Friday, June 06, 2008

Sinema - The Surrogates


Wadau, mnakumbuka mwezi wa tatu niliitwa kwenye audition ya sinema, The Surrogates, ambayo stelingi wake ni Bruce Willis. Bahati mbaya sikupata role niliyofanyia audition, ila wiki ijayo wananichukua kwa siku mbili kucheza kama Dread. Nitakuwa mchafu mchafu na nitavaa nguo zilizochakaa hasa. Jana nilienda kwenye fitting ya costume, nilichukia kweli kuonekana kama ombaomba, lakini ndo hivyo tena. Sinema hiyo. Nitawapa updates wiki ijayo.
Hadithi ya The Surrogates inatokea mwaka 2054. Watu wanaishi maisha yao kupitia Surrogates robots ambazo wanafanana na binadamu lakini ni warembo na wazuri. Inatokea wimbi la kuliwa kwa maSurrogates na Bruce Willis ndiye anatafuta ni akina nani wako nyuma ya njama hiyo. Hao Dreads ni watu ambao wanataka kuishi kama binadamu.

6 comments:

Anonymous said...

hongera dada yangu hundio mwanzo baada ya hapo utapata nafsi kubwa zaidi. tengeneza cv dada. God bless you

Anonymous said...

Tunangojea kwa hamu kusikia habari kutoka kwenye seti. Hongera Da Chemi!

Anonymous said...

Kila siku longolongo eti audition sijui vi nini?Don`t waste your time gal uzee unakuzonga huko uliko,can you do something else?

Anonymous said...

Da Chemi una moyo na mambo ya sinema. Utakuwa na mafanikio makubwa. Tutasikia!

Anonymous said...

Wewe anony wa 3:20pm mbona unachekesha. Huoni sinema zinakuwa na watu wa kila aina. Hakuna uzee katika sinema. Au unataka mtu wa miaka 21 aigize mzee wa miaka 70?

Anonymous said...

mi sisemi humu