Hii habari inatoka kwa mdau aliyeona hii picha ya 'Mzungu na mke wake 1905' . Bado hatujajua ni akina nani hao katika picha hii. Lakini Bwana Komba Muhili ameniletea habari za mzaa babu yake aliyelazimishwa kuolewa na mjerumani wakati huo huko Songea.
********************************************************************************
Binti Daria Adamu Juma
Imeandikwa na Komba Muhili
Hii picha inanikumbusha marehemu Mama mkubwa yaani Bibi yake Baba. Alikuwa anaitwa daria Binti Adamu alifariki mwaka 1981. Tulikuwa tunahisi alifariki akiwa na miaka 107. Alikuwa akitusimulia Habari za wajerumani wakati akisimulia alikuwa analia sana mpaka tunamwambia asilie kwani atatupa majonzi sana.
Yeye na familia yake waliishi katika Kijiji kimoja kiitwacho Rumecha, Songea wakati wa vita ya Maji maji alikuwa na miaka kama kumi na sita alikuwa amewekwa ndani si kama amefungwa amewekwa ili achezwe unyago pune vita ikaanza na wajerumani wakvamia kijiji chao.
Klichotokea ni cha kusikitisha baadhi walitekwa na wengine walikimbia cha kusikitisha zaidi yeye alikuwa mwali ndani akuweza kukumbia pamoja na familia yake ilibidi wakamatwe kilichotokea wazazi wake na nduguzake wote walipigwa Risasi na kufa papo hapo. Huku akiwaona wazazi wake wakiuliwa na wajerumani.
Kilichotokea yeye alichukuliwa na kamanda mmoja wakijerumani akawa mke wake bila ridhaa yake mwenyewe. Alikuwa aklia sana akikumbuka wazazi wake na nduguze alikaa na yule mjerumani zaidi ya miaka kumi na tano kama mke na mume kwani akuweza kufanya kitu chochote. Kilichotokea vita ilivyoisha tu yule mzungu akaenda nae Ujerumani na wakaishi huko na kubahatika kupata watoto wawili wakiwa na asili ya kizungu.
Baada ya kuzaa mtoto wa pili alilia sana na akaanza kususa hata kula akiulizwa shida nini akasema nakumbuka sana nyumbani hasa ndugu zangu. Basi yule mjerumani alichofanya alikuja nae mpaka Tanganyika akamuacha Bandari salama mwaka 1918 wakati vita ya kwanza ya Dunia ilivyokwisha.
Alivyofika hapa nyumbani alibusu ardhi ya Tanganyika huku akilia sana kwa uchungu alikuwa anafikilia watoto wake aliowaacha Ujerumani. Basi alifanikiwa kufika kijiji kwao kule Rumecha,Songea lakini akumfahamu mtu yeyote kilichotokea pale alipokewa na kukaribishwa kwa furaha.
Sasa kuna Mtu mmoja alitokea kumpenda sana Daria kilicho tokea pale alikubali kuolewa na yule mzee alikuwa anaitwa muhili komba na hatimae wakabahatika kupata watoto watano. Kati ya hao mmoja wapo ndio babu yangu mzaa baba na bahati nzuri niliishi nae. Mama mkubwa takribani miaka mitatu nikiwa na akili chakushangaza alikuwa mzee sana lakini meno yake yote yaliku meupe na hajang`oa hata moja.
Kwa kusema ukweli alikuwa mzuri sana nafikiri hata yule Mjurumani alimpenda kwa uzuri wake .Nimeona niwape kisa hiki ili nanji muone huko tilikotoka.
6 comments:
Kweli katika historia yetu kuna stories! Asante bwana Komba.
mbona huyu mama analia kuolewa na mzungu au anaogopa mateso ya kipindi cha utumwa lakini sasa hivi watoto wake au wajukuu wanakula raha majuu na raia wa majuu hata huko songea hawakujui wala tz watakuwa wanasema wanatoka afrika magharibi
mbona huyu mama analia kuolewa na mzungu au anaogopa mateso ya kipindi cha utumwa lakini sasa hivi watoto wake au wajukuu wanakula raha majuu na raia wa majuu hata huko songea hawakujui wala tz watakuwa wanasema wanatoka afrika magharibi
Janani hii story Chemi inasikitisha sana. Sasa huyo mama mkubwa watoto wake wa kizungu hawataki tena? jamani nao wamekuwa hawana mam, hii kali wajerumani walikuwa wabaya sana. Keep it up with good stories.
Byeeeeeee
Hitler aliua karibu watu weusi wote waliokuwa wanaishi Ujerumani wakati huo. Maskini lazima hao watoto waliuliwa. Bora yeye alirudi zake Tanganyika la sivyo na yeye angekufa.
That poor girl. She looks young and scared and then she will be abused by the German. But their children are worshipped because of their light skin and fine hair!
Post a Comment