Friday, August 22, 2008

DVD za Bongoland II Zinapatikana sasa!


Kwa wadau wa Boston, nitakuwa nazo wiki ijayo. Unaweza kuwasiliana na mimi kupitia e-mail chemiche3@yahoo.com.

************************************************************************
Taarifa kutoka Kibira Films:

BONGOLAND II - IMETOKA KWENYE DVD - AGIZA LEO

Kusubiri kumekwisha BONGOLAND II imetoka katika DVD. Jipatie nakala yako kwa kubofya hapa.

Kama kawaida ys filamu za Kibira Films , unapojipatia filamu ya Bongoland II unapata zaidi ya filamu yenyewe katika DVD. Utaweza kuona jinsi sinema hiyo ilivyotengenezwa pale mjini Dar, katika vitongoji vya Manzese, Magomeni na Tenki Bovu. Pia utaona milolongo iliyowatesa watengenezaji wa sinema hii walipokuwa pale mjini Dar. Vile vile utaona watu wote walioshiriki katika utengenezaji wa sinema hii kama waliotupatia nyumba, usafiri na kadhalika. Pia katika DVD hiyo utaona scene ambazo ingawaje zilikuwa sehemu ya sinema, lakini hazikutumiwa katika makala ya sinema ya mwisho.

Mwisho unapata sinema iliyotengenezwa na wasanii wa kitanzania waliokubaliwa katika matamasha ya kimataifa kuanzia Zanzibar, Marekani na Uingereza mwezi wa kumi mwaka huu wa 2008.

Kibifa FIlms inakuhakikishia kuwa sinema hii itakuburdisha na kukufurahisha sana maana kusema kweli kama hadithi inavyosema "kuondoka kutoka nyumbani kama Juma ni rahisi kuliko kurudi nyumbani"

Jipatie makala yako hapa.

Kwa wale wote mlioko Bongo, mipango iko mbioni kwa kuwaletea BONGOLAND II!!

No comments: