Saturday, October 25, 2008

Mama na Kaka wa Jennifer Hudson Wameuawa!

Jennifer Hudson ma Mama yake mzazi

Kuna habari za kusikitisha. Mama yake mzazi Jennifer Hudson, Darnell Donerson (57), na kaka yake Jason Hudson (29), walmeuawawa kikatili jana nyumbani kwao huko Chicago. Mpwa wake mwenye miaka 7 anatafutwa na polisi wametoa Amber Alert (tangazo maalum kwa ajili ya watoto waliohatarini). Polisi wanamshikilia William Balfour (27) ambaye ni mume kwa mdogo wake.

Jennifer Hudson alipata tuzo la Oscar mwaka jana kwa ajili ya sinema, Dreamgirls. Aliigiza kama Effie White ambaye alikuwa mwimbaji mkuu wa kikundi cha Dreamgirls kabla ya kupinduliwa na Deena Jones (Beyonce). Jennifer alipata umaarufu kwenye American Idol.

Wiki iliyopita sinema, The Secret Life of Bees, ilitoka. Jeenifer anaigiza mle na akina Queen Latifah, Alicia Keys na Sophie Okonedo. Hivi karibuni kachumbiwa na mwanasheria na mwigizaji, David Otunga.

Mungu awalaze roho za marehemu mahala pema mbinguni. Amen.

Watu wanauliza kwa nini Jennifer hawakuhamisha familia yake kutoka South side ambayo inajulikana kwa kuwa eneo hatari sana huko Chicago. Habari zinasema kuwa mama yake hakutaka kuhama maana alikaa pale maisha yake yote.

Kwa habari zaidi someni:

http://www.latimes.com/news/nationworld/nation/la-na-hudson25-2008oct25,0,4062243.story

http://hollywoodinsider.ew.com/2008/10/jennifer-hudson.html?iid=top25-20081025-Jennifer+Hudson

http://ap.google.com/article/ALeqM5iIqSbmp7cCrnSvw1FIMxIvjQa8AQD941DLG80

7 comments:

Anonymous said...

Poleh sana Jennifer Hudson.

Anonymous said...

Innalillah wainna ilaih rajiuun, inshallah mwenyezi mungu awasamehe makosa yao na ampe imani jenniffer koz this ia not easy but inshallah she will get there, we are all in the same path, ila kutangulia ni kugumu.

Wote imetugusa

Chemi Che-Mponda said...

Wadau, hamwezi kuamini kuna watu wanafurahia hivi vifo. Wanasema eti ni malipo kwa vile Jennifer hakustahili ile tuzo la Oscar. Mimi nasema alistahili 100% ile Oscar ukilinganisha na wale wanne wenzake wlaioteuliwa kwenye Best Supporting Actress Category. Pia Mungu yupo, hao wanaofurahia watakiona!

Natoa tena pole kwa Jennifer Hudson na dada yake na mpwa wake. Tuombe wamkute huyo mtoto yu hai.

Anonymous said...

Mungu awapumzishe kwa amani na kumjaza faraja na matumaini Jen

Anonymous said...

Huku Marekani kuna mambo ya ajabu mimi sijawahi kuona sasa subirini Obama akishinda. Ila dada chemi hiki kiswahili chako cha kuuliwa si sahihi mara nyingi sana unatumia neno hili ni kuuwawa si kuuliwa please! unaniangusha

EDWIN NDAKI (EDO) said...

pole Jennifer.

Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi.Amina

Anonymous said...

nimesikitishwa sana na hizi taarifa mbaya.Mungu awape wafiwa faraja ya kweli katika kipindi hiki kigumu.