Sunday, August 17, 2008

Hongera Flaviana Matata!

Kutoka Jiachie Blog

Pichani ni Miss Universe Tanzania 2007 Flavian Matata akiwa nchini South Afrika ambapo ameuchinja kwa kusaini mkataba wa mwaka Mmoja na Kampuni ya kubwa ya mitindo ya Ice Model Agency,pamoja na mambo mengine Flavian Matata anatarajia kutua mapema mwezi huu nchini Tokyo Japan chini ya mwaliko wa kampuni ya Wilna International Limited ya Japan ambapo atajaribu zali na kampuni kubwa ya mambo ya Ulimbwende nchini humo ya Jones.Blog ya JIACHIE inamtakia kila la kheri mlimbwende huyu katika kuifanikisha ndoto yake zaidi katika masuala ya Modeling.
*****************************************************************
Na mimi nampongeza Flaviana kwa kupata mkataba na moyo wake wa kuendelea na modelling. Naomba afike mbali katika fani huo. Flaviana ni wa pekee, na tusisahau alivyofika mbali katika mashindano ya Miss Universe. Bado wanazungumzia kipara chake. Flaviana ni mfano wa kuigwa.

1 comment:

Nalitolela, P. S. said...

Dachemi nina comment ambayo haihusiana na hii post, ila inahusiana na blog yako kiujumla.

I am guessing you recently changed something in your template, sasa alignmnet ya page items imevurugika kabisa kamma unaangalia kwa kutumia Firefox.

Since Firefox is a highly rated browser; its are increasing on a daily basis even amongst windows users, and it is arguably the better browser; hivyo basi ningekushauri uwe una-preview your changes in both IE as well as Firefox (kama una muda na uwezo, hata browsers nyingine pia). That way you know watembeleaji wako ambao default browsers zao sio IE hawabaki nyuma