Monday, October 27, 2008

Maiti ya Mpwa wa Jennifer Hudson Yapatikana

William Balfour (Kushoto mwneye kofia) na mke wake Julia Hudson (Katikati) William ameshikiliwa na polisi kwa sasa. Inaelekea yeye ndiye aliyewaua Familia ya Jennifer Hudson.
Mama yake Jennifer Hudson, Darnell Donerson
Mpwa wa Jennifer Hudson, Julian King (7)
Kaka yake Jennifer Hudson, Jason Hudson (29)


Maiti ya mpwa wa Jennifer Hudson, Julian King (7), ulikutwa ndani ya SUV iliyokuwa imegeshwa upande mwa Magharibi mwa Chicago (West Side) leo asubuhi. Polisi wanasema kuwa mtoto alikuwa amebakwa na alipigwa risasi mara kadhaa.

Kwa kweli sijaweza kulala vizuri tangu nisikie habari za mama na kaka yake Jennifer kuuwawa siku ya Ijumaa iliyopita. Na sasa huyo malaika mwenye miaka 7 tu kauliwa kikatili hivyo.

Kwa sasa polisi wanamshikilia mume wa dada yake Jennifer, William Balfour (26). Habari zinasema kuwa wiki kadhaa zilizopita aliiba gari ya mke wake Julia Hudson, na kuiuza bila ruhusa yake. Ugomvi ulizuka hasa Julia alipokataa kumpa 'title' ya gari. Balfour alimtishia Julia kuwa atamwua mtoto wake na familia yake yote. Julia hakutoa taarifa polisi maana hakutegemea atatenda maovu yake ingawa jamaa aliwahi kufungwa miaka saba kwa kosa la kutaka kuua mtu.

Mungu alaze roho za marehemu mahala pema mbinguni. AMEN.

Kwa habari zaidi someni:

http://omg.yahoo.com/news/fbi-says-body-found-is-that-of-hudsons-nephew-7/14640

http://www.chicagotribune.com/chi-julian-king-1027,0,7364921.story

http://edition.cnn.com/2008/SHOWBIZ/10/27/jennifer.hudson.profile/?iref=hpmostpop

http://www.abcnews.go.com/Entertainment/story?id=6114149&page=1

http://www.chicagotribune.com/chi-jennifer-hudson-1028,0,7284673.story

2 comments:

Anonymous said...

REST IN PEACE! How tragic for Jennifer and her sister.

Anonymous said...

huyo mume wa dada yake jennifer ukimwangalia tu anasura ya kigansta. The boy was so cute jamani ndugu ndani ya familia tunachukiana namna hii? lakini hata kwetu Africa watu wanalogana na kuuana ndugu ni dhambi kubwa kwa Mungu, Mungu awalaze marehemu wote mahali pema uwiii marekani hii ikifika tarehe 4 Nov tutakoma!