Monday, February 25, 2008

Nafasi za Kazi Tanzania - Wizara ya Mambo ya Nje



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFATANGAZO LA NAFASI ZA KAZI


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa anapenda kuwatangazia Watanzania wenye sifa kutoka Bara na Visiwani, kuomba kazi zilizotangazwa hapa chini. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inazingatia usawa wa kijinsia katika kutoa ajira. Hivyo Wanawake wenye sifa wanahimizwa kuomba.Nafasi zinazotangazwa ni kama ifuatavyo:-


1. AFISA MAMBO YA NJE MKUU DARAJA LA I,TGS H(NAFASI 2)


KAZI ZA KUFANYA:


i) Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje kwa kutilia maanani masuala yaliyopewa kipaumbele katika kukuza na kuimarisha uchumi wa Taifa.ii) Kufanya tathmini za utekelezaji wa Sera mbalimbali za kiuchumi na kutoa ushauri na mapendekezo ya utekelezaji wake.iii) Kuratibu Wizara na Taasisi mbalimbali kutekeleza majukumu/makubaliano yaliyokubalika Kikanda na Kitaifa (Regional and International Cooperation) kwa wakati uliokubalika.

SIFA ZA MWOMBAJI:


i. Awe na shahada ya Uzamili (Masters) kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapoya fani zifuatazo:a. Uhusiano wa Kimataifa;b. Public Policy;c. Uchumi;d. Biashara ya Kimataifa; nae. Sheria ya Kimataifa.ii. Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta pamoja na uzoefuwa kazi kwa muda usiopungua miaka kumi na mbili

(12).SIFA ZA ZIADA:Awe mwenye uwezo wa kuzungumza lugha za kigeni kamavile Kifaransa, Kireno, Kirusi, Kichina, Kijerumani,Kihispania na Kiarabu.


2. AFISA MAMBO YA NJE MWANDAMIZO, TGS F(NAFASI 1)

KAZI ZA KUFANYA:1. Kuhudhuria mikutano ya Kimataifa.2. Kutafiti na kuchambua taarifa mbalimbali.3. Kuratibu njia za wageni toka nje zinazopitia Anga zaNchi yetu au kutua nchini.4. Kuratibu mabaraza ya pamoja ya ushirikiano baina yanchi yetu na Mataifa ya nje.5. Usaili katika ngazi za Kiwaziri na Kibalozi.SIFA ZA MWOMBAJI:i. Awe na shahada ya Uzamili (Masters) kutoka VyuoVikuu vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapoya fani zifuatazo:a. Uhusiano wa Kimataifa;b. Public Policy;c. Uchumi;d. Biashara ya Kimataifa; nae. Sheria ya Kimataifa.ii. Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta pamoja na uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka saba (7).

SIFA ZA ZIADA:Awe mwenye uwezo wa kuzungumza lugha za kigeni kama vile Kifaransa, Kireno, Kirusi, Kichina, Kijerumani,Kihispania na Kiarabu.


3. AFISA MAMBO YA NJE DARAJA LA II, TGS D(NAFASI 8)

KAZI ZA KUFANYA:i. Kuandaa Muhtasari, nakala na taarifa zinazohusu masuala ya mahusiano ya Kimataifa.ii. Kuhudhuria mikutano mbalimbali.iii. Kuandaa mahojiano.iv. Kufuatilia masuala mbalimbali ya kimataifa.v. Kufanya utafiti juu ya masuala mbalimbaliyanayohusu uchumi, siasa na jamii.vi. Kutunza kumbukumbu za matukio mbalimbali.

SIFA ZA MWOMBAJI:i. Awe na shahada ya Sanaa (B.A.) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serkali, na ambaye amejiimarisha (major) katika mojawapo ya fanizifuatazo:a. Uhusiano wa Kimataifa;b. Uchumi; nac. Sheriaii. Awe amefanya na kufaulu mtihani unaotolewa na Chuo cha Diplomasia, Dar es Salaam.iii. Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.SIFA ZA ZIADA:i) Awe mwenye uwezo wa kuzungumza lugha za kigeni kama vile Kifaransa, Kireno, Kirusi, Kichina, Kijerumani, Kihispania na Kiarabu.ii) Mwenye Shahada/Stashahada ya Uzamili (Masters/Postgraduate Diploma) kutoka VyuoVikuu vinavyotambuliwa na Serikali katikamojawapo ya fani zifuatazo:i. Uhusiano wa Kimataifa;ii. Public Policy;iii. Uchumi;iv. Biashara ya Kimataifa; nav. Sheria ya Kimataifa


4. AFISA TAWALA MWANDAMIZI, TGS F (NAFASI 7)

KAZI ZA KUFANYA:i. Kuandaa bajeti ya matumizi ya Wizara.ii. Kuratibu na kuhifadhi kumbukumbu za matukio muhimu katika Wizara.iii. Kufanya kazi za uhusiano na itifaki Serikalini.iv. Kushughulikia masuala ya nidhamu na ufanisi wa kazi kwa watumishi wa Wizara.v. Kusimamia utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo kulingana na mahali alipo.vi. Kuandaa taarifa za utendaji na matukio mbalimbali kila mwezi.vii. Kutekeleza utaratibu wa uundwaji na utendaji wa Mabaraza ya Wafanyakazi kwa mujibu wa kanuni na taratibu.

SIFA ZA MWOMBAJI:
i. Awe mwenye Shahada/Stashahada ya Uzamili (Masters au Postgraduate Diploma) kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali katika fanizifuatazo:-a. Utawala;b. Elimu ya Jamii;c. Sheria (baada ya internship);d. Menejiment Umma; nae. Uchumiii. Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta pamoja na uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka saba (7). Aidha, maafisa tawala wakaoajiriwa katika cheo hiki watatakiwa kufanya au kufaulu mtihani wa maafisa tawala katika kipindi cha miaka miwili tangu waajiriwe.

SIFA ZA ZIADA:Awe mwenye uwezo wa kuzungumza lugha za kigeni kama vile Kifaransa, Kireno, Kirusi, Kichina, Kijerumani,Kihispania na Kiarabu.


4. KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III, TGS B (NAFASI 2)

KAZI ZA KUFANYA:i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.ii. Kupokea wageni na kuwasaidia shida zao na kuwaelekeza sehemu wanapowezakushughulikiwa.iii. Kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi, na kumuarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitajika.iv. Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kaziWizarani.v. Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.vi. Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo, na kukusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.

SIFA ZA MWOMBAJI:i. Awe amehitimu Kidato cha Nne (IV) na kuhudhuria Mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua ya Tatu.ii. Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na awe amepata mafunzo ya kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika programu za windows, Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher.

SIFA ZA ZIADA:Awe mwenye uwezo wa kuzungumza lugha za kigeni kama vile Kifaransa, Kireno, Kirusi, Kichina, Kijerumani,Kihispania na Kiarabu.MASHARTI YA WAOMBAJI WOTE:1. Maombi yaandikwe kwa mkono na kuambatanishwa nakala za vyeti vya Shule, Vyuo, Vyuo Vikuu (Certificat and transcript) na kozi ulizohudhuria.2. Wasifu binafsi wa mwombaji (CV) pamoja na picha moja ya pasipoti ya siku za karibuni.3. Kwa wale wote walioajiriwa maombi yao ya kazi ni lazima yapitishwe kwa waajiri wao.4.


Waombaji wawe na umri kati ya miaka 18 na 45.5. Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi yote ni Februari 29, 2008.Maombi yote yatumwe kwa anuani ifuatayo:

Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
S.L.P. 9000
DAR ES SALAAM.

14 comments:

Anonymous said...

Wala msihangaike kuomba hizo kazi! Ndugu wa watu wameshapewa. Haya ni magrini tu!

Anonymous said...

matunda ya george bush hayo,hiyo ni groundwork ya tanzanias own FBI

Anonymous said...

wewe uliyetoa comment hapo juu nakuunga mkono msiangaike watu washapewa hizo kazi hayo magrini tu,labda ingekuwa shirika la kimataifa sio tz gov wanafiki tu kazi zina wenyewe

ned said...

Simply put ni hivi... usipo-take a shot you will miss it a 100% of the time. If you make an attempt and take a shot you have a 50-50 chance of getting it. Whatever the case, uchaguzi ni wako. Yawezekana kweli post ishakuwa filled... lakini tena inawezekana kabisa kuwa bado ipo wazi... Wakati tunakatishana tamaa, kuna watakao apply na mungu si Athumani - kupata. Wengine tutabaki stories tu.
Peace

Anonymous said...

Waombe tu, hapo si BoT, mawizarani watu wanapata,ila hata uwe na PhD BoT ni mbinde, teheteheteh

Anonymous said...

Jamani..mkae mkijua kwamba.."lisemwalo lipo na kama halipo linjiani" hivyo basi naunga mkono yote yaliyo semwa katika mchango..uhakika upo.
By:Sule

Anonymous said...

Mimi washikaji nahisi hizo nafasi nyingi zina wenyewe tayari si unajua tena mara huyu ni mtoto wa shangazi yangu huyu ni binamu yangu huyu ni mdongo wangu nakadhalika hii ndo bongo bwana. Ila washikaji nashauri tusiachekuomba hadi kitaeleweka tu siku moja manake sisi waislam tunafundishwa kuwa swala la riziki liko mikononi mwake yeye mwenyewe wala hakuna mtu atakayewewza kuizuia ila anachoweza ni kuichelewesha tu vinginvyo sisi tusio na vijisent tungepigika kinoma na pia tujue kuwa A STRONG MAN IS THE ONE WHO CAN STAND ALONE na pia hizo nafasi kama ni kumi ujue mbili ndo za kina sisi ambazo zinaitwa GOMBANIA MANYANI

Anonymous said...

my friends....its obvious that jobs are there!! lets try our best.e us not loose hope. it depends; sometimes the posts are still open...this is for sure, i used to say the same untill one day it came to pass, wizara hizo hizo...nikapata!! dont think that guys wont aplly, no n no! may guys will ost there application.....keep going.

Anonymous said...

guys, msiseme eti hizo nafasi ni za watu fulani! hizo kazi ni zetu sisi wenyewe. usipo omba wewe ujue unapunguza ushindani! usisikilize maneno ya watu kabisa. jaribu bahati yako. siku hizi 'undugu hamna', shule ndio inaangaliwa! jaribu uone, ndio jaribu leo....

Anonymous said...

jaman mimi wananikera sana wanapotangaza kazi halafu wanasema eti awe na experience ya miaka miwili, sasa sisi graduates tutapataje experience msipo tuajiri?????? basi serikali iweke sheria mtu anavyokuwa chuo ndio miaka ya experience.mimi mnanikera sana. na wala hzo kazi watu tusiojulikana hatupati. sana sana tunapoteza hela zetu za photocopy na stamp. jamani tuangalieni graduate ili na sisi tupate experience ya kazi eeh!

Anonymous said...

dah,ila kweli jamani,wapunguze hzo experience zao coz ni wengi tunaotamani sana kufany kaz katika wizara kma hzo,bt tunabanwa na hzo experience,itafutwe njia ya kukuza vipaji na ajira kwa vijana,tanzania bila vijana haiwezekani.

Anonymous said...

Unaposema experience ya miaka 7 una maana gani? Hii ni kudiscourage watu kwa sababu hizo nafasi wameshagaiana huko kindugunization, kwahiyo wana advertize formality tuu.
Hii nchi iuzwe tuu sasa tushachoka na sera za kitapeli na kazi za kitapeli, kila kitu utapeli tuu, mmeadvertise ya nini sasa??

Anonymous said...

siku zote tunakufa sisi watoto wa kabwela ila ipo siku mambo yatakuwa poa kama vipi masela ombeni ila ujue inahitajika bahati kubwa sana.utakuta hiyo ni gelesha tu wakwao wanawajua.

Anonymous said...

sijafurahia na comenti zilizonyingi, na tumeharibiwa na vitu tunavyopandikizwa kwenye akili zetu. pia saa nyingine mtu anatakiwaafahamike vizuri hasa katika ufanisi wa kazi, kwani ofisini siyo sehamu ya majaribio. pia wanao adivatize kazi waangalie wale wanaotokachuoni hata kwa nithamu,hekima walizokuwanazo vyuoni hao wanavyuo wapya. kwa upande wangu sijakata tamaa kuaply wizara yeyote ile ni vile elimu ya chini hatupewi kipaumbele, lakini mnatakiwamjue sisi ndio twawezafanyakazi kwa ufanisi zaidi tukipewa nafasi. jamani wasomi acheni siasa na muandike barua kwani unaambiwa mtembea bure siyo sawa na mkaa bure labda barua inawezahifadhiwa unashangaa siku moja wapigwa na kuambiwa unahitajika wizarani. jipe moyo mkuu mtanzania wa sasa.