Sunday, August 03, 2008

Mbwa KaziniWadau, kuna mzungu kaleta haka kajibwa aina ya Daschund kazini. Hivyo vijibwa ni wadogo na warefu kama sauseji. Basi ni lazima umshabikie mbwa wa watu kama vile mtoto wake. Unasema "oooh, ahhh, nice dog!" kusudi usionekane mbaya. Hata inabidi kucheza naye kidogo. Kajibwa kalikuwa kana bweka na kana cheza na mpira kake. Alivyochoka na mpira alianza kuila na vipande vili zagaa kwenye kapeti. Hakuna alityelalamika. Wanasema, "Your dog is so cute!" DOH! Lakini umelete mtoto na aanze kulia mle au kukimbia inakuwa balaa wanakuona mbaya!

8 comments:

Mamdogo said...

Da chemii umenikumbusha, hapaa holland kuna siku kaka mmoja alipata ajali ya baiskeli alikuwa kwenye mwendo wa kasi kwenye taa mtu akakatisha mbele yake ghafla kumkwepa akaanguka, alivunjika mkono pale pale hakuna mtu aliyemjali wala kumsaidia.
Sasa siku hiyo tuko kwenye mataa hapo hapo, mbwa alikuwa amebebwa kwenye trela ya baiskeli, ile trela ikagongwa na mbwa akaanguka jamani....nadhani dunia ilisimama kwa sekunde kadhaa, watu walivyotoka kwenye butwaa wote wakamkimbilia mbwa, taa haziendi, watu hatuvuki, kila mu anahangaika kumpeti mbwa, kumrudisha kwenye trela mwenye mbwa analia nikachoka....yaani mbwa ana thamani kuliko mtu.....mi mpaka sasa sielewi.

Anonymous said...

Ungejifanya bahati mbaya, ukapiga teke! Halafu unaanza kulalamika "jamani lol, pole mbwa wetu". Hata mimi nipo hapa UK mizungu inaniudhi kweli, yaani mpaka inabusu mijibwa, kweli majuu hamnazo!

Anonymous said...

UMENICHEKESHA BASI HUKU UK NDIO ZAO YAANI MBWA WANAMTHAMINI SANA LAKINI MTU UNAWEZA UKAWA NA MTOTO AKAMWAMBIA MZUNGU HELLO ZUNGU LIKACHUNA,BASI WENYEWE WANAPENDA KUSEMA YOUR DOG IS LOVELY,OOH SUCH A CUTIE.

Anonymous said...

Siku nyingi piga kelele kuonyesha unamwogopa, wakikuuliza waambie kwetu mbwa ni adui na hawako friendly. Tehetehetehete

Anonymous said...

Wengine wanayavisha mpaka chupi, duh hawa kweli punguani. Hapa uingereza uthamani unajipaga kama ifuatavyo. Moja mtoto, mbili mwanamke, tatu mnyama, nne mwanaume(Muingereza), tano mtu yoyote mweupe (Asians, Polish, Chinese etc) sita na mwisho, ........ unajua sisemi. Lakini manaume yao yanawapenda dada zetu eti watamu na wana joto! Kwi kwi kwi!

Anonymous said...

ni kweli hata hapa uingereza kuna baadhi ya watu huwa wanakuja na mbwa kazini, mi huwa nawakwepa sijawazoea kwa kweli!
nadhani pia huwa wanajisikia vibaya; ni kitu ambacho sikukizoea kule kwetu -mbwa ni kwa ajili ya ulinzi nje ya nyumba na sio hapa mbwa anaishi ndani kama binadamu na bajeti yake ni kubwa kuliko bajeti za watu kule kwetu afrika.

Anonymous said...

Duh! anony hapo juu, sijawahi kuona mzungu hata mmoja anayependa wanawake weusi. Ingawa wapo wachache wanaopenda kuwa***** tuu just kwa experience.

Anonymous said...

Wewe kuna wazungu wanapenda sana wanawake weusi. Mpaka wanaoa kabisa!