Tuesday, June 10, 2008

McCain anasema ata Veto kila Bia!


Loh! Mgombea rais wa Republicans, John McCain kajikanyaga kweli. Kasema ata veto kila bia!

"I will veto every beer..." Yaani badala ya kusema akiwa rais ata 'veto' bill kasema ata 'veto' beer. Huwa maSenator wanaleta bill kuhusu mambo mbalimbali kwa rais na ni juu yake kuzipitisha au anaweza kupinga. Akipinga inaitwa 'veto'.
Sasa watu wamekasirika. Wapenda bia wanasema kuwa ni bora wananyime kila kitu lakini wasinyimwe bia zao! Wengine wanasema kuwa sasa ni wazi kuwa McCain ni mzee mno na hafai kugombea urais. Wanasema kuwa yeye ni mjinga kama George Kichaka na wanamwita McBush.

Mnaweza kuona na kumsikiliza hapa:

9 comments:

Anonymous said...

duh si mchezo anaendelea kujikanganya.

Anonymous said...

Akitaka kujua nguvu ya walevi AMWAGE POMBE YAO! Tehetehetehe

Stella Fumbuka said...

Huyu kikongwe akipata uraisi ni kasheshe nyingine kwa miaka minne ijayo-vita vyote (Iraq na Afghanistan) vitaendelea na si ajabu akaanzisha vingine dhidi ya Iran. Mawazo yake na kauli mbiu zake nyingine zinachanganya na kuduwaza kweli. Ngoja tuone ngoma itakavyokuwa

Stella Fumbuka said...

Dada Chemi, nimeshatoa ile picha mbaya na natumaini sasa nami utaniruhusu kuchangia hoja bila wasiwasi. Asante sana dadangu!

Anonymous said...

Jamani uyu babu miaka72 anahangaika anatafuta nini jamani? akiwa anatoa spichi utamuonea huruma anachusha, spichi flati! Pole zake. Nasubiri debate kwa hamu kwani braza atamsambaratisha mpaka atalose tempa, hapo ndo patam haswaaaaa.
Sue.

Anonymous said...

Au kwa kiswahili anaitwa McPori!

Anonymous said...

Da Chemi,Mimi binafsi ningependelea Mama Clinton awe mgombea mwenza wa Obama,ili kuunganisha nguvu za hao wawili against McCain.Nimekuwa nikisikia wachambuzi wakisema uwezekano kama huo utampa wakati mgumu Obama.Eti wewe unalionaje hilo na pia Je hali halisi ikoje uko kuhusu suala hili?
Niko Kinshasa

Anonymous said...

Lakn nadhani ni matamshi tuu beer/bill yanakuwa yananaelekeana wakati wa ku-pronounce

Anonymous said...

mpenda wowowo una matatizo. Sasa unaweka picha la jibaba linahomoa zinga la hamburger. Inachekesha kweli.