Wednesday, June 25, 2008

Wazimbabwe Wakatwa Mikono na Vidole! - Ushenzi wa Mugabe


Ama kweli raisi Mugabe wa Zimbabwe kawa kichaa mwendawimu. Badala ya kutoka kwenye ofisi ya raisi na heshima zake atatoka kama mnyama!
Leo kuna habari kuwa watu huko Zimbabwe wanakatwa mikono na vidole kusudi wasipige kura. Wengine wamevunjwa mikono na vidole. Pia watu wanapigwa ovyo!

Na mpinzani wake, Morgan Tsvangirai ameomba hifadhi kwenye ubaolizi wa Uholanzi huko Zimbabwe.
Sikutegemea kuwa nitasikia habari za kusikitisha kama hizi kutoka Zimbabwe. Kweli huyo Mzee Mugabe kapatwa na 'senility' (kichaa) ya ajabu. Labda anadhani ataishi daima. Ametawala Zimbabwe kwa miaka 28 na sasa ni nchi enye dhiki.

Kwa habari zaidi someni:


1 comment:

Anonymous said...

Hivi jamani Mugabe ana nini haswa? mi bila shaka nadhani atakuwa na mapepo huyu, Mungu msamehe na ampe upeo wa kujua anachokifanya si kizuri, Mungu wahurumie wazimbabwe.
Ms Bennett