Monday, June 30, 2008

Kusogoa Chooni - Marudio


Niliposti kwa mara ya kwanza- August 23, 2006

Jamani Marekani watu maofisini wananishangaza sana. Kuna mtindo wa watu kusogoa na kupiga gumzo chooni. Tena kwa muda mrefu. Yaani mtu anajisaidia, huko mwenzake yuko nje anamsemesha. Au unaingia chooni na kukuta watu wamepiga kambi kwenye masinki ya kunawia mikono na kupiga soga, huko watu wanajisadia kwenye stalls. Wanasikia mtu anakojoa, au anadonssha haja kubwa, hao wanaongea bila kujali.

Kwa kweli nashangaa sana. Labda mtu akiwa anajisaidia haja kubwa ndo wakimbie kwa ajili ya mishuzi.Kwa kweli Restrooms/Bathrooms za Marekani maofisini ni safi sana, yaani unakuta toilet bowl cheupe kama vile bado kipya. Zinasafishwa mara kwa mara kwa siku. Nakumbuka Mbongo fulani aliwahi kusema vyoo vingine visafi mpaka unaweza kula huko, (mhhh sijui, mimi siwezi kula huko)! Usafi chooni ni muhimu sana hapa, na hao wanaosafisha wakizembea wanashutukia kazi hawana wanaletwa wengine. Lakini bado sijaona kama chooni ni sehemu ya kupiga gumzo.

Unaingia kwenye stall (kichumba chenye choo), mwenzako yuko nje kaona unaingia anaanza kupiga mastori. Aisei umesikia, hivi na hivi, je, unaonaje hivi na vile. Kwa kweli naona mkojo unataka kwa shida huko unajisaidia, huko unajaribu kuongea.

Lakini kuna kitu niligundua. Kisheria Marekani, mwajiri anarushisiwa kuweka recording devices kila mahala ofisini na Mfanyakazi asijue. Wanaweza kuwa na makamera na ma-audio device na usijue. Ila ni mwiko kuweka hizo devices chooni! Je, ni sababu ya watu kupiga gumzo chooni kwa vile wanajua

hawawezi kunaswa kwa ajili ya kupoteza muda kazini.

Mnaonaje kuhusu suala hii?

3 comments:

Anonymous said...

kusema kweli da chemi hao watu ni wastaarabu sio vibaya kupiga story au soga wakati mtu anajisaidia,..kusema kweli ukitaka kuona maajabu njoo lagos -nigeria.watu wanakunya nje barabaranii,alafu wanawake kwa wanaume.pamoja na huku wanapiga soga hata kupeana sigara .bila haya..mbona ya amarica poa..ya ya noma yapo nigeria..utalia wewe mwenyewe watu wasivyo na aibu..mbona sisi wabongo wastarabu sana.na hata hao wamerica ni wastaarabu pia,
mwana mtandao

Anonymous said...

Dada chemi.Kwa nature ya binadam mtu ni lazima usogowe wakati fulanifulani na sio kazi tuu mda wote na hii inasidia kurudisha akili hasa baada ya ku-concetrate kwenye kazi.Issue hapa nadhani ni eneo la kusogolea (yaani chooni!!!) kwa kweli nadhani hapa ni suala la utamaduni/mila,kwa mwafrika ni ngumu sana kwa mtu kujisaidia huku mwenzake anasikiliza 'kishindo'.kwa waafrika jambo la 'haja zote' ni sehemu ya AIBU yaani ina-associate na 'naked' na ndio maana vijiji vya kiafrika choo kina kuwa 'a distance' na nyumba.Sasa kwa wazungu wengi (sio US tu)nadhani utamaduni wao kwenye hili ni tofauti na waafrika na ndio maana wewe mwafrika Chemi unawashangaa wakati wao wanaona ni sawa tu.Je chemi unadhani hata kama vyoo ivyo vingekuwa usafi wake ni so-so wasingesogoa chooni?

Anonymous said...

je utafiti wako ni vyoo vya wanawake au na pia vya wanaume?? Nadhani kwa wanaume ni tofauti kwani chooni hakuna story hivyo. Kwanza vyoo sio visafi kwani watu wengi hukojolea juu. Na pia naona kama idadi ya vyoo haitoshi kulingana na wafanyakazi. Nadhani wanume wana aibu zaidi hivyo kila mtu anaondoka as soon as possible. Kuna wengine wanakwenda na gazeti kusoma lakini inakuwa sio mazungumzo.