Tuesday, June 10, 2008

The Omen yatokea Kweli!


Picha kutoka Michuzi Blog

Wadau, mmewahi kuona ile sinema ya The Omen? Mbwa anazaa kitoto chenye umbo la bindamu. Kale kanachuliwa na mapadri na wanawapa mama fulani wa kitajiri ambaye ni mgumba. Kale katoto kanakuwa kazuri na kanalelewa katika maisha ya kifahari, kumbe ni mtoto wa shetani!
Nimeona hii picha kwa Michuzi na ilinikumbusha hiyo sinema. Anasema mdau kamletea picha kutoka Angola. Kwa maoni yangu hako kitoto katakufa siku za karibuni maana ni genetic deformation. Nimefuga mbwa wengi sana na nimeona vitoto vinazaliwa vingi wengine wazima wengine na deformations. Hao wenye deformations hawaishi muda mrefu.

DUH! Kweli kafanana na binadamu hata nywele za mbwa hana.

1 comment:

Anonymous said...

Nimeona The Omen. Huenda huyo kweli ni mtoto wa shetani. Duh! Au kuna mtu alitembea na huyo mbwa!