Sunday, June 22, 2008

75th Anniversary Screen Actors Guild Celebration - Boston

Jana nilikuwa kwenye sherehe ya kusherekea miaka 75 ya Screen Actors Guild (SAG) hapa Boston. Party ilifanyika katika hoteli ya Ritz Carlton, mjini Boston. SAG ni chama kinachowakilisha actors wote wa Hollywood. Mimi ni mwanachama na tawi letu hapa ni Boston Branch. Nilibahatika kupata mwaliko wa kujiunga na SAG baada ya kuigiza katika sinema mbalimbali. Nilijiunga mwaka huu. Bado nangojea 'break', yaani nafasi ya kupata role kubwa katika sinema ya Hollywood.

SAG ilianzishwa mwaka 1933 kutetea haki za waigizaji wa sinema za Hollywood. Kabla ya hapo walikuwa wanateswa na wakati mwingine kuwa kama watumwa wa studios. Mnaweza kusoma historia ya SAG hapa. Bofya hapa.

Hapa niko na baadhi ya marafiki zangu ambao ni actors wa hapa Boston. Katikati ni rafiki yangu, Ellen Becker-Gray (gauni nyekundu) Kutoka Kushoto, Ron Murphy, Rob Gray, Paul, mimi, Doug Weeks na Maria.


3 comments:

Anonymous said...

da chemi huyo alievaa nguo nyekundu mmefanana sana angekuwa mweusi ningeuliza nyie ni mapacha?

Anonymous said...

Hongera Da Chemi! Tena umetuwakilisha kwa kuvaa kinyumbani! Keep it up girl!

Anonymous said...

Da Chemi,
Hii picha inaelezea mengi cha zaidi na cha mno ambacho kimenigusa ni jisi unavyozidi kuutea uasili wako kwa maana ya kutoutupa mbali utamaduni wako. Jinsi ulivyo vaa kwenye picha hii mtu haitaji kuuliza asili yako bali atajua moja kwa moja ya kuwa wewe ni mwafrika. Asante sana dada, Mwanamke kitenge bwana. Keep it up. Chukua tano hizo.