Friday, June 13, 2008

Nyama Pori Adimu Afrika

Wadau, hebu cheki hii habari. Wanasema nyama pori ni adimu huko Cameroon, Afrika Magharibi. Wanasema nyama wengine wamepotea kabisa.

Nadhani Afrika Mashariki hatujaingia kwenye hatua ya kusema nyama pori ni adimu. Wanyama walikuwa wengi kweli huko Afrika Magharibi kama walivyokuwa Bongo mfano Serengeti. Ila waliruhusu watu kuwamaliza. Bora Tanzania tuna hifahdhi za wanyama. Na wanyama wako kibao.

http://ac360.blogs.cnn.com/2008/06/13/whats-for-dinner-porcupine/

1 comment:

Chris said...

I wonder if you can justify kwamba wanyama Tanzania bado tunao wengi! Hususani Serengeti, kwetu ni Musoma! wakati wa kiangazi hadi late 80's nyumbu walikua wanakuja hadi majumbani kutafuta maji ya kunnywa! Hata wanawake waoga walikua wanawaua na kitoweo kinapatikana kwa nyumba karibu zote za karibu! Nilienda mwaka jana on my annual vacation, nikaenda zangu na kijijini Musoma! Ni jangwa, hakuna cha wanyama! Nyama pori (tunaita KIMORO) ilipatikana kwa sababu babu ni maarufu, na aliomba sana kwasababu niliitaka sana ili nikumbukie miaka hiyo! Da Chemi, tukiwa huku tunaona vitu vingine vi sawa, but nothing is sustainable! I was so disappointed! Ni jangwa, wanyama wameisha!