Friday, October 17, 2008

Tanzia - Ndalima Yusuph Nzaro

Wadau, nimesikitika sana kupokea habari za kifo cha Ndalima Yusuph Nzaro. Alipata ajali ya gari huko Michigan wiki hii na kufariki kutokana na majeraha aliyopata.

Ajali ilisababishwa na kijana mhuni na asiye na adabu mwenye miaka 15. Inaelekea anatoka kwenye familia inayojiweza sana hapa Marekani. Wadau, tufuatilie kwa makini kesi ya huyo kijana itaishaje. Nina wasiwasi kuwa tutamwaona anakata mitaa hivi karibuni baada ya familia yake kukodi mwanasheria wa bei mbaya.

Huyo kijana anatashilii kushitakiwa kama mkubwa na kwa kosa la vehicular homicide na makosa mengine mengi.

Ninatoa pole kwa familia ya Nzaro. Mola ailaze roho yake mahala pema peponi. AMIN.

*************************************************************************************
HAYATI NDALIMA YUSUPH NZARO

Kwa masikitiko makubwa Familia ya Mohamed Nzaro na Balozi Eva Nzaro inatangaza kifo cha mtoto wao Ndalima Yusuph Nzaro kilichotokea jana Alhamisi Katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Michigan mjini Ann Arbor ambapo alikuwa amekimbizwa kutibiwa baada ya ajali ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia Jumanne ya Oktoba 14, 2008.

Gari alilokuwa akiendesha marehemu liligongwa na gari nyingine wakati likisubiri taa za kuongozea magari.

TAARIFA ZA AJALI HIYO IPO HAPA http://www.clickondetroit.com/news/17709594/detail.html?taf=det

Mipango ya kuusafirisha mwili wa marehemu nyumbani Tanzania kwa mazishi inaendelea. Vile vile, utoaji wa heshima za mwisho mjini Detroit unatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 18 Oktoba, 2008. Muda rasmi utatangazwa baada ya maandalizi kukamilika.

Familia inapenda kutumia nafasi hii kuwashukuru na kuwaomba msaada wenu wa hali na mali katika kufanikisha safari hii ya mwisho ya kijana wao mpendwa Ndalima.

Michango kwa ajili ya msiba huu inaweza kupelekwa moja kwa moja kwenya akaunti maalum ifuatayo:

Bank Of America:
A/C Name: Mboja Nzaro (Dada wa Marehemu)
Routing No. 072000805
A/C No. 5407722411

Mawasiliano zaidi Kuhusu habari za msiba huu wasiliana na wafuatao:
Anna Royal Mfinanga 248-778- 6395
Abdul Kufakunoga 248-515- 5509
Salum Ndolanga 248-796-1267
Philemon Mnzava 248-417-5015
Leo The Saint 614-426-3422

Msiba huu kwa Detroit unafanyika nyumbani kwa binamu yake Ayubu Mfinanga.
Anuani ya Kwa Ayub:
22255 Hessel Detroit,
MI 48219
Tutaendelea kuwahabarisha kwa kadiri mipango inavyoendelea.
Asanteni kwa sala zenu, ushirikiano wenu na misaada yenu.
FAMILIA YA NZARO

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Marehemu astarehe kwa amani amina