Monday, June 09, 2008

Tanzia - Omary Jaffary Ngwaya aka Salum Longa

Mwenyekiti wa Watanzania Italy alifika katika sehemu ya ajali na baadae kuongozana na polisi,huku akifuatana na Katibu mipango wa jumuiya ya Watanzania Napoli ndugu SALIM ISIHAKA, kwenda kuitambua maiti ya marehemu LONGA.Pichani Mwenyekiti katika sura ya majonzi akiwa na mjumbe maalum wa Jumuiya ndugu A.BENDERA(njano) , MR SAIDI na HAJI aka James ambao ni rafiki wa karibu sana na marehemu. (picha kutoka http://www.tnzncommunity.blogspot.com/)




Msiba Italy

MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WATANZANIA ITALY YA JUMUIYA ANAWATANGAZIA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI NA WATANZANIA WOTE HAPA ITALY NA NDUGU ABDULRAHAMANI A. ABDALLAH KWA NIABAHUKO NYUMBANI KUWA NDUGU YETU OMARY JAFFARI NGWAYA aka 50 cent au SALUM LONGA AMEFARIKI LEO ASUBUHI KATI YA SAA KUMI NA SAA KUMI NA MOJA ASUBUHI KWA AJALI YA GARI.
AJALI HIYO ILITOKEA SEHEMU YA ISCHITELLA/LAGO PATRIA MJINI (NAPOLI)BAADA YA DARAJA.

NAE KATIBU WA JUMUIYA YA WATANZANIA NAPOLI ANAWATANGAZIA WATANZANIA WOTE KUWA KUTAKUWA NA MKUTANO LEO SAA KUMI JIONI PALE MABEMBEANI,WOTE MNATAKIWA KUFIKA BILA KUKOSA ILI KUWEZA KUFANIKISHA MIPANGO YA MAZISHI. KWA WALE WOTE WALIO NJE YA NAPOLI TUNAOMBA MICHANGO YENU KWA ILI TUWEZE KUFANIKISHA MIPANGO YA MAZISHI HARAKA NA KUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU NYUMBANI TANZANIA.

KWA MAELEZO ZAIDI JUU YA KUWAKILISHA MCHANGO WAKO PIGA SIMU YA OFISI YA JUMUIYA
+39 081 3340635
FAX + 081 3340624
E-MAIL: tnzncommunity@yahoo.com

Marehemu amecha watoto wawili huko Tanzania.

REST IN PEACE LONGA!

PICHA ZA AJALI NA MAELEZO ZAIDI YAPO KATIKA BLOG YETU

3 comments:

Anonymous said...

Jamani kufia ugenini jamani! Sasa familia yake nyumbani watafanya nini maskini. Mola amlaze mahala pema peponi. AMIN.

Anonymous said...

he 50 cent hana pesa kwenye account ya kumrudisha home?

Anonymous said...

Doh inasikitisha. Jamaa alikuwa kwenye spidi kwenye kona. Maskini.

Mola ailaze roho yake mahala pema peponi. AMIN.