Monday, October 20, 2008

Mtoto Albino auawa Bongo

Jamani, hivi huu imani na ushrikina unatupeleka wapi? Wanatoa roho ya mtoto aliyezaliwa albino, kisa???? Hao waliomwua wanaenda motoni! Kwa kweli serikali ifanye juu chini kuwakamata waliyomwua na wanyongwe hadharani.

Mungu alaze roho ya mtoto Esther Charles mahala pema mbinguni. AMEN.


***************************************************************************
Mtoto mmoja Albino auawa kikatili mkoani Shinyanga

Kutoka ippemdia.com

2008-10-20

Na Radio One Habari

Wimbi la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi -Albino limeingia mkoani Shinyanga kufuatia mauji ya mtoto mmoja Albino katika kijiji cha Shilela, Kata ya Segese wilayani humo.

Mtoto huyo wa kike aitwaye Esther Charles, mwanafunzi wa Darasa la Tatu katika shule ya msingi kijiji hapo ameuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana.

Diwani wa Kata ya Segese Bwana Joseph Mayala amesema watu wasiojulikana wakiwa na mapanga usiku wa manane walivamia nyumba ya Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Bwana Mzolewa Mashili ambaye ni baba wa mtoto huyo kwa kuvunja mlago wa nyumba yake kwa kutumia jiwe kubwa.

Amesema watu hao waliwaweka chini ya ulinzi wazazi wa mtoto huyo na kuanza kumchuna sehemu za usoni, kichwa hadi ngozi ya kisogoni na kumkata miguu yake kuanzia sehemu za nyonga na kuondoka nayo.

Diwani huyo amewataka wananchi wakiwemo walinzi wa jadi Sungusungu Wilayani Kahama kuhakikisha watu wanaojihusisha na mauaji hayo wanafichuliwa.

SOURCE: Radio One

No comments: