Friday, August 08, 2008

Mzungu Atishia Kumwua Obama!


Watu wamekuwa wakihofia maisha ya Senator Barack Obama, ambaye anagombania urais wa Marekani. Kisa historia ya ubaguzi hapa Marekani. Kumbuka mauji ya Martin Luther King Jr. na Medgar Evers. Wazungu wamekwishaua weusi ovyo hapa Marekani tena wala hawachukuliwa hatua yoyote. Wakati mwingine hata mapolisi walikuwa wanashiriki katika mauji hayo.
Leo tumesikia mwanaume mwenye miaka 22 kutoka Maine amekamatwa huko Florida. Habari zina sema kuwa Raymond Hunter Geisel, alisema kuwa hatawezi kustamili mtu mweusi (n-word) kuwa rais wa Marekani, hivyo atamwua. Alikutwa na silaha aina mbalimbali kwenye chumba cha hoteli huko Florida.

Wadau, inabidi tumwombea Obama usalama! Maana wazungu wenye siasa kali (white supremacists) bado wapo hapa Marekani.

Kwa habari zaidi someni:

1 comment:

Anonymous said...

Tunamwomba Mungu amlinde Senator Obama na familia yake maana wako hatarini! AMEN/AMIN.