Thursday, February 21, 2008

Mke wangu Mpendwa!

Mzungu na mke wake (1905)

Hii picha pia iko kwenye collection ya Northwestern University, lakini hawajui ni akina nani. Imepigwa Tanganyika enzi za Mjerumani.

10 comments:

Anonymous said...

Hao watakuwa wazazi wao akina Hans Poppe. Mtoto wao ni yule generali aliyeuliwa na Iddi Amin kikatili halafu Amin alisema jeshi la Tanzania ina wazungu! Mwingine alikuwa kati ya wale waliotaka kumpindua Nyerere.

Anonymous said...

Huyo mama ni kabila gani? Ana vidude masikioni.

Anonymous said...

Sio vidude ndugu yangu huo ndio ulikuwa urembo maridhawa wa mwanamke wa kiafrika. Huyu mama anaonekana ana hofu kweli kweli hapo usoni kwake hakuna tabasamu ya mapenzi. Halafu hizo kanga itakuwa pwani huko, mambo ya Tanga, Bagamoyo au Mzizima. Chemi kuna kitabu cha binti wa Sultani aliyetoroka na mjerumani wake kutoka Zanzibar, bibi huyo alilowea kabisa ujerumani sikumbuki jina la kitabu. Lakini wajerumani walizaa pia na wahehe huko Iringa na wachaga wa Kilimanjaro.

Anonymous said...

Ukute chifu kamkabidhi huyo mke. Kweli anaonekana kama ana hofu. Ni siku yao ya ndoa nini?

Anonymous said...

Huyo mama alipigwa na hofu baada ya kuona babaake kamuozesha kwa mtu (mjeremani, jerumani, )mwenye govi. Sasa akawa hajui la kufanya asuke au anyoe.

Anonymous said...

Huyo dada anajiona kaukata ila anaogopa hiyo kamera itapunguza maisha yake.

Chesi said...

Nimetatizika. kama hawawajui majina yao wanajuaje kama walikuwa ni mke na mume? Si inawezekana kuwa huyo ni Dakitari wa Kijerumani
akimuangalia mgonjwa wake kwa karibu? Maana hawa jamaa walivyokuwa wabaguzi...

Anonymous said...

Chesi wazungu na ubaguziwao wote lakini ikifika kwenye hiyo shughuli ya kunako sita kwa sita na kwa uzuri wa bibi zetu na utalaam wenyewe walikuwa wanaishiwa maneno! Ushahidi upo, wapo halfcaste wa kijerumani, kiingereza. Pia kuna binti sultani (huyu atakuwa wa Oman) alitoroshwa na afisa wa kijerumani kutoka Unguja eti walikuwa mapenzini.

Ushahidi mwingine tazama wamerakani weusi walivyochanganya hata kwa kubakwa nahao wazungu.

Ila nawashangaa wachina,sijui huwa wanakula dawa gani yaani jinsi walivyo wabaguzi wala usitegemee kuona watoto wa kichina na kiswahili kama wapo ni wachache sana na atakuwa amezidiwa kweli kweli!

Anonymous said...

Angekuwa Dr. huyo asingeweka mkono mabegani mwake huku anamwangalia kwa uchu mkubwa! Hiyo picha ikikuzwa ikawekwa makumbusho watu wanaweza kumkumbuka huyo bibi ni binti nani atakuwa tu yumo kwenye simulizi za kwao kwamba fulani ama aliolewa au alibebwa na mzungu!

Anonymous said...

Enzi hizo msichana miaka saba anaanza kufundwa mambo ya kukata viuno na kumtunza bwana! Huyo mzungu alinogewa kweli. Ni kweli hafucasti wako wengi Bongo!