Thursday, October 02, 2008

Maafa mjini Tabora! - Part 2

Okay, ni hivi....hao watoto walikufa kwa kukosa hewa (Suffocation). Wanasema kuwa kuna joto sana mjini Tabora sasa na ule ukumbi ulikuwa umejaa kupita kiasi.

Sasa si uchu wa pesa huo? Mnajaza watu kupita kiasi katika eneo ndogo, unatagemea nini? Wafilisiwe hao washenzi wenye klabu na wafungwe gerezani maisha!


Watoto wamepoteza maisha yao shauri ya uchu wa pesa!

Hivi hakuna standards za kusema, eneo fulani unatosha watu kiasi fulani tu? Mfano chumba kinatosha watu 50 lakini mnaweka watu 300! Kuna wakaguzi huko? Hapa Marekani hiyo ni moja ya kazi ya zimamoto.

Hii ni jambo la kisikitisha sana tena mno na ni aibu kwa nchi yetu.

Poleni wafiwa. Mungu alaze roho za marehemu mahala pema mbinguni. AMEN.

Vyombo vya habari vya kimataifa sasa wanatangaza habari hizi someni:

http://www.bloomberg.com/apps/news?pid=20601116&sid=apHD09_PuR1w&refer=africa

http://www.nation.co.ke/News/-/1056/476772/-/tkwn0r/-/

http://afp.google.com/article/ALeqM5j4Yux0NoN6fz9qovrCN9uTpMSNsA

http://www.cnn.com/2008/WORLD/africa/10/02/disco.deaths.ap/index.html

**************************************************************************
Kutoka gazeti la Daily News:

http://dailynews.habarileo.co.tz/home/?id=7627

RAPHAEL LUCAS in Tabora
Daily News; Thursday,October 02, 2008 @19:01

President Jakaya Kikwete has sent condolences to the families of 19 children who died in a discotheque when celebrating Idd el Fitr, calling for a thorough investigation into the matter -and stern measures taken against all those involved. Six other children are hospitalized, two of them in critical condition, following the incident.

The owner of the club, Mr Shashi Patel, is under police custody as authorities continue with investigations. The Minister for Labour, Employment and Youth Development, Prof Juma Kapuya, said that the president had also given 500,000/- to the families of children who perished in the accident.

Prof. Kapuya said that President Kikwete received with profound shock the children’s death that occurred at around 6:30 pm at Bubbles Night Club within Tabora municipality on Wednesday. According to the Tabora Acting Regional Police Commander, Mr Daudi Siasi, the tragedy struck after the children suffocated within the club’s overheated poorly ventilated dance floor.

Tabora municipality is at the moment very hot with temperatures recorded at over 33 degrees Centigrade. The children who perished were aged between 7 and 15 years. Reports from Tabora say that the Uyui District Medical Officer, Dr Moses Makelele, lost two children in the tragedy. His wife passed away three weeks ago.

The National Social Security Fund (NSSF), owners of the building that houses the club, have also promised to give another 500,000/- to the families of each of the children that died in the tragedy and 100,000/- to the families of the injured children.

Tabora regional authorities have given each family of the deceased children 50,000/- and the go-ahead for them to bury their dead. Mr Siasi identified those who died in the incident as Veronica Manigu (7), Beatrice Makelele (14), Jacob Gerald (12), Salma Hamis (12), Khadija Waziri (13), Rehema Moto (14), Selemani Iddi (11), Mrisho Selemani (10), Abdallah Rehani (14) and Agatha Manigu (12).

Others are Paulina Emmanuel (11), Mohammed Kapaya (15), Ramla Yenga (15), Habiba Shabani (15), Donald Kasera (12), Mwanahamisi Waziri (11), Philipo Haule (11), Ashura Jacob (12) and Yasini Rashidi (11). Those injured are Msimu Rehani (14), Tatu Amani (15), Kulwa Iddi (12), Sakina Alli (10); the latter was discharged but later returned to hospital. Two of the casualties are in critical condition – Jumanne Abdullah (age not immediately established) and Naomi Joseph (13).

5 comments:

Anonymous said...

Life is so precious. Do we Tanzanians realize that? The culprits must be punished severely!

Anonymous said...

Poleni Tabora.
Tukio kama hili linahitaji Rais Jakaya kwenda kutoa pole, hasa inapozingatiwa kwamba huwa anahudhuria ajali za watu ambao huwa wanamajina pale Muhimbili. Hili ni swala kubwa na sio kumtuma Mh. Kapuya.
Anatakiwa kuwasili katika eneo la tukio na kukagua , kutoa pole na pia kuhutubia wananchi.
Pia ni wakati wa TZ, hasa Fire marshal kuanza kuangalia uwezo wa sehemu za disco kuchukua kiasi fulani cha watu na njia za tahadhari (Exit)kama hali kama hii ikitikoea.Ikiwa ni pamoja na kuwa na Genereta, na wasaidiza wa haraka.

Anonymous said...

HAWA WAHINDI NDIO KAWAIDA YAO WANAWEKA MASLAHI MBELE BILA YA KUJALI WANYONGE. HUU UKUMBI UNAENDESHWA NA MHINDI AMBAE AMEJAZA WATOTO KWA KUJIPATIA KIPATO ZAIDI. AFUNGWE MILELE.

LOAKINI PIA NIMESHTUSHWA NA HUO MKONO WA POLE WA RAIS NI AIBU NI LAKI5 TU? RAIS? INA MAANA UKIGAWA KWA FAMILIA 19 NI KAMA 26 ELFU HIVI NI FEDHA NDOGO SANA KUTOKA IKULU WAKATI STAREHE NA VITU VYENGINE HUTUMIA MAMILIONI.

TABORA AUTHORITY IMETOA KILA FAMILIA 50ELFU SASA ITAKUWAJE WAMSHINDE RAIS WA NCHI ALIETOA LAKI5 KWA FAMILIA ZOTE?

Anonymous said...

Poleni sana wafiwa. Nafikiri huu ndio wakati muafaka hata serikali kutunga na kupitisha sheria kuhusu idadi ya watu wanaoruhusiwa kuwa katika jengo na pia ni jinsi gani ventilation iwepo.

Pia naona watu wameshaaamua tatizo lilikuwa suforcation lakini huenda hata hilo jengo laweza kuwa na hewa zingine zisizofaa kwa matumizi ya binadamu, labda kuna mtu kaweka mikemiko pahala ktk hilo jengo.

Pia hii inaenda kuonesha ni jinsi gani viongozi wetu hawajali watu wao tena taifa la kesho! Yeye Pinda waziri mkuu anaonekana kuendelea na ziara zake huko kwene mkutano wa Asia Pasifiki wakati watu wake wana angamia.

Da chemi unakumbuka Daraja la MN lilipobomoka comishina wa usafiri akashindwa kurudi nyumbani akafukuzwa kazi? na Gavana wa PA ilibidi arejee kama sikosei kutoka kwene ziara yake huko uchina pale watu wale walipofukiwa kwene machimbo ya makaa ya mawe. Lakini kwetu sisi trend inaonekana viongozi wetu hawaoni wanapaswa kuwa mahala ilikotokea janga kwa wakati. Mfano mzuri ni pale MV bukoba ilipozama Waziri mkuu wakati huo Sumaye aliendelea na ziara yake Afrika kusini na safari Pinda Mizengo Pita yeye anaendelea na ziara yake huko Ghana

Simon Kitururu said...

Poleni sana Wafiwa!:-(