Wednesday, August 20, 2008

MAKUBWA....Bongo Kesho!!!!!!


Kaka Beda Msimbe (Lukwangule Entertainment Blog) anatabiri kuwa kesho yatatokea makubwa huko Tanzania!

*******************************************************************

Gumzo la Lukwangule

Kesho kuna kitu kinataka kutokea nchini hapa, natumaini si kuvunjwa tena kwa baraza la mawaziri, manake hii sasa itakuwa taabu kubwa, lakini ni wazi Rais Jakaya Kikwete
kesho ataleta taabu kidogo mpaka hotuba yake imalizike na kila mtu ajuwe nini kimetokea.
Si kawaida kwa rais katikati ya safari yake akahutubia Bunge moja kwa moja labda kuna daawa inatafutwa kwa tatizo kubwa au anavunja bunge, natumaini tena si kuvunjwa kwa bunge manake itakuwa sooo.

Bungeni kesho asubuhi kila mtu atakuwa tisti, hii ni kutokana na rais kuifanya ziara yake hiyo bungeni kuwa ni siri yake mwenyewe hata wasaidizi wake hawajui wanahisi tu Rais ataenda kufanya nini. Masikhara hayo!!!

Ni baada ya maswali na majibu mishale ya saa nne Rais atakuwa yu katika mimbari ya pale bungeni akizungumza kinachomkera na kumfurahisha lakini akipeleka ujumbe mkataa kwa umma na kwa watunga sheria.

Naam yapo mengi ambayo watu tunahisi..labda rais atazungumzia haya yafuatayo ni labda:

PA-- MANAKE AMEIPOKEA RIPOTI YA TUME ALIYOIAGIZA NA NDANI HUMO WAPAMBE WANASEMA CCM INATAJWA LAKINI KWA KUZUNGUKA SANA lakini unajua hii inapingana na nini hasa? Ni kuwa aliomba kuhutubia bunge kabla ya kupokea ripoti sasa sijui ni coincidence au alishaelewa vitu vinavyokwenda akasema njia ni hii hii.. wape salamu zao bungeni
SUALA ZA ZENJ-- WABUNGE WA ZANZIBAR WAMECHACHAMALIA HAKI YA KUWA TAIFA LISILO TAIFA NDANI YA JAMHURI YA MUUNGANO, NA MOTO UMESHIKA KASI KWELIKWELI.

MIGOMO YA WAFANYAKAZI-- HILI SASA LINATIBUA ZAIDI, MIGOMO SI DALILI NJEMA PAMOJA NA WALIMU KUSHIKISHWA KITU KIDOGO INAONEKANA KUWA MAMBO SI SHWARI

MPASUKA WA KISIASA ZENJ--HILI NDILO SUALA AMBALO ALIAZIMIA KABISA KULIFANYA AKIWA IKULU LABDA ANA YA KUSEMA KUHUSU HILI.
LAKINI PENGINE ANAKUJA KUTUPA TATHMINI YAKE YA KAZI KWA KIPINDI CHA MIAKA MIWILI

Vyovyote itakavyokuwa Rais kesho atakuwa na mambo mazito ya kuzungumza kwani pamoja na ziara zake za nje hizi na za ndani kuna maeneo alikuwa anaonekana kuwa mkali kigodo kutokana na watu kushindwa kujituma na viongozi kubweteka.Isije ikawa kesho ni kiama cha mambo wakati rais anajiandaa kuelekea ughaibuni kutekeleza majukumu yake ya kimataifa katika kijiji Dunia.

7 comments:

Mzanzibar 100% said...

Ama kweli nyinyi wadanganyika!!! Yaani mpaka leo hamjui usanii wa rais wenu. Ngoja niwadokezee atakachoongea kesho.

1.Atatumia dk 10 kutoa pole kwa wabunge na wananchi wa Tarime kwa kumpoteza mbunge wao Chahawangwe.

2. Atatumia dk 20 kueleza masikitiko yake kwa kuuwawa kwa maalbino, na atatoa agizo kwa wakuu wa mikoa,na wakuu wa wilaya kupambana na wauwaji wa maalbino (kama kawaida yake order nyingii)

3. Atatumia dk 10 kuwaelezea sababu za kupanda kwa gharama za maisha akihusisha kupanda kwa bei ya mafuta, hivyo wananchi muwe wastahamilivu.

4.Kuhusu report ya EPA atasema ndo amekabidhiwa juzi tu, anahitaji kuipitia kwa umakini ili wahusika wafikishwe mbele ya sheria,hivyo wananchi muwe na subra matunda yake mutayaona.(kama kawaida usanii, Utafkiri yeye ndo DPP) hapo atatumia dk 8 tu.

5 Kuhusu swala la zanzibar atasema kama alivyoagiza waziri mkuu, wanasheria wapande zote mbili wakutane na watoe ufafanuzi, kwani hata yeye mwenyewe hajui kwamba zanzibar ni nchi au si nchi, ataenda mbali zaidi kwa kudai kwamba wanaojuwa ni waasisi mwalim nyerere na Sheikh karume ambao wote ni marehemu, kama alivyosema mzeee mwinyi kwamba hajui, hata yeye hajui, Atasema tena mimi nimeingia madarakani wakati waasisi wote hawapo ntajuaje ikiwa mzee mwinyi wa awamu ya pili pia hajui???! Hivyo kuwatuliza munkar wazenj atasema wasubir uamuzi wa wanasheria. (atatumia dk 15)

6. Kuhusu muafaka, atasema bado CCM inafanya juhudi za kuwaita CUF kwenye meza ya majadiliano ili wamalize mtafaruku, na anamatumaini watafikia muafaka wananchi wawe na subra. (dk 7 tu)

7 Atasema Ahsanteni sana kwa kuniskiliza, atapeana mikono na wabunge na mafisadi wengine, kisha huyooo ataingia kwenye benz lake la bei mbaya (new model) ataelekea ikulu ya chamwino na mkewe!

8 Wadanganyika watashangiria he he he huyu ndo rais bwana, watangoja 2010 watapewa t-shirt na kepu na pilau watapiga tena kura kwa CCM.

Anonymous said...

Mzanzibar 100% unaweza ukawa sahihi manake JK kwa longolongo hajambo!

Anonymous said...

Blah blah ni zile zile.

Anonymous said...

duh, mjomba hapo juu unamjua JK kweli kweli. jamaa ni msanii mpaka mwisho, wenyewe tunamuita "muuza sura". with this kind of culprit we aina gona nowhere. we need someone like kagame who can move bongoland

Anonymous said...

Jamani Beda kalala au anatunga sheria?
Bongo pix

chesi said...

Mzanzibar 100pc, PLEEAASE, TAKE FIVE!! YOU ARE GOOD!!!

Anonymous said...

kweli sisi ni wadanganyika,yaani huyu fala.unreliable and untrustworthperson,ndio wa kumsikiliza?alikuja na sera ya kasi mpya.mpaka leo hii kazi yake ni kutalii tu kama christopher columbus.leo hapa kesho kule,huyu jamaa si mtu mkweli.ni mmoja wa mafisadi,na mfano wake tayari tumeshauona,anamuaandaa hata mwanae ridhwani kikwete aje kua mbunge wa chukua chako mapema,alafu yeye ni jopo la mafisadi,akiwatumia wadosi katika kuhujumu nchi yetu..mshauri wake mkubwa ni dostum aziz,mwenye asili ya iran,hivi niandikavyo wairan wengi wamepewa ardhi nchi.na kikwete ana share katika kampuni hizo.kwa hiyo mwizi hawezi kumchukulia hatua mwizi mwenzie,huyu hataleta maendeleo wala mafanikio ya mlala hoi mtanzania.ni msanii fulani tu.anyway wadanganyika mlichagua eti sababu ni handsome,sasa kuleni huo uhandsome wake ,bila maendeleo..na mwanchi kupata huduma bora,nga'nganieni huo uhandsome wake..kwa udanganyika wetu....