Friday, August 08, 2008

Morgan Freeman atoka Hospitalini

(pichani) Morgan Freeman na Mke wake

Mcheza sinema mashuhuri, Morgan Freeman (71), ametoka hospitalini leo baada ya kufanyiwa upasuaji kutokana na majereha aliyopata katika ajali ya gari hivi karibuni huko Tennessee.

Kwa kweli ni habari njema kuwa tutazidi kumwona Mzee wetu akiigiza kwenye sinema zingine siko zijazo. Wanasema kuwa itabidi avae 'neck brace' (kifaa cha kukaza shingo) kwa miezi sita hadi minane. Tunamwombea apate uzima.

Ila kuna habari za kusikitisha kuhusu Mzee Freeman. Habari zinasema kuwa anaachana na mke wake Myrna Colley-Lee (67) baada ya miaka 24 za ndoa. Bi Myrna ni mke wake wa pili, wa kwanza ni Jeanette Adair Bradshaw.
Mzee Freeman alipata ajali akiwa anaendesha gari la mwanamke fulani, Demaris Meyer, (48) ambaye mwanzo walidai kuwa ni rafiki wa mke wake. Sasa wanasema kuwa ni mpenzi wa Mzee Freeman! Kumbe bado wamo!

1 comment:

Anonymous said...

Asante Viagra!