Monday, October 27, 2008

Njama ya Kumwua Obama

Paul Schlesselman, left, and Daniel Cowart said they planned to kill more than 100 African-Americans.

Wadau, si nilisema wabaguzi bado wapo hapa Marekani na hawapendi kuona maendeleo ya watu weusi.

Leo jioni, Federal Bureau of Investigation (FBI) wametangaza kuwa skinheads (wabaguzi) wawili wamekamatwa wakiwa wakipanga kumwua Senator Barack Obama ambaye anagombea urais wa Marekani kupitia chama cha Democrats.

Pia hao wabaguzi walikuwa wamepanga kuua watu weusi mia moja. Wasingechagua watu wa kuua. Walipanga kwenye kwenye shule za weusi kusudi waue wengi! Walipanga wapite kwenye maenoe ya weusi na magari yao na kuwinda weusi! Jamani!

Leo nilikuwa naongea na watu hapa Boston na tulikubali kuwa weusi wako hatarini Obama akishinda. Kwanza hao McCain na Palin wamechochea ubaguzi kiasi kwamba wabaguzi wanaona ni haki yao kuua weusi. Juzi kwenye rally ya Palin mbaguzi alifoka Obama ni 'n-word' lakini Palin hakusema kitu.
Wadau mlio nje ya Marekani, ninawaomba mtuombee sisi ndugu zenu tulio kwenye mikoa ya hapa Marekani. Mtuombee usalama maana kuna watu wametabiri kuwa Obama akishinda na atashinda watu watakufa.'
Kwa habari zaidi someni:

3 comments:

Anonymous said...

hamna haja ya kuwaombea,just rudini tu nyumbani.
maombi yetu tutayaelekeza kwa wenye shida za kweli.

EDWIN NDAKI said...

Poleni sana ndugu zangu wote huko.Ubaguzi wa rangi bado upo sehemu nyingi tu katika dunia.

Binafsi nilishangaa nilipokutana na Skinhead huku Ufini eti amevaa T-shirt ya kumkashifu OBAMA.

Nikajiuliza huyu kiumbe yuko huku Ufini...yaani roho inamuuma sana kuona mtu mwenye asili ya afrika akiongoza Ameriac?je angekuwa anagombea hapa ingekuwaje.

Lazima wakubali siku hazigandi ..na hawawezi kuzui MVUA.

Walimwaga UGALI..sisi tumemwaga MBOGA..

TUTAFIKA TU

Anonymous said...

jamani si mrudi nyumbani muendeleze kilimo,yanini kusubiri kufa mweh!