Thursday, October 02, 2008

Maafa mjini Tabora!

Kitete Hospital Tabora Mortuary
Wazazi ndugu na marafiki wakisubiri kuchukua miili ya wapendwa wao

Wadau, bado sijaelewa watoto wote 19 hao walikufaje. Walilishwa sumu? Kulikuwa na sumu kwenye hewa? Paa iliwaangukia?

Na pia nimesikitika kuona mortuary ya Kitete hospital ni ile ile tangu nasoma Tabora Girls miaka ya 80! Haina refrigeration (ubaridi). Pia mjia wa Tabora umepanuka sana mbona mortuary ndogo?
Mungu alaze roho za marehemu mahala pema mbinguni. Amen. Hii ni hasara kwa taifa letu na ninshukuru kuona kuwa rais ameagiza uchunguzi ufanyike. Hongo isitembee hapo!
******************************************************************


RAIS Jakaya Kikwete amemuagiza Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw. Abed Mwinyimsa kuchunguza na kubaini chanzo cha vifo vya watoto 19 waliokuwa wakishiriki disko toto, tukio lililotokea jana jioni mjini humo.

Pamoja na watoto hao kufa wengine 16 wapo hospitalini Kitete kwa matibabu.
Watoto waliofariki ni Veronica Wanigu(7)Beatrice Makelele(14)Jacob Gerald (12)Salma Hamisi(12)Hadja Waziri(10) Rehema Moto (12)Seleman Idd (11) MrishoSeleman (10)Abdalah Rehan (14’)Agatha Manigu(12) Paulina Emanuel (11) Mohamed Kapaya (15) Ramla Yenga(15)Habiba Shaaban (14).Wengine ni Donald Kasela (12)Mwanahamisi Waziri (11) Ashura Jabal (12) na Yasin Rashid (11).

Waliolazwa hospitali hospitali hadi sasa baada ya wengine kumi kuruhusiwa ni Msimu Rehani (14) Naomi Joseph (13) Tatu Amani (15) Kulwa Idd(12) Sakina Ally (10) na Jumanne Abdallah(11) .

Rais kwa kupitia Waziri Athuman Juma Kapuya amesema kwamba amesikitishwa sana na tukio hilo na kutuma salamu zake za rambirambi kwa mkuu huyo wa Tabora na wafiwa.

Kutokana na agizo hilo serikali mkoani hapa imeunda tume maalumu itakayoshirikish
a wadau mbalimbali ili kubaini chanzo cha tatizo hilo na kuhakikisha halijirudii tena.

Kutokana na msiba huo, Rais Kikwete ametoa ubani wa shilingi laki tano kwa kila marehemu ambapo shirika la hifadhi ya jamii(NSSF) ambalo jengo lake ndilo lina kumbi hizo limetoa shilingi tano kwa kila marehemu na shilingi laki moja kama pole kwamajeruhi, na serikali ya mkoa wa Tabora imetoa shilingi elfu hamsini kwa kila marehemu.

Mitaa mingi ya mji huu imebaki kuwa na watu katika makundi makundi wakijadili tukio hilo na wengine wakilia kwa kupoteza watoto au ndugu zao.

Mkuu wa Mkoa ameagiza kufungwa kwa kumbi zote za disko na dansi mpaka atakavyotangaza vinginevyo.

Naye Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Tabora amesema kwamba wamiliki wa kumbi mbili za disko Bubbles Night Club, Shashikanti Patel na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Projestus ambaye anamiliki Top Five disco sound wanashikiliwa na polisi mjini hapa kufuatia tukio hilo.
Watu hao wanatakiwa kuisaidia polisi katika uchunguzi wake.

Msanifu wa majengo aliyesanifu jengo hilo la NSSF ambako tukio hilo lilitokea John Mlundwa alisema kuwa kumbi hizo zilijaza watoto kinyume na uwezo wake nakuongeza kuwa kumbi hizo zilijengwa kwa matumizi ya mikutano na matumizi ya ofisi na siyo matumizi ya sherhe za watoto kwani watoto wanatakiwa kustarehekatika maeneo ya wazi.

Picha hizi japo hazipendezi kwa namna yoyote ile ni jengo la NSSF Tabora ambalo lilikuwa na kumbi hizo za disko,chumba cha maiti cha hospitali ya kitete ambapo miili ya watoto hao ilikuwa inahifadhiwa na mamia ya wananchi wakiwa katika hospitali.Picha na mdau wa Tabora.
********************************************************

No comments: