakijiji
Tuesday, 19 February 2008

Jeshi la Polisi Mkoani Dar-es-Salaam limewaachilia vijana Mike Mushi na Mac DeMello ambao ilikuwa inawashikilia kwa zaidi ya masaa 24 yaliyopita. Vijana hao walikuwa wanashikiliwa kwa madai ambayo hadi hivi sasa hayajaeleweka lakini inadaiwa kuhusiana na mtandao maarufu wa Jambo Forums. Muda mfupi uliopita email kutoka kwa mtu anayejiita Melo imetuma ujumbe kwa klhnews ikisema kuwa

" Kaka unayafanya maisha yangu kuwa hatarini SANA. Sina simu ningekupigia. Tafadhali SANA futa haraka habari hiyo inayotuhusu kwakuwa itaharibu kila kitu na kunifanya nitoweke kwenye uso wa dunia. Mapambano niliyaona yenye haja lakini sasa hali NI MBAYA SANA. Wasiliana na mwenzio....... akwambie nini kimempata. NAKUOMBA SANA leave us for this moment, unawarahishia upelelezi wenzio!
Bora kuendeleza mijadala mingine kuliko hivi, kaka balaa kwangu!"

Hata hivyo haieleweki ni kwanini kama kweli email hii ni ya vijana hao wanakuwa na wasiwasi hata wa "kutoweka duniani" wakiwa chini ya vyombo vya usalama. Msimamo wa KLH News ni kuwa jambo lolote likiwatokea vijana hao hata kujikwaa au kuvunjika ukucha wakiwa mikononi mwa Polisi watakaowajibika mbele za wananchi ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Tanzania na Inspekta Jenerali wa Polisi kwa kushindwa kulinda usalama na uhaki wa vijana hao.

Tunaendelea kutoa wito kwa vyombo husika kwenda kutafuta majambazi na wezi wa fedha zetu za umma kama kina Balali ambao wanatanua ughaibuni badala ya kuwatafuta na kuwabambikizia kesi zisizo na msingi vijana ambao wanatumia vipaji vyao kuinua uhuru wa habari nchini.

Taarifa za vijana hawa kuwekwa kizuizini zinaanza kuendelewa kuandikiwa ripoti ya kuonesha ni jinsi gani Taifa lililosifiwa kuwa ni "mfano" katika Bara la Afrika limeshindwa kujizuia kuvumilia maoni huru siku chache baada ya kumpokea kwa shangwe Rais wa Marekani Bw. George Bush nchi ambayo hakuna kitu kinaenziwa sana kama uhuru wa maoni na mawazo.
*****************************************************************

Naona mambo mazito!!!

Kusoma na maoni ya watu Bofya hapa:

6 comments:

Anonymous said...

Mkono wa Mzee Pinda unatembea!

Anonymous said...

Hao lazima wameminywa!

Anonymous said...

Waziri Mkuu wetu ana taaluma ya ki-CIA, kwa hiyo utendaji wake wa kazi hauwezi kutofautiana sana na ule wa CIA. Huu ni mfano mmoja wapo wa kuwa anajua kufanya waterboarding na kuendesha Guntanamo Bay.

Anonymous said...

http://tinyurl.com/yppmhy

Anonymous said...

Tatizo lao hawajui kuwa huko JF wanakulana wao kwa wao! Kuna mtu alitoa wasi wasi muda mrefu kuhusu huyo mtu anayejiita Mwanakijiji na akasema mpaka na profession yake na wapi alikosomea intelligencia sasa watu wakampuuza tena ilikuwa mwishoni mwa mwaka jana. Ehe mio simo yasijenikuta yasiyonihusu.

Anonymous said...

Sasa hivyi JF inajulikana kama JamiiForums.com

ukitaka kutembelea nenda www.jamiiforums.com