Monday, October 06, 2008

Habari za Kuudhi! Vifo Vya Toto Disko Tabora

Kutoka Lukwangule Blog:


HABARI za kuudhi zinaendelea kumiminika kuhusiana na mkasa mzito wa kupoteza watoto 19 kwa mpigo wakati wa disko mjini Tabora kwenye sikuku ya Idd.

Baadhi ya watoto walionusurika kifo katika ukumbi wa Bubbles Night Club siku ya Idd mosi ambako wenzao 19 walipoteza maisha, wamesema wanaamini ulevi wa baadhi yao ulisababisha janga hilo.

Watoto hao walisema pia kwamba tathmini yao inaonyesha kwamba waliokuwamo ndani ya ukumbi siku hiyo walikuwa kati ya 1,000 hadi hata 1,500.

Uwezo wa ukumbi huo ambao ulijengwa kwa ajili ya mikutano ni kuhudumia watu wazima 150. Mmoja wa watoto hao akizungumza kwenye maziko ya rafiki yake ambaye walikuwa naye disko siku hiyo, Said Sudy (12) alisema siku hiyo ya tukio, mabaunsa wa ukumbi huo walikuwa wakimlazimisha kila mtoto aliyekuwa anaingia ukumbini kununua pombe aina ya Simba Gin.

Polisi inaendelea kuwatafuta mabaunsa hao ambao walikimbia baada ya tukio hilo .

Kwa habari zaidi ingia saiti ya HabariLeo:

http://www.habarileo.co.tz/

No comments: