Wednesday, August 27, 2008

Obama Ateuliwa Rasmi!


Senator Barack Obama wa Illionois, leo ametuliwa rasmi kuwa mgombea rais wa Marekani kupitia chama cha Democrats. Ni jambo la kihistoria maana yeye ni mtu mweusi wa kwanza kuteuliwa na chama kikubwa hapa Marekani kuwa mgombea rais.

Kesho Obama atakubali kuteuliwa kwake. Watu wanangojea kwa hamu kusikia atasema nini.

Mungu amlinde yeye na familia yake maana wabaguzi bado wamejaa hapa Marekani. Hata juzi tuklisikia wazungu watatu walikamtwa wakiwa na mpango wa kutaka kumwua kesho akienda kutoa hotuba yake huko Colorado.
Kwa habari zaidi soma:

3 comments:

Anonymous said...

hivi jesse jackson hajawahi kuteuliwa kuwa mgombea?

Anonymous said...

INA MAANA ZOGO LOTE LILE ALIKUWA HAJATEULIWA NA CHAMA CHAKE? SASA KAMA WANGEMKATAA INGEKUWAJE NA YEYE ALISHAMSHINDA HILARYY CLINTON NA PIA AMETUMIA FEDHA NYINGI KWA KAMPENI ZAKE. ACHILIAM BALI MUDA NA USUMBUFU, UTUKANWA NA KASHFA. SASA NDIO WANAMTEUWA RASMI?AU HICHO KITENDO CHA KUMTEUWA JUST NI RUBBER STAMP TU HAKINA UZITO WOWOTE?

Anonymous said...

Mungu awalinde Obama na familia yake in Jesus name Amen.