Sunday, June 22, 2008

Sisi Marafiki Tutapata Mimba Pamoja!Jamani! Kwa kweli kuna habari ya kusikitisha sana kutoka Gloucester, Massachusetts. Wasichana 27 was shule ya sekondari huko Gloucester wamepata mimba. Ajabu ni kuwa hawa wasichana wanasherkea na kuringia mimba zao! Wana miaka 14 hadi 16.

Kama mko Marekani lazima mmesikia habari hizi kwenye TV na kwenye talk shows. Kwanza ni wasichana wengi mno waliopata mimba. Pili sababu ya wao kupata mimba, "eti wanataka kulea watoto wao pamoja na kuwa marafiki daima".

Huko kwenye zahanati ya shule, wasichana walikuwa wanapongezana wakithibitishwa kuwa wana mimba, na kulia wakiambiwa hawana. Si ndo watu walishutuka na kuanza kuchunguza kuna nini. Maana si kawaida kwa wasichana wadogo kutaka mimba, mara nyingi ni za bahati mbaya.

Baada ya uchunguzi waligundua kuwa hao wasichana wanatoka kwenye nyumba zilizovunjika, yaani mzazi au wazazi hawapo. Au hali ya maisha nyumabni kwako ni mbaya. Baada ya kuulizwa walisema kuwa "Nataka mtu ambaye atanipenda" (Mtoto).
Aliyemtia mimba msichana fulani ni jamaa wa mitaani ambaye hana pa kukaa mwenye miaka 24. Hapa Marekani ki kosa la jinai kwa mwanaume mwenye miaka 21 au zaidi kutembea na msichana chini ya miaka 17. Of course inatokea, lakini ole wao wakamatwe.
Na pia watu wanalaumu hiyo shule kwa ku-glorify (kusifia) uzazi na umri mdogo. Kuna day care safi sana (Nursery) kwa ajili ya watoto wa wanafunzi. Tena wanasema nzuri kweli. Wanafunzi wanapishana na wanafunzi waliozaa wakisukuma wanao kwenye baby stroller. Mmh!
Huko Gloucester, uchumi ni mbaya maana ni mji wa wavuvi. Kwa sasa kuna vikwazo vingi kwa wavuvi na ni shida wao kuvua samaki bila kuvunja sheria zilizowekwa. Na pia samaki wempungua baharini. Hali ya maisha umekuwa mbaya huko. Wengi wa wale wasichana na wanao wataishia kwenye 'welfare' (yaani kulelewa na serikali).
Tanzania nakumbuka wenzangu na ndugu zangu walifukuzwa shule baada ya kupata mimba. Je, wangekuwa wanafukuza wasichana hapa wangetaka kupata mimba kweli? Zamani hapa ilikuwa msichana akipata mimba, basi anatolewa kwenye hiyo shule na kupelekwa shule maalum.
Mnaonaje hii suala?

Kwa habari zaidi someni:

2 comments:

Anonymous said...

Hawa kwanza wangechagua mwanamme mmoja wa mbegu, ana akili, pande la baba, sasa wao wanatoa kwa omba omba, kweli mapenzi hayana macho. Lakini wametumia uhuru wao wa mawazo. Kweli majuu hamnazo, teheteheteheteheeeeeee

Anonymous said...

Kumbe wazungu hawana akili!