Wednesday, February 20, 2008

Mwigizaji wa Bongo - Emmanuel Myamba

(kutoka kushoto, Emmuel Myamba, Mimi, Steven Kanumba)

Hii picha nilipiaga mwezi wa saba mwaka jana Bongo. Tulikuwa Magomeni, Dar es Salaam kwenye shoot ya filamu Bongoland II siku ya kwanza. Bongo Superstars Steven Kanumba na Emmanuel Myamba walikuja kututembelea kwenye seti. Sikujua kuwa huyo Emmanuel naye ni actor alielekea mpole kweli.

Nimebahatika kuona sinema ya Fake Pastors. Mle Emmanuel anaigiza kama Evangelist wa kanisa. Kwa kweli ana kipaji cha kuigiza yaani kama kuna tuzo ya Best Supporting Actor Bongo, anastahili yeye. Anaigiza vizuri mno mpaka wewe mtazamaji unasema unataka kumwona zaidi na zaidi. Unaamini kabisa kuwa huyo ni Evangelist anayependa kanisa lake, dini yake na waumini wake. Haonekani kama anaigiza hata kidogo. Natabiri ataenda mbali sana katika fani ya uigizaji na si Bongo tu hata nje ya nchi. Sinema ya Fake Pastors ina kasoro zake lakini huyo jamaa ni nyota!

4 comments:

Anonymous said...

huyo mshikaji anatisha!!! uwezi kuamini movie za kibongo zinaangalia watu sio vipaji!! wenye vipaji wapati nafasi kwenye movie, jamaa hata kwenye dar to lagos alifanya vizuri tuuu. na wapo wengi tuu bongo wenyewe vipaji ila hawajulikani na wahapati nafasi kwenye movie, movie zimejaa kanumba, vicent kigosi wale wale kila siku, director kanumba kila tu yeye lazima tachangua watu wake ndio waingie kwenye movie, inabidi hao bikira wafanye movie kwa wingi ndio wanajua kuchangua vipaji sio majina bila ya vipaji. na hadhani umenisoma!!!!

Anonymous said...

Kanumba anageacti kama Pator Patrick hapo ingenoga!

Anonymous said...

Dada Chemi, tafuta Dar to Lagos umcheki jamaa alivyoigiza vizuri! Huyu jamaa mie namkubali!

Unknown said...

Haswa! I couldnt have said it better! Niliona Fake Pastors, kwa kweli kutokana na raves zake zote, I was disappointed. Lakini huyo jamaa is really good. That is what I call acting. Hakuna tofauti na mhubiri wa kweli na yeye!