******************************************************
HII IMEANDIKWA NA MILLARD AYO
TAARIFA NILIZOZIPATA MPAKA SASA KUHUSU KIFO CHA MWIGIZAJI STEVEN KANUMBA.
Posted: 7th April 2012 by MillardAyo in NewsPolisi wameondoka nyumbani kwa Kanumba muda mfupi uliopita baada ya kuwachukua waliokua wanaishi na Kanumba akiwemo mdogo wake Fetty ili kwenda kusaidia maelezo ya kilichotokea.
Bado watu wanazidi kuongezeka nyumbani kwa Kanumba ambapo tayari idadi kubwa ya wasanii wenzake wamefuka pamoja na watu mbalimbali, millardayo.com itaendelea kukufahamisha kinachoendelea kadri taarifa zitakavyozidi kupatikana.
Ila kumekua na taarifa nyingine ambazo hazijathibitishwa kwamba Kanumba alianguka na kuumia kichwani baada ya mpenzi wake ambae anatajwa kuwa ni mwigizaji LULU kumsukuma na kuanguka wakati wanagombana.
‘Inasemekana’ Kanumba wakati akijiandaa kutoka saa sita usiku aliingia bafuni kuoga, alipotoka alimkuta Lulu akiongea na mwanaume mwingine kwenye simu ndipo alipokasirika na ugomvi kuanza.
Alipelekwa hospitali Muhimbili ambako muda mfupi baadae alifariki dunia, mwili wake bado uko katika chumba cha kuhifadhia maiti Muhimbili hospital.
Hapo chini ni baadhi ya kauli nilizokutana nazo kwenye facebook wakati huu na chini yake ni maneno ya mwisho STEVEN KANUMBA kuyaandika kwenye kurasa zake za facebook na twitter.
BOFYA HAPA KWA HABARI ZAIDI!
2 comments:
rip steven kanumba wengi tulimpenda lakin mungu kampenda zidi lakin pengo lange alitafutika kamwe mungu ailaze roho ya marehemu mahara pema peponi ameni atuna jinsi ishakuwa
Laiti tungekuwa tunajua siku au saa tungekuwa tunajiandaa na hali ya umauti, lakini hakuna hata binadamu mmoja nayejua siku yake ya kuiaga dunia, Mungu atakupumzisha mahali pema, tutaendelea kukuezi kwa kuangalia kazi zako amabzo naamini zinakuweka katika hali ya kutosahaulika hapa diniani daima.
Ualale mahali pema peponi
AMINA
Post a Comment