Friday, August 22, 2008

Ridhiwani Kikwete Aoa!

Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwa na mai waifu wake mara baada ya kufunga ndoa leo ukumbi wa ubungo plaza, dar. Maharusi wote ni wanasheria na wanafanya kazi mjini Dar es Salaam.

Akina dada mliokuwa mnamwania bachela Ridhiwani Kikwete, mlie tu. Leo amemwoa kipenzi chake Bi Arafa Mohamed. Hongera Ridhiwani na Arafa, nawatakaieni maisha mema ya ndoa. Zaeni matunda mema.

Pichani - Rais Jakaya Kikwete akimuaga mkwewe Bi.Arafa Mohamed pamoja na mtoto wake Ridhwani Kikwete muda mfupi baada ya mtoto wake kufunga ndoa na Bi Arafa katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam leo majira ya alasiri kuelekea Magharibi. Picha imepigwa na Freddy Maro wa Ikulu.

No comments: