Wednesday, June 04, 2008

Tamasha la Filamu - Alliance Francaise

Tungependa kuwakaribisha waongozaji wote wa filamu hapa Tanzania kuzipelekea filamu zao pale Alliance Francaise – kwa ajili ya uchaguzi wa awali (preselection).

Filamu za kiswahili, hata za kiingereza, za aina na mitindo zote zinakaribishwa. Tafathali mnaombwa kuja kabla ya mwisho wa mwezi wa sita kuzifikisha hapo.

Filamu zitazochaguliwa zitaonyeshwa wakati wa Tamasha la filamu za Ulaya hapa Dar es Salaam. Tamasha hili linahuandaliwa kila mwaka, watanzania na raia wa nchi mbalimbali duniani hufika kuangalia filamu tofauti.

Tamasha hili huandaliwa na balozi za nchi za Ulaya na Kamisheni ya Ulaya hapa Tanzania.

Mwaka huu, kuanzia tarehe 10 mpaka tarehe 30 mwezi wa kumi, takribani filamu arobaini kutoka Ulaya zitaonyeshwa. Na zaidi kwa mara ya kwanza filamu za Tanzania zitaonyeshwa jijini Dar es Salaam na Arusha.

Kama unahitaji maelezo zaidi yoyote, kujaza fomu, kujisajiri na kuumua filamu zako, nenda Alliance Francaise, barabara ya Ali Hassan Mwinyi, nyuma ya Las Vegas Casino, Dar es Salaam. Tel. (022)2131406 / 0755481374 or email director@afdar.com, cultural@afdar.com.

Karibuni sana!

Regina
EFF Coordinator

No comments: